Vita Vya China Dhidi Uislamu Mashariki ya Turkestan Vitamalizwa Pekee na Khilafah Rashidah

بسم الله الرحمن الرحيم

Ofisi Kuu ya Habari Hizb ut Tahrir imeandaa kampeni yenye kuonyesha uhalisia wa mzozo baina ya China na Waislamu wa Turkestan Mashariki ambao walianza kusibiwa na mauwaji (chinese massacre) tangu mwaka 1863. Zaidi ya waislamu milioni moja wa Uyghur waliuwawa katika mapambano yaliyotokea mwaka 1949 wakati utawala wa kiukomunist/ujamaa  uliposhika hatamu  chini ya Mao Zedong walipoingia katika ardhi yao na kuuvunja uhuru waliokuwa nao kwa kuikalia ardhi yao. Waislamu walipungua katika miji ambapo walikimbilia katika vijiji vya ndani sana ndani nchi ya china. Lakin uvamizi huo na kuuwawa huko hakukuwafanya waislamu wa Uyghu kujisalimisha chini ya serikali ya China, walianzisha vuguvugu la mapinduzi mnamo mwaka 1933 na mwaka 1944, na vuguvugu hilo likaendelea katika mji huo dhidi ya uvamizi wa China kama ilivyokuwa mwaka 2009.

Uislamu ndio sababu msingi inayowajaza chuki wachina dhidi ha waislamu wa Uyghur. Misikiti ni moja ya vilengwa vikuu ambapo Uchina inamwaga sumu yake yakuusambaratisha uislamu ndani ya Uyghur, Uchina imeivunja misikiti inayokadiriwa 25,000 mwaka 1949, na misikiti 500 tu ndo iliyobakizwa.
Uchina ya leo imeacha kutumia falsafa za kijamaa/komunist katika upande wa uchumi lakin inaendelea kufuta athari zozote za kidini/uislamu katika jamii na vijana ambapo kufanya hivyo nikukubaliana na sera za kijamaa katika upande mwengine. Hii ndio imekuwa sera ya uchina ndani ya miji katika nchi hiyo.

Licha ya yote hayo wanayofanyiwa waislamu wa mashariki wa Turkestan wanazidi kusubiri na kuwa na msimamo juu ya dini yao kiasi cha kupelekea kuanza kushamiri na kuenea nuru ya uislamu pembezon mwa mji. Vitisho na matukio ya maangamizi yanayozidi kuendelea yanaufanya kuwa ni mji wakitofauti kulinganisha na miji mengine isio na waislamu. Hii ni kwa sababu ya kukosekana kwa amani katika mji huo kunakosababishwa malipuzi ya mabomu pamoja na vitendo viovu vinavyofanya na serikali ya Uchina dhidi yao na msimamo wao wa kutoka kujitoa kutoka jamhuri ya watu wa China. Hatimaye kuwa ndio sehemu ya upenyo (sehem dhaifu) ndani ya serikali. Kutokana na hivyo China ikawa inafuafutilia maisha ya waislamu wa Uyghur kwa lengo la kuwadhuru na kuvizuia vyombo vya habari kufuatilia maovu yafanywayo na serikali pamoja na kamatakamata ifanywayo nyakati za giza katika miji. Pia serikali ya Uchina imekuwa ikawafatilia waislamu wa Uyghu waliotoroka kutoka mji huo na wenye uwezo Wakupaza sauti zao mbali ya Uchina, imeweza kuwakamata wengi katika hao kwa msaada wa watu wa usalama katika mataifa mengine (internation security channel) kama Pakistan na nchi za Asia ya kati, watu hao walikamatwa kwa tiketi ya ugaidi.

Kinachoumiza zaidi ni kwamba ukatilii huu wafanyiwao waislamu wa Uyghur, unatekelezwa mbele ya macho na masikio ya mamilioni ya waislamu duniani bila ya wao kukemea chochote juu ya uovi huo. Hii ni kwa sababu hawa mamilion ya waislamu wametawanyishwa baina yao na mipaka ya kijiografia na hawajaunganishwa pamoba na serikali ya kiislamu. Kwa kukosekana huko serikali ya kiislamu kuna wajibisha kila muislamu muweza kufanyakazi ya kuirejesha na kumweka khalifah atakayesimamia mambo ya ummah kwa uadilifu na ambaye atakuwa kinga na ngao ya waislamu ambapo nyuma yake watu watapigana. Kama ilivyo elezwa katika sahih bukhari kutoka kwa Abuu hurairah(r.a), Mtume wa Allah(s.a.w) amesema:

«وَإِنَّمَا الإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ»

“Hakika kiongozi ni ngao, mtapambana nyuma yake na kujikinga kwayo”.

Kwa sababu hiyo China na makafiri wengine hawatothubutu kuwatesa waislamu mahali popote duniani kwa sabab watafahamu chuki na uovu wao dhidi ya waislamu utajibiwa/utarudiwa vikali.

Hakika Allah(s.w) ni mkali na mwenye nguvu.

##Khilafah_Liberates_EastTurkestan

http://hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/hizbuttahrir/16793.html

Maoni hayajaruhusiwa.