Kushiriki Maziko ya Kafiri
بسم الله الرحمن الرحيم
Swali:
Hukmu ya muislamu kushiriki ibada za kumzika ndugu yake kafiri na Mtume (S.a.w) alifanyaje wakati wa kumzika ami yake?
Jibu:
Inajuzu kwa muislamu kushiriki katika kumzika kafiri katika jamaa zake wa karibu, kwa yale yaliopokelewa na Abudaud na wengineo, toka kwa Ally (R ) amesema : “Nilimwambia Mtume (S.a.w): Hakika ami yako ni mtu mzima aliyepotea na amekufa, akaniambia (Nenda kamfukie Baba yako, kisha usiongee chochote mpaka uje kwangu) nikaenda kumfukia na nikaja kwake Mtume (S.a.w) akaniamrisha nikaoge na akaniombea dua” Hadithi hii iko wazi kwamba Mtume (S.a.w) alimuamrisha Ally akamzike baba yake abi twalib nayeye alikuwa ni mshirikina, ikaonyesha kuruhusiwa kufanya hivyo…
Hii ikiwa kuzika ni kwenye mchanga, ama ikiwa si katika mchanga basi si ruhusa kwa muislamu kushiriki katika jambo hilo, kwa sababu Allah amesema :
{ مِنْهَا خَلَقْنَاكُمْ وَفِيهَا نُعِيدُكُمْ وَمِنْهَا نُخْرِجُكُمْ تَارَةً أُخْرَى }
Kutokana na Udongo Tumekuumbeni, na ndani ya Udongo Tutakurudisheni, na kutokana na huo udongo tutakutoeni kwa mara nyingine
Ama ikiwa si katika yale yalioelezwa na uislamu, kama vile kuchomwa moto, basi hairuhusiwi kwa muislamu kushiriki katika ibada hizo za maziko.
Ama kuhusu alifanyaje Mtume (S.a.w ) wakati wa maziko ya Ami yake, ni kwamba yeye Mtume (S.aw ) hakushiriki katika maziko yake na alimtaka Ally akamzike baba yake, na pamoja kwamba Mtume (S.a.w) hakushiriki katika maziko, lakini alimuamrisha Ally akamzike Baba yake, hii inaonyesha kuruhusiwa kwa Jambo hilo.
Na jambo muhimu kulitaja hapa ni kuwa hukmu ya kushiriki katika ibada za kimazishi za makafiri kama vile swala za maiti na mfano wa hayo, haifai kushiriki katika ibada hizo kwa maiti wa makafiri kwa namna yoyote ya ukaribu uliopo, nayo ni kwa sababu “La Ilaaha Illa llah” ambayo ndio alama ya uislamu ina maana ya kwamba hakuna ambaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, na kwamba swala na ibada za makafiri kwa mauti zao ni katika mambo ya kiibada yaliokinyume na “La Ilaaha Illal Llah” kwa hiyo haifai kwa muislamu kushiriki katika swala zao za maiti au kushiriki katika maombi na misa zao kwa namna yoyote ilio ya ukaribu wao.
Na pia kuna namna nyingine katika mas’ala haya kama vile kuosha muislamu maiti ya jamaa yake kafiri na kufuata jeneza lake, mimi nakunukulia rai za wanafiqhi katika mas’ala haya mawili kwa ajili ya kupata faida .
1 – Kushiriki katika kuosha maiti wa makafiri
Wamekubaliana wana Fiqhi kuwa si wajibu kwa muislamu kumuosha kafiri… ama upande wa kujuzu kulifanya hilo wametofautiana wana Fiqhi wa Madhehebi wapo walioruhusu na wapo waliozuia…. Na nakunakilia rai zao ili ufuate katika mas’ala haya rai ya madhehebi ambayo utakinaika nayo :
A – Kwa Mahanafi : Ikiwa maiti ya kafiri ana ndugu zake wa karibu waislamu, na wala hakuna wa kulifanya hilo katika watu wa dini yake na mila yake, basi ni ruhusa kwa ndugu zake waislamu kumuosha, kama wapo wa dini yake basi muislamu atawaachia wao wamuoshe.
B : Madhehebu ya Shafii: Ni ruhusa kwa waislamu na kwa wengineo kuwaosha makafiri, na ndugu zake makafiri wenzie wana haki zaidi kuliko ndugu zake waislamu.
C : Madhehebu ya Maliki na Hanmbali : Muislamu hamuoshi kafiri hata kidogo, sawa ni ndugu yake wa karibu au si ndugu yake wa karibu .
2 – Kushiriki Kusindikiza Mauti wao baada ya kukamilisha Ibada zao:
A – Mahanafi : Imepokelewa kwao kwa upande wa muislamu kwenda kusindikiza jeneza la ndugu yake kafiri au jamaa yake wa karibu kwamba inaruhusiwa, lakini awe mbali na asiwe karibu nao … na hayo yamekuja kwenye kitabu “Durarul Hukaami Fii Sharhi Ghuraril Ahkaam” Mtunzi wake ni Muhammad Bin Faraamirzi Bin Ally Mashuhuri kwa jina la Mula Khasru aliekufa Mwaka 885 Hijria (…. Na afuate Jeneza kwa Mbali, hii kwa Yule ambaye ukafiri wake si wa Kuritadi….. )
B – Kwa Maliki: Asibebe muislamu Jeneza la kafiri na wala asilisindikize na wala asimzike…katika kitabu “Annawadiru Wazziyaadaat Alaa Maa Fiil Mudawwanah Min Ghairihaa Minal Ummahaat” Kilichotungwa na Abdallah Bin AbdirRahmaani Alqairawaaniy Almaalikiy Aliyefariki 386 Hijria yamekuja haya yafuatayo : “Amesema Ibn Rajabu: Asibebe Muislamu Jeneza la Kafiri na wala asilisindikize na wala asimzike…. Na hata kama Muislamu atafiwa na Jamaa yake kafiri kama vile Baba, Mama,Kaka nk, basi hakuna ubaya wa Kishiriki na kusimamia jambo lake na atajiweka mbali na watu wa dini yake, kama watatosheleza na kukawa na usalama wa kutokupotea atawaacha wamzike, na kama ataogopea hilo basi awe mbele yao kwenye kaburi lake na kama hakuogepea kupotea kwake na akapenda kuhudhuria maziko basi awe mbele ya jeneza lake huku akijitenga nalo na wale wanaolibeba, Imepokelewa Kwa Mtume (S.a.w ) ameruhusu hivyo. Amesema Atwaa: Na yule ambaye mama yake Mnaswara akafariki, ana haki ya kumkafini na kusimamia maziko yake na akasindikiza Jeneza huku akijitenga na mambo yao, Amesema Ibn Rajab: Kupanda na kutembea vyote ni sawa sawa katika hilo. Amesema Malik: hakuna ubaya kusimamia Msiba wake wote kisha awakabidhi watu wa dini yake, na wala asifuate Jeneza Isipokuwa akichelea Kupotea, basi atatungulia kwenye kaburi lake na wala asiingie humo isipokuwa itakapokuwa hakuna wa kulifanya hilo.
C – Kwa Mashafii : Inajuzu kwao kufuata Jamaa wake wa karibu kafiri….Imekuja kwenye kitabu “Almajmuu Sharhel Muhadhab” cha Mtunzi Zakariyyah Muhyid diin Yahya Bin Sharafu Annawawi aliekufa mwaka 676 Hijria” ( Amesema Imam Shafii katika Mukhtasar Almzani na Wafuasi wake kuwa Inajuzu kwa Muislamu kufuata Jeneza la Jamaa yake wa karibu Kafiri….)
D – Kwa Mahanbali: Inajuzu kwa Muislamu kufuata Jeneza la Mzazi wake Kafiri, lakini iwe Mbele ya Jeneza na wala sio nyuma yake….Imekuja katika Mughni ya Ibn Quddaamah Almaqdisy aliyekufa mwaka 620 Hijria, amesema Ahmad (kuhusu Myahudi au Mnaswara alikufa na ana mtoto Muislamu, na apande kipando na aende mbele ya Jeneza…)
Ndugu yenu Atta bin Khalil Abu Rashta
Maoni hayajaruhusiwa.