Kumbukumbu ya kifo Cha Sheikh AbdulHamiid Kishki
بـسم الله الرحمن الرحيم
Habari:
Mnamo tarehe 6 Disemba ilikuwa ni kumbukumbu ya 22 ya kifo cha bingwa wa mimbari Sheikh Abdulhamiid Kishki (Allah Amrehemu )
Maelezo :
Katika usiku wenye kiza huwa ni muhali kuonekana mbaramwezi. Na hivyo ndivyo zilivyo zama hizi ambazo wanazuoni wengi wamekuwa ni wanyeyekevu kwa watawala madhalimu, na wamekuwa wachache wanazuoni wachamungu wenye kuulea Ummah malezi ya kisawa sawa, ni wajibu juu yetu tuwakumbuke mabingwa wa mimbari kama Sheikh Abdulhamid Kishki, Sayyid Qutbi ,Ibnu Ashuur na wengineo.
Ameishi Sheikh Abdulhamiid Kishki wakati wa tawala za maraisi Jamal Abdul Nasri, An’war Saadat na Hussni Mubaraka,na wote hao aliwakosoa kwa ulimi wake,,,wakamfunga na wakamuadhibu kwa adhabu kali sana kwa kiwango cha kubakia alama za adhabu hizo katika mwili wake,lakini uhai wa Sheikh bado ukawepo. Akafa Rais Abudul Nasir, akamuacha Sheikh bado duniani, akafa Raisi Saadaat, akamuacha pia Sheikh Kishk bado duniani, na hatimae mnamo mwaka 1996 Sheikh Kishki alirudi kwa Mola wake akiwa katika Sijda.
Hakika ya mwanazuoni haipimwi kwa wingi wa elimu yake, isipokuwa
hupimwa kwa misimamo yake.
Kuna Maulamaa wa Kiislamu katika tareekh ya Waislamu wa wakati huu na wakati uliopita ambao zimebakia kumbukumbu zao na utajo wao , hawakuwa mashuhuri na kujulikana mpaka leo hii kwa elimu yao tu kubwa na upana wa ujuzi wao wa kifiqhi peke yake, bali kwa misimamo yao ya kiunaume ( kirijali ) kwa kule kuitumia elimu yao ya kisheria kwa kadhia kubwa zilizotokea wakati wao.
Iko mifano mingi ya maulamaa hawa wasiokuwa na idadi, kama vile Imam Ahmad bin Hambali alyeijitokeza kuzungumzuia mas’ala ya kuumbwa kwa Qur’an, na Abdullah Bin Abbas alijitokeza kupambana na Khawaariji,na Said Bin Jubeir alipambana na Hajjaaj Bin Yusuf, Izzu bin Abdis Salaam akipambana na utawala wa Mamaaliki na Ibn Taymia alipambana na Tataar… na kama hivi. Misimamo yao ya kiume ndio iliyobakisha utajo wao na kukumbukwa kwao mpaka leo hii.
Wako wapi leo maulamaa wa Kiislamu? Wako wapi wasimamie kadhia za Ummah zinazoendelea kutokea? Wako wapi wao katika kushikamana na maneno ya Allah
لَتُبَيِّنُنَّهُ لِلنَّاسِ وَلَا تَكْتُمُونَهُ﴾؟!
(Wallah) … “Mtabainisha kwa watu na wala hamtoficha (haki )” TMQ 3:187﴿
Wako wapi wao wanavyuoni na na kauli ya Imam Ghazaali aliposema
: “Kuharibika Raia ni kwa sababu ya kuharibika watawala, na kuharibika kwa watawala ni kwa sababu ya kuharibika maulamaa”?!
Enyi Wanavyuoni wetu! Enyi chumvi ya biladi zetu ! Ni nani atakayeibadilisha chumvi pindi ikiharibika !
اللهم ارحم الشيخ عبد الحميد كشك وجميع العلماء الربانيين واحشرنا معهم
مصداقا لقول رسولنا ﷺ «الْمَرْءُ مَعَ مَنْ أَحَبَّ»
Ewe Allah Mrehemu Sheikh Abdulhamiid Kishi na Maulamaa wote waliokuwa marijali,na tufufue pamoja nao,ikiwa ni kusadiksha kauli ya Mtume (S.a.w) :
“Mtu atakuwa pamoja na wale anaowapenda”
Imeandikwa na Jaabir Abu Jaabir
Kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari
Hizb ut Tahrir
Maoni hayajaruhusiwa.