Je, “Hesabu” Imeanza Kumaliza Utawala wa Dola Juu ya Uchumi wa Kiulimwengu?

Swali
Majaribio yameibuka katika baadhi ya nchi, hususan Urusi, China na Muungano wa Ulaya, ili kubadilisha dola kwa sarafu nyengineyo katika miamala ya kimataifa. Makubaliano hata pia yamefanywa ili kukabiliana  na sarafu za nyumbani za baadhi ya nchi, kama vile makubaliano ya Urusi pamoja na India mnamo 31/10/2018, ya kuuza makombora aina ya S-400 kwa sarafu ya Urusi. Na makubaliano yake na Uturuki mwezi mmoja uliopita ya kutumia sarafu za nchi mbili hizi katika biashara ya makombora sawa na hii. Katika mkutano wa Erdogan wa nchi zinazo zungumza lugha ya Kituruki…

China imetangaza kuwa italipia uagizaji wake wa bidhaa za mafuta ya Iran kwa “petro-yuan” na Benki Kuu ya China ilitia saini makubaliano kati ya pande mbili ili kubadilishana sarafu ya nyumbani pamoja na ya mwenzake nchini Japan, bilioni 200 za yuan ($29 bilioni) kwa badali ya yen trilioni 3.4 ($31 bilioni). Je “hesabu” ishaanza kumaliza utawala wa dola juu ya uchumi wa kiulimwengu?

Jibu

Ili jibu hili liwe wazi, uhalisia wa msimamo wa dola katika uchumi wa kiulimwengu ni lazima ufafanuliwe:

Kwanza, hadhi ya dola ilianza kuibuka kupitia Makubaliano ya Bretton Woods mnamo 1944, pindi Amerika ilipo lazimisha dola na utawala wake katika mkutano huo, kwa sababu ilikuwa ndio mada iliyokuwa haikuathiriwa katika vita vya dunia … Hivyo basi mfumo wa fedha uliidhinishwa ambapo nchi kuu kumi zilizoendelea kiviwanda zilikubaliana kuweka bei maalumu kwa sarafu zao za nyumbani kwa msingi wa dola ya Kiamerika. Zaidi ya hayo, Amerika ilikubali kuiunganisha dola ya Kiamerika kwa msingi wa dhahabu ($35 kwa kila pauni) na kisha ubadilishanaji wa dola zilizo peanwa na benki kuu kwa bei makhsusi ya dola iliyo unganishwa kwa dhahabu. Hifadhi ya dhahabu nchini Amerika wakati huo ilikadiriwa kuwa thuluthi mbili, na ile ya ulimwengu uliosalia ilikuwa thuluthi moja … lakini kuendelea kudhoofika kwa mizani ya kibiashara ya Amerika kutokana na athari ya matumizi ya nje yalipelekea kudhoofika kwa hifadhi ya dhahabu. Kati ya 1961 na 1970, ilishuka hadi karibu dola bilioni 5. Ili kuhifadhi hazina ya dhahabu ya Amerika, Raisi Nixon aliamua mnamo 1971 kusitisha ubadilishaji wa dola kwa dhahabu, akitangaza mwisho wa mfumo huo uliounganisha dola kwa dhahabu.

Utawala wa Nixon kisha ukakabiliana na mabadiliko haya ya kifedha kupitia msururu wa makubaliano na  Saudi Arabia mnamo 1972 hadi 1974, na kuanzisha ile inayoitwa “petro-dola”, ukizipa nchi za kigeni sababu nyengine ya kuzikinaisha ya ukusanyaji na utumizi wa dola kwa sababu ya haja yao ya mafuta ambayo yametiwa thamani kwa dola kwa mujibu wa makubaliano na Saudi Arabia, mzalishaji mkubwa zaidi wa mafuta duniani. Saudi Arabia pia ilikubali kurudisha upya mzunguko wa mabilioni ya dola za Kiamerika wa hifadhi ya mafuta kupitia watengezaji zana wa Kiamerika, miundo mbinu na ununuzi wa bondi za Hazina ya Amerika. Kufikia 1977, kwa uchache asilimia 20 ya bondi zote za Hazina ya Kiamerika ng’ambo zilikuwa mikononi mwa Saudi Arabia … endapo mafuta yataongezwa juu ya dhahabu, ambayo pia yametiwa thamani kwa dola, hivyo basi nchi zilikuwa makini kupata dola. Mgao wa hifadhi ya pesa taslimu za dola katika benki kuu duniani ulikuwa ni takriban asilimia 71 hadi 2000, lakini ukashuka baada ya mwaka huu hadi asilimia 62, vilevile asilimia 40 ya deni la kiulimwengu limetawaliwa kwa dola.

Pili: Leo, dola ya Kiamerika inatawala miamala mingi ya kimataifa. Hii imesababisha soko kubwa la kubuni kwa dola ya Kiamerika, linalotafautisha dola ya Kiamerika kutokana na kila sarafu ya kinyumbani ya nchi. Dola imekuwa muamuzi katika miamala iso hesabika yenye thamani ya zaidi ya trilioni 5.4 kwa siku, isiyo husiana na bidhaa au huduma za Kiamerika …

Kinacho shangaza ni kuwa dola inawakilisha asilimia 84.9 ya miamala ya ubadilishanaji wa pesa za kigeni, mbali na miamala ya kibiashara ya Amerika yenyewe kuwa chini ya nusu ya mgao huu, kwa sababu nchi zisizo za Kiamerika huamiliana na dola katika mambo yao ya kibiashara! Nguvu ya kiuchumi ya dola imekusudia kuwa Amerika ina uwezo wa kuliadhibu sio tu taifa lililo lengwa kiuchumi na kifedha; bali pia kuzishajiisha nchi nyenginezo kutokana na kufanya biashara na nchi iliyo lengwa. Amerika ina uwezo wa kufikia hatua hii kali kupitia mfumo wa SWIFT: (Jumuia ya Kiulimwengu ya Mawasiliano ya Kifedha baina ya Mabenki).

Ni nidhamu ya malipo kwa dola. Kwa kuwa dola ndio sarafu ya hazina ya kiulimwengu, SWIFT husahilisha
nidhamu ya dola ya kimataifa. Nchi zote ulimwenguni hulipia miamala kupitia kwayo, zikihakikisha kuwa
miamala yote kati ya pande mbili imejengwa juu ya dolari. Kwa mfano, Urusi na China haziwezi
kubadilishana bidhaa na huduma kupitia pesa zao za nyumbani isipokuwa miamala ya dola ya Kiamerika
ilipwe kupitia SWIFT. Amerika yaweza kutumia nihamu hii kulazimisha vikwazo vikali vya kiuchumi. Chini ya nidhamu hii, Amerika ilipiga marufuku, kati ya 2014 na 2015, benki nyingi za Urusi kutokana na SWIFT pindi mahusiano baina ya nchi mbili hizo yalipo zorota. Mnamo Novemba 2018, Amerika ilizindua tena vikwazo vikali dhidi ya Iran kwa kutumia SWIFT. Kampuni nyingi za Ulaya zilikataa kutekeleza biashara zao na Iran kwa kuiogopa Amerika.

Yote haya, kama tulivyo taja awali, ni kwa sababu dola ndio sarafu ya hazina ya kiulimwengu: hisa ya dola
katika hazina hiyo ya benki kuu 146 kote ulimwenguni ilifikia asilimia 64 ya hazina zote za sarafu za benki hizo mwishoni mwa mwaka jana. Sarafu ya euro ilichukua nafasi ya pili kwa asilimia 20, huku mchango wa yen ya Japan na pauni ya Uingereza ukiwa ni asilimia 5. Hii ni pasi na kuzungumzia kuhusu yuan ya China, ambayo hazina zake katika benki hizi zilikosa kuzidi dola za Kiamerika bilioni 108, ambayo ni chini ya asilimia 1. (www.alquds.co.uk 19/8/2018)

Tatu: Katika kuangazia hili, nchi za kiulimwengu zilizo nanguvu na umuhimu zilianzisha njia mbili ili kupunguza athari ya dola. Ya kwanza ni msimamo wa Ulaya mnamo 1999, ambapo sarafu ya euro ilitumika rasmi katika biashara, mnamo 2002 katika ushindani na dola. Hii ni kutokana na nguvu ya uchumi wa Ulaya na ujasiri wao katika uwezo wa kushindana. Ya pili ni kupitia nchi, kama Urusi na China, ambazo juhudi zao zilichelewa kuzuia utawala wa dola; hii ni kwa sababu ya kukosa kwao uwezo wa kushindana wakati huo (hadi kuzinduliwa kwa euro) hadi mgogoro wa kifedha wa 2008. Zilihofia kumomonyoka kwa hazina zao za dolari na kupotea kwa thamani yake. Zilijiunga na nchi za kale za Ulaya katika kupunguza utawala wa dola. Kwa kuwa China imekuwa na uchumi mkubwa ulimwenguni, juhudi zake kimataifa zilianza kuathiri utawala wa dola.

Hivyo basi, mgogoro wa kiuchumi wa 2008 ukawa ni mwito wa uamsho kwa nchi ili kufikiria kuhusu dola kama natija ya mgogoro huu. Lakini kilichoifanya hatua hii kuwa ya haraka ni uchokozi wa Trump na vikwazo. Sera mpya iliyo fuatwa na utawala wa Raisi Trump imeharakisha hamu ya dola nyenginezo kuu kuzuia utawala wa dola ya Kiamerika kiulimwengu. Sera ya Raisi Trump ilibeba kwa jeuri mwito wa “Amerika Kwanza”, ingawa tawala zote za Amerika kwa yakini zilikuwa zikifanya kazi kwa ajili ya maslahi ya Amerika, lakini utawala wa Trump uko karibu na kutotambua maslahi ya nchi nyenginezo. Trump aliitaka Ulaya kulipia kuanzia nyuma ulinzi wa kijeshi wa Amerika na kuanzisha cheche kali zilizo tishia kuwasha moto wa vita vya kibiashara na China.
Alizitaka Japan na Korea Kusini kulipia ulinzi kutokana na makombora ya Korea Kaskazini. Pindi Raisi Trump
alipo lazimisha vikwazo juu ya Iran, vilivyomjumuisha kila anayetumia dola kununua mafuta ya Iran, na kwa sababu China kwa sasa ndio muagizaji mkubwa zaidi duniani wa mafuta, vitendo vya Trump viliipelekea China kuchukua hatua kukomesha utumizi wa dola, hususan kwa kuwa imo katika vita vya kibiashara na Amerika. Hivyo basi, mnamo Machi 2018, soko la hisa la Shanghai lilianzisha mikataba ya wazi ya hisa kwa wawekezaji wa kigeni. Katika mkataba huo, mkataba wa mafuta, ulitawaliwa na sarafu ya yuan ili iwe hasimu kwa Brent na WTI zilizo  simama kwa msingi wa dola, ambazo zinatumika kama viwango vya sasa.

Kwa hivyo mgogoro wa kifedha wa 2008, mmuliko wake juu ya uchumi wa nchi nyingi na athari yake kwa
mgogoro huu, ikifuatiwa na hisia ya kuhifadhi ya Trump, vita vya kibiashara, na sera za kifedha na kiuchumi … yote yameharakisha miondoko dhidi ya utawala wa dolari.

Nne: Hivyo basi, vitendo hivi vimechochea baadhi ya nchi, hususan zile zenye nguvu za kipekee, na wakati
mwengine hata kupita nchi zilizo pambizoni mwa nchi zenye nguvu, ingawa harakati imara na zenye ushawishi ni zile za kutoka kwa dola huru, kwa sababu ushawishi wa dola hizo zilizo izunguka Amerika uko thabiti na kwa lengo maalumu na kisha kusita kwa sababu haziwezi kupinga upinzani imara wa Amerika, maadamu zinazunguka katika duara lake, na tutaregelea vitendo vya nchi hizi:
1- Vitendo vya nchi huru:
A- Urusi: Mnamo 2009, Raisi wa Urusi Medvedev alipendekeza “sarafu mpya ya kiulimwengu” katika
kongamano la G8 jijini London kama sarafu badala ili kubadilisha dola. China, Urusi, India, Uturuki na
nchi nyenginezo zinazo zalisha mafuta hivi majuzi zilikubaliana “kufanya biashara zao zote na miamala yao
yote ya uwekezaji kwa sarafu yao wenyewe.”

Lakini licha ya yote haya, bei ya dhahabu na mafuta ghafi imesalia kuwa kwa dola! Taarifa za kukariri za Urusi za kubadilishwa dola kwa sarafu nyenginezo za kitaifa na kupokea bei ya mafuta ya Urusi kwa sarafu nyenginezo kuliko dola ni kutokana na vikwazo vya Amerika juu ya Urusi baada ya uvamizi wake na kuikalia kwake Crimea na Mashariki mwa Ukraine mnamo 2015. Vile vile ni natija ya uchunguzi juu ya uingiliaji wa Urusi wa uchaguzi wa Amerika wa 2016.

Amerika imeongeza zaidi vikwazo vyake dhidi ya Urusi tangu 2015, na bunge la Congress limepanua
zaidi vikwazo, kwa kutumia “Kifungu cha Sheria cha Kupambana na Maadui wa Amerika kupitia vikwazo,”
kilichotungwa mnamo Agosti 2017, na kulazimisha vikwazo vikali juu ya Urusi. Hatua hizi zilikuwa kali dhidi
ya Urusi, na hili lilikata fungamano la benki kuu nyingi za Urusi na dola, ikipelekea kushuka kwa asilimia 18 ya ruble (sarafu ya Urusi) dhidi ya dola …

Yote haya huku Urusi ikitumia dola katika asilimia 58 ya deni lake, yaani, inakopa karibu nusu ya mikopo yake kwa dola, hivyo Urusi ikaanguka ndani ya matatizo yaliyo isukuma kujaribu kupunguza matumizi yake ya dola, na kujiweka huru kifedha, kiuchumi na kibiashara kutokana
na dola.

Putin alisema katika hotuba mbele ya dola ya Duma:
“Ni sharti tuimarishe ubwana wetu wa kiuchumi … biashara ya mafuta katika soko la hisa iko kwa dola, na bila shaka tunafikiria namna ya kuuondoa mzigo huu …” aliendelea. “Tumekuwa limbukeni katika miongo iliyopita, tukitaraji kuwa kutakuweko na kujitolea katika misingi iliyotajwa katika biashara ya kiulimwengu na uchumi wa kiulimwengu, na sasa tunaona kuwa sheria za Shirika la Biashara Duniani (WTO) zimekiukwa mno, na kuna vizingiti vimewekwa kwa makadirio ya kisiasa, wanaviita vikwazo” (Duniya Al-Watan, 9/5/2018). Kisha Urusi kidogo kidogo ikapunguza umiliki wake wa bondi za Hazina ya Amerika ambazo zilikuwa zimefikia kileleni mwake mnamo 2008 kwa dola bilioni 223, hadi ilipo kuwa karibu bilioni mia moja mwishoni mwa mwaka jana.
Kama natija ya vikwazo vya Amerika juu ya Urusi, Urusi imeachana na nyingi ya bondi zake katika miezi ya Aprili na Mei 2018, na Urusi sasa ina dola bilioni 14.5 za bondi hizo …

Lakini, ruble ya Urusi haiwezi kuchukua nafasi ya dola, kwa sababu ukosefu wa imani katika ruble haiisaidii
kuzisukuma nchi zilizo na nguvu kusimama nayo. Hii ni kwa sababu nchi nyingi ulimwenguni hazitaki kununua ruble kwa kuwa ina mwanya mkubwa wa kupanda na kushuka katika masoko ya fedha, na kimsingi ni kwa sababu ulimwengu hauna imani na ruble ya Urusi kama hifadhi ya fedha. Kile ambacho Urusi yaweza kufanya zaidi ni kuzisukuma baadhi ya nchi kulipia ununuzi wa kawi yao ya Urusi kwa ruble, lakini fedha hiyo ya Urusi haiwezi kuchukua nafasi ya dola … msemaji wa Putin Dimitry Peskov alisema katika mahojiano na Runinga ya Rossiya.

“Nchi nyingi zaidi, sio tu upande wa Mashariki lakini pia Ulaya, zinaanza kutafakari njia za kupunguza utegemeaji wao wa dola ya Amerika … Ghafla zimetambua: A. haiwezekani, B. ni lazima ifanywe, na C. jiokoe nafsi yako kama unaweza, yanapaswa kufanyiwa haraka iwezekanavyo.” “Kufutilia mbali dola kwa kiasi fulani
kunawezekana, lakini sio kuhusu ima unataka kutoka eneo la dola, bali ni ipi badali kisha: euro? yuan?
Au Bitcoin?” “Kila mojawapo ya machaguo haya lina gharama zake, ni sharti tupime gharama za kubakia
na dola na gharama za kutafuta msimamo mpya,” alisema Oreshkin, aliyekuwa makamu wa raisi wa
Benki Kuu ya Urusi (Financial Times, 3/10/2018). Yote haya yanaashiria kuwa maafisa wa Urusi wenyewe
hawajakinai kuwa ruble inatosha kuwa sarafu ya kiulimwengu badala ya dola!

B- China: China inaifanya yuan yake kuwa sarafu mshindani imara wa kiulimwengu, lakini upeo wake
wa kisiasa wa kiulimwengu ni mwembamba, hivyo basi kuathiri upeo wake mwembamba wa kiuchumi
wa kimataifa katika upande wa ushindani na mzozo na Amerika. Hivyo basi, haikulazimisha sarafu yake
kiulimwengu katika biashara na masoko ya fedha licha ya ukubwa wa uchumi wake, lakini ikatabanni dola, na ikazikusanya kwa viwango vikubwa katika miaka ya hivi karibuni kati ya dola trilioni 3 na 4! Ingawa ilifanya majaribio ya kujiondoa kutoka katika taasisi za kifedha za Amerika, na kuunda jumuia ya kiuchumi BRIX pamoja na Urusi, India, Brazil na kisha Afrika Kusini. Ukubwa jumla wa jumuia ya BRIX ulizidi dola trilioni 15, sawia na asilimia 20 ya uchumi wa kulimwengu wa $ 74 trilioni … pia iliasisi benki ya maendeleo kwa ajili ya kufadhili na kukopesha (jumuia ya BRIC) mnamo Julai 2015 jijini Shanghai ikiwa na mtaji wa dola bilioni 50 hadi hatimaye kufikia dola bilioni 100 kama badala ya Benki ya Dunia, ingawa bado haikuachana na dola!

Pindi Raisi Trump alipo lazimisha vikwazo juu ya Iran na kuvifanya kumjumuisha kila aliyetumia dola kununua mafuta ya Iran, na kwa sababu China kwa sasa ndio muagizaji mkubwa zaidi wa mafuta ulimwenguni, tabia ya Trump ndio iliyoipelekea China kuchukua hatua ili kusitisha utumizi wa dola, hususan kwa kuwa imo katika vita vya kibiashara pamoja na Amerika. Hivyo basi, mnamo Machi 2018, Soko la Hisa la Shanghai lilianzisha mkataba wake wazi wa hisa kwa wawekezaji wa kigeni.
Mkataba huu, mkataba wa mbele wa mafuta, ulitawaliwa kwa yuan ili kushindana na mikataba ya Brent na WTI, iliyotawaliwa kwa dola, ambayo inatumika kama viwango vya sasa, hatua zote za juu ziko dhahiri na zaweza kuitingisha dola.

Kinachoidhibiti bidii ya China kuiondoa barabara au kuitingisha dola ni kule kutegemea kwake pakubwa juu
ya uchumi wa Amerika na dola. Kiwango cha biashara ya Amerika na China ni kikubwa mno kiko dola bilioni
500 kwa mwaka na sasa ina dola bilioni 1,170 katika bondi za Hazina ya Amerika (tovuti ya gazeti la fedha
la China la Xinhua 20/9/2018) chini kutoka dola bilioni 1,300 mnamo 2013, mmiliki mkubwa zaidi wa bondi
hizo. Hazina ya dola ya China iko kati ya dola trilioni 3 na 4 zilizo ongezwa katika usafirishaji bidhaa wa China duniani mnamo 2016, zenye thamani ya dola trilioni 2.1 na kuagiza bidhaa za dola trilioni 1.6 kwa mujibu wa Shirika la Biashara Duniani, ikiifanya kuwa nchi ya pili kuu kibiashara duniani baada ya Amerika …

Hivyo basi, uzito wa biashara yao katika dolari, ikiongezewa na bondi za Hazina, inawafanya kuchukua
hatua moja mbele na hatua moja nyuma katika kazi makini ya kuitingisha dola. Mafanikio ya Amerika katika
kuivutia China kwa biashara ya kimataifa kwa dola imeifanya China kuvutiwa zaidi na kutoitingisha dola.
Inajua kuwa itakuwa mwathiriwa mkubwa zaidi duniani wa mtingisho wa dola; hili linaisukuma kupunguza dori yake polepole na kwa uangalifu ili kuhifadhi rasilimali zake za dola na bondi. Na hata kama biashara yote ya China itakuwa kwa Urusi kando na dola, hili halitatui tatizo kwa sababu ukubwa wa biashara ya dola bilioni 120 kwa mwaka katika mielekeo yote miwili (Arabic China 23/9/2018) inabakia kufungika ikilinganishwa na biashara ya kiulimwengu, ambayo ni zaidi ya dola trilioni 20 kwa mwaka. Hivyo, China sio kakamavu kushinda Urusi na ina tahadhari zaidi katika kiu yake ya kuzuia utawala wa dola.

China inaonekana kutambua madhara ya kuamiliana na dola, katika upande wa uzito wa rasilimali zake za dola au katika upande wa bondi za Hazina ya Amerika, nk. Imekuwa nchi inayo nunua dhahabu zaidi duniani, akiba yake ya dhahabu imekuwa kutoka tani 600 mnamo 2008 hadi tani 1,842 mnamo 2018.

Hii inatoa ufafanuzi wa kushuka kukubwa katika hazina yake ya dhahabu, iliyo fikia kilele mnamo 2014 na kuzidi dola trilioni 4 (tovuti ya Trading Economics). Tambua kuwa China imenunua zaidi ya tani 700 za dhahabu mnamo 2015 pekee. Ama kuhusu hazina za Amerika, baada ya mgogoro wa kifedha wa 2008, China ilianza kuziuza. Thamani ya rasilimali zake ilishuka wakati wa miaka miwili baada ya mgogoro huo, lakini tishio la Kiamerika la kuzuia biashara ya China, lililoibuka wakati huo katika kadhia ya usalama wa vikaragosi vilivyo safirishwa kutoka China hadi Amerika, iliifanya kurudi na kupata dola zaidi. Hili liliendelea hadi kufikia kileleni mnamo 2013, lakini China ilirudia kuuza nyuma ya pazia ya vitisho vya kibiashara kutoka kwa utawala wa Trump.

Ilipunguza rasilimali za bondi hizi kwa njia isiyo ya majibizano … na kisha kutafuta njia ya kupunguza dori
ya dola katika biashara yake. Ilitia saini makubaliano na Urusi, Japan na nchi nyenginezo kwa ajili ya biashara kwa pesa za kinyumbani. Vile vile iliasisi Soko la Hisa la Shanghai kwa ajili ya biashara ya mafuta iliyo tawaliwa kwa yuan iliyo egemezwa kwa dhahabu, iliyoifanya kushikilia asilimia 10 ya biashara ya mafuta duniani wakati wa miezi sita ya kwanza ya kuasisiwa kwake, ilijiunga na haki maalumu za uchukuaji, (SDR) (yuan inajiunga na dola ya Kiamerika, euro, yen ya Kijapani na pauni ya Uingereza katika kapu la sarafu la SDR, yuan inaongezea kapu la sarafu lililo na haki maalumu za uchukuaji (SDR) moja kwa moja kuanzia 1/10/2016. (https://www.imf.org 30/9/2016)

Lakini, kwa yote haya, uzito wa rasilimali za dola za China, bondi nk. yanaifanya kazi yake ya kuiondoa dola
kutokuwa thabiti; hii ndio sababu Yuan inashikilia asilimia 1.7 pekee ya malipo ya kimataifa, ikilinganishwa na asilimia 40 ya dola ya Kiamerika.

C- Muungano wa Ulaya:
Mnamo 1999, euro iliibuka; ilitumika katika mabenki na kubadilisha sarafu za kinyumbani za baadhi ya nchi
kama sarafu badala katika Muungano wa Ulaya kuanzia 2002. Ilijaribu kushindana na dola, kwa kuwa nyuma
yake zinasimama nchi imara za kiuchumi kama vile Ujerumani na Ufaransa, zikiungwa na nyenginezo zilizo
endelea kiviwanda na nchi tajiri. Hivyo basi euro ikawa ni sarafu yenye nguvu kiulimwengu. Na nyuma yake
unasimama mkusanyiko wa nguvu zinazo weza kuwa
na athari ya kisiasa ya kiulimwengu inayo shindana
na Amerika, na ina uwezo wa kuunda jeshi huru lenye
nguvu kama inavyo tafuta. Euro hii imekuwa ndio hazina
katika benki kuu za kimataifa kwa asilimia 20-23. Lakini
mojawapo ya mambo makuu yanayo zuia euro kutokana
na kuutawala uchumi wa kiulimwengu ni udhaifu wa
ushawishi wa kisiasa, kijeshi na kiuchumi wa Ulaya
kukabiliana na Amerika. Muungano wa Ulaya wenyewe
ungali unahami uwepo wake, kwani kuna matishio
yanayotishia kwa urahisi uwepo wake, na kujiondoa
kwa Uingereza kutokana nao ilikuwa ni mshtuko wa
kiujasiri dhidi yake pamoja na kuibuka kwa harakati za
kujitenga za ubaguzi wa rangi katika nchi zake, pamoja
na matakwa ya kujitenga kutokana na muungano
huo, yanayo dhoofisha imani ya Muungano huo …
kuongezea ni ukosefu wa umoja katika maamuzi ya
kisiasa, yote ni mambo yanayo mulika sarafu ya euro na
imani kwake.

2- Dola zinazo zunguka katika duara la Amerika kwa makubaliano ya Urusi, China na Ulaya:
• Uturuki, Iran, India, na Japan:
– Kinara wa Benki Kuu ya Iran Abdul Nasser Hamati alitangaza katika mkutano na wawakilishi wa Urusi na
Uturuki kuwa “kadhia ya biashara ilijadiliwa kutumia sarafu ya kinyumbani badala ya dola” (Tehran Times,
9/9/2018)
– Uturuki, Urusi na Iran zimekubaliana kutumia sarafu zao za kinyumbani katika biashara baina yao badala ya dola ya Amerika, shirika la habari la Anatolia liliripoti. Shirika hilo, linalo endeshwa na dola hiyo lilimnukuu gavana wa Benki Kuu ya Iran, Abdul Nasser Hamati akisema jijini Tehran, “miamala ya kibiashara itakuwa ikitumia kiwango maalumu cha ubadilishanaji”. (https://ahvalnews.com/ar 9/9/2018)
– Mnamo Oktoba 2018, China na Japan zilikubaliana kubadilisha dola bilioni 30 ya sarafu, mkataba mkubwa
zaidi kufanyika nchini Japan. “Mkataba wa kusambaza makombora aina ya S-400 kwenda India utafanywa kwa kutumia sarafu ya Urusi ya ruble,” Naibu Waziri Mkuu wa Urusi Yury Borisov alisema mnamo 31/10/2018.

Nchi hizi, ambazo China na Urusi zinajaribu kuleta sera ya kukabiliana na sarafu za kinyumbani, zingali
zinazunguka katika duara la Amerika au ni vibaraka wake, yaani, kisiasa zimeunganishwa na Amerika na kwa
haraka zimejipanga na Amerika, na hazifanyi maamuzi ya kuachana na kupambana na dola au kuachana na
kuifanya kuwa sarafu ya hazina zao za pesa taslim.
Uamuzi wa uhuru wa kiuchumi ni lazima ulinganishwe na uhuru wa kisiasa, mithili uhuru wa China na Urusi.
Na ikiwa zitakubali kutafiti kupambana na sarafu ya kinyumbani pamoja na Urusi na China, hii ni kwa sababu wamesukumwa na Amerika kutokana na hali ya dharura, lakini pindi itakapomalizika mambo yatarudi kama kawaida:
Tangu vikwazo viwekwe juu ya chuma cha Uturuki, na tangu Amerika iishambulie sarafu ya Uturuki,
Erdogan alianza kuikashifu dola kwa ajili ya rai jumla ya nyumbani. Deni jumla la Uturuki la zaidi ya dola bilioni 400 hukusanywa kwa dola, ikimaanisha kuwa kila wakati sarafu yake inashuka thamani dhidi ya dola malipo ya deni yanahitaji lira zaidi na zaidi, na kisha bei kupanda na kuwapa mzigo watu, na Erdogan akitoa hotuba zake za kuzuzua kama kawaida! Taarifa za Erdogan kwa kongamano la sita la Baraza la Uturuki katika Kituo cha Kitamaduni cha Roh Ordu nchini Kyrgyzstan, mnamo tarehe 3 Septemba, ndani yake alisema: “Tunapendekeza kufanya biashara kwa sarafu yetu wenyewe badala ya dola ya Kiamerika.”

Taarifa hii haina uhalisia, na iko mbali na kuwa kweli, kwa sababu Uturuki kimsingi inafanya biashara na EU! Lakini, Uturuki inafanya biashara kwa dola, inakopa kwa dola na nyingi ya hazina zake za sarafu ya kigeni ziko kwa dola, na mafuta, gesi na mali ghafi zinazo agizwa zote ni kwa dola… Tuliiona Uturuki pindi Amerika ilipoondoa vikwazo baada ya mchungaji wa Kiamerika kuachiliwa huru, mambo yalirudi kama kawaida, na ikapoteza ari ya kuupa kipaumbele muamala wa sarafu za nyumbani kabla ya kuondolewa vikwazo … Ama kuhusu nchi zinazo zungumza Kituruki eneo la Asia ya Kati, zinafuata sera ya Urusi, na biashara ya Uturuki kwazo hata kama zinabadilishwa kwa sarafu za kinyumbani hazifikii kiwango cha tarakimu za ushawishi katika biashara ya kiulimwengu kutokana na kutengwa kwa uchumi wa nchi za Asia ya Kati.

Iran imepigwa marufuku kuamiliana na dola kwa sababu ya vikwazo vikali vya kifedha vilivyo ekewa juu yake kwa miaka mingi baada ya kuondolea katika mfumo wa benki wa Kiamerika … Lakini baada ya kuondolewa vikwazo hivyo mnamo 2015, ilikuwa ikiuza mafuta yake kwa dola na kutia saini mikataba mikubwa na kampuni za kimataifa, ikiwemo kampuni za Ulaya kama vile Airbus na Total na kampuni ya Kifaransa kwa dola pekee, kana kwamba hakuna kitu chochote kilichotokea! Vikwazo hivyo na kuondolewa kwake vimeathiri matendo ya Iran kwa muda muwafaka. Amerika ndio inayo iingiza au kuitoa Iran kutoka katika nidhamu ya kibiashara (SWIFT) kwa dola. Amerika inapoongeza taarifa zake dhidi ya Iran na kufunga milango yake ya dola, majibu ya Iran ni taarifa kwamba haitaamiliana na dola.

Ama kuhusu India, tangu jadi inaagiza silaha za Urusi na Amerika haijali hilo. India ina nafasi maalumu kwa
Amerika kwa sababu inaitaka iwe nguvu muhimu ya kupambana na ongezeko la ushawishi wa China barani
Asia. India inajua hilo, kwa hivyo India haitarajiwi kutafuta mabadiliko ya dola kwa ruble au yuan kama sarafu ya kiulimwengu. Japan, inayo nasibishwa na Amerika, haihitaji kuelezwa kwa kina. Kuamiliana kwake na Urusi haimaanishi kuwa wako dhidi ya dola au kwamba wanaikubali ruble kama badali ya dola.

Kwa kutamatisha, nchi ambazo zaweza kusemwa kuwa na athari thabiti juu ya kuondolewa kwa dola kutoka
katika cheo chake ni Urusi, China na Muungano wa Ulaya. Lakini kila moja ya nchi hizi zina mambo yanayo
dhoofisha harakati yao kama tulivyo fafanua, lakini endapo watayaondoa mambo hayo, zinaweza kuiondoa
dola kutoka katika cheo chake. Ikiwa hazitafanya kazi juu ya jambo hili, watashtushwa na ile inayoitwa “dola
hafifu” na utajiri wao wa hazina ya dola utapotea.
Amerika inateseka kutokana na deni kubwa. Kwa mujibu wa Washington Examiner, jarida la Kiamerika, mnamo 1/10/2018, “deni la serikali ya Amerika limekuwa kwa zaidi ya dola trilioni 1.2 wakati wa mwaka wa matumizi ya serikali uliomalizika mnamo 30 Septemba 2018 kwa mujibu wa mtandao wa serikali unaofuatilia deni hilo.

Deni la kitaifa la Amerika mwishoni mwa mwaka wa matumizi ya serikali wa 2017 limefikia 20.25 trilioni …”
Mrundiko wa deni la Kiamerika kwa miongo kadhaa limeitia nchi hiyo katika tatizo la kifedha. Kwani
mrundiko huu uliongezeka baada ya mgogoro wa 2008, ukiongezeka kutoka dola trilioni 8 hadi dola trilioni 21 leo, tatizo la kifedha la Kiamerika limekuwa baya zaidi, ambapo Bolton ameliita tishio kwa usalama wa kitaifa, na linahitaji suluhisho ya haraka, yaani, karibuni na hivi punde, na wala si mbeleni … Kutokana na uhalisia huu, suluhisho lililobakia kwa Amerika ili kumudu fedha zake ni kuzalisha pesa zaidi (kuchapisha dola). Kuongeza pesa katika idadi inayo kimu ufadhili wa dola, mbali na kulipa madeni yake, ambayo itapelekea kuporomoka kwa dola hiyo, au kile ambacho Waziri wa Hazina wa Amerika alikiita “dola hafifu”, akimaanisha kupotea kwa sehemu ya utajiri wa nchi za kiulimwengu zinazo amiliana na dola katika biashara zao, hazina za fedha zao, na bondi za hazina ya Amerika, hasara kama vile kudhoofika kwa dola, ambapo itakuwa ni pigo kwa nchi hizo!

Lakini, uhalisia wa sasa ni kuwa nchi hizi haziwezi kutabanni sarafu ya kiulimwengu badala ya dola
lakini, inawezekana kusema kuwa majaribio ya Urusi na China ya kuamiliana na sarafu za kinyumbani na
kufanya mikataba na nchi nyenginezo kwa sarafu za kinyumbani, yana athari ya kuvunja utawala wa
dola ikiwa yataendelea kuwa imara pasi na ulegevu, harakati ya Ulaya sambamba na China ina athari
kubwa. Matakwa ya kununua dhahabu yatatilia nguvu hilo, hayatatui tatizo maadamu itabakia kuwa bidhaa
katika benki kuu inayo uzwa kwa dola inapo hitajiwa na dola, au hazina ili kuisaidia sarafu ya karatasi ya dola ili kuiwezesha kufikia sarafu madhubuti. Lakini haitatatua tatizo hilo, mpaka dhahabu na fedha ziwe sarafu na noti za benki zichapishwe na ziwe kwa thamani ya dhahabu au fedha, na sio tu zitumiwe kama bidhaa katika benki za kununulia ile inayo itwa sarafu madhubuti. Hii yamaanisha kuwa Benki Kuu ya kila nchi itatoa sarafu kwa dhahabu na fedha, inakubalika kuchapisha noti za benki kwa thamani ya dhahabu na fedha, na mmiliki wake atakuwa na haki wakati wowote kwenda benki na kuchukua thamani ya dhahabu au fedha badala yake, yaani kuitumia kama sarafu badala ya dhahabu na fedha lakini kwa thamani ya dhahabu na fedha iliyo andikwa katika noti ya benki … kwa hivyo dhahabu na fedha zitatawala. Na kisha hakuna nchi yoyote itakayo weza kufuja utajiri wa wengine au kudhulumu juhudi zao na kupeleka mashini ya vita na kuanzisha vita vyake viovu kwa noti zisizo na thamani kama tuonavyo sasa. Hakuna dola yoyote itakayo weza kufanya hivi, bali dola ya Khilafah, ambayo yaweza kutekeleza hilo kwa sababu ni hukumu ya kisheria iliyo amrishwa na Mwenyezi Mungu, na ilitekelezwa na Mtume wake (saw) katika dola yake, na kufuatiwa na makhalifa waongofu na makhalifa waliowafuata hadi kuvunjwa kwa Khilafah 1342 H sawia na 1924 M, kisha batili ikatawala … Mfumo wa kirasilimali umetawala ulimwengu, wamiliki wake wanachojua ni uporaji na kula pesa za watu kwa batili na ukusanyaji wa pesa kwa mabilioni. Ni dhuluma ya sheria ya binadamu,
na tunaona natija haribifu ya migogoro ya kifedha na fadhaiko la kiuchumi ikiongezewa na kuutumia vibaya
uwezo wa watu na kupora utajiri wao na kupotea kwa pesa zao kama makaratasi yasiyo na thamani yoyote! Ni muhimu kuangamiza mfumo huu batili na kufanya kazi kwa ajili ya ubwana wa mfumo wa Kiislamu mfumo wa haki na uadilifu uliojifunga ndani ya dola yake ambayo Mwenyezi Mungu amewaahidi waumini wake wenye ikhlasi, wafanyikazi wema:

(وَعْدَ اللَِّ لَ يُخْلِفُ اللَُّ وَعْدَهُ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَ يَعْلَمُونَ)
“[Ni] ahadi ya Allah. Mwenyezi Mungu, hakhalifu ahadi yake, lakini wengi wa watu hawajui” [Ar-Rum: 6]

Ulimwengu utabakia katika matatizo ya kifedha na kiuchumi maadamu hauhukumu kwa sheria ya Mwenyezi
Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mkweli

(وَمَنْ أَعْرَضَ عَنْ ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنْكاً)
“Na yeyote anayeupa nyongo utajo wangu – kwa hakika atakuwa na maisha ya dhiki, na Tutamfufua kipofu Siku ya Kiyama.” [Ta-Ha: 124]

18 Rabii’ Al-Awwal 1440 H
26/11/2018 M

Inatoka Jarida la Uqab: 24        https://hizb.or.tz/2019/01/01/uqab-24/

Maoni hayajaruhusiwa.