Rabiul-Awwal: Mwezi wa Upambanuo Baina ya Batili na Haki

Ummah wa Kiislamu ulimwenguni kote upo katika harakati za kusherehekea kuzaliwa kwa Bwana na Kipenzi chetu Muhammada ibn Abdullah (saw). Ni mwezi uliojaa nishati na furaha kwa Ummah wa Kiislamu duniani. Kila mwanachama wa Ummha huu mtukufu daima hapitwi na tukio hili adhimu ambalo ni msingi madhubuti wa mwamko wa Ummah huu. Kwani (saw) alikuwa ni Mtume wa mwisho kuwahi kutumwa ulimwenguni.

رَّسُولَ ٱللَّهِ وَخَاتَمَ ٱلنَّبِيِّـۧنَۗ

“(Muhammad) ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mwisho wa Manabii.” [Al-Ahzaab: 40]

Na ujumbe wake ni kwa walimwengu wote kinyume na mitume waliotangulia:

وَمَآ أَرۡسَلۡنَـٰكَ إِلَّا رَحۡمَةً۬ لِّلۡعَـٰلَمِينَ

“Nasi hatukukutuma (Muhammad) ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.” [Al-Anbiyaa: 107]

Na hakika kuja kwake ni Nuru iliyoangaza juu ya ulimwengu na kitabu alichopewa kinabainisha baina ya Haki na Batili:

قَدۡ جَآءَڪُم مِّنَ ٱللَّهِ نُورٌ۬ وَڪِتَـٰبٌ۬ مُّبِينٌ۬

“Bila shaka imekujieni kutoka kwa Mwenyezi Mungu nuru (Muhammad) na Kitabu (Qur’an) kinacho bainisha (Haki na Batili).” [Al-Maaida: 15]

Kwa masikitiko makubwa Mwezi huu umetujia lakini Waislamu tumo katika hali duni na tuliojawa na hizaya kutoka kila pembe. Hali hii imetokana na Ummah huu mtukufu wa Kiislamu kujiweka mbali na mafundisho ya Nuru (Muhammad) na Kitabu (Qur’an). Badala yake umejisalimisha kutawaliwa na mfumo batili wa kisekula wa kirasilimali unaotokana na dola za kimagharibi za kikoloni. Dola hizi za kimagharibi ndizo zilizosambaza sumu kupitia itikadi yake ya kiilmaniyah (kutenganisha dini na maisha). Itikadi hii ndiyo chanzo kilichowapelekea baadhi ya wanachama wa Ummah huu mtukufu wa Kiislamu kusalitika nayo na kuwapelekea kufanyakazi na kushirikiana na viongozi wa kimagharibi katika Kumdunga Kisu Mama wa Faradhi zote Katika Uislamu – Khilafah. Kisha wakaivunja na kuigawa vipande vipande na kukabidhiwa kama ngawira kwa wajinga wakubwa wakiongozwa na Mustafa Kamal aliyepewa Uturuki iliyokuwa ndiyo makao makuu ya Khilafah kabla kuiangusha. Akifuatiwa na Sharrif Hussein na wanawe wakipewa Saudi Arabia, Iraq na Jordan n.k.

Kuangushwa kwa Dola ya Kiislamu ya Khilafah ndiyo chanzo cha hizaya juu ya Ummah huu mtukufu ambao kitakwimu unakaribia bilioni 2! Licha ya kuwa Ardhi za Waislamu ndiyo chanzo cha rasilimali muhimu zenye kuendesha uchumi wa dunia kwa mfano mafuta, gesi na madini n.k bado wafuasi wake wanazama ndani ya umasikini wa kupindukia kuanzia Yemen, Somalia, Iraq n.k. Majeshi yake lau yataunganishwa chini ya Dola moja basi litakuwa jeshi kubwa duniani na lenye zana nyingi! Tukichukua rasilimali, majeshi na Waislamu wote duniani chini ya Dola Moja ya Khilafah iliyosimamishwa kwa njia ya Utume inayoongozwa na Khalifah mchaMungu anayetawala kwa Qur’an na Sunnah; kattu hakuna atakayejaribu kuwacheza shere Waislamu na kuzimwaga damu zao kama inavyoshuhidwa hjvi leo nchini Palestina, Somalia, China, Afghanistan, Kashmir, Syria n.k. Hakika kama alivyofanya Mtume (saw) juu ya Kabila la Kiyahudi la Banu Qaynuqa lililomchezea shere mwanamke mmoja Muislamu likafurushwa kabila lote! Nalo Kabila la Kiyahudi la Banu Qurayza lililowaendea kinyume Waislamu, wanaume wao wote waliobaleghe wakauliwa! Na mifano mingi chini ya Makhalifa wachaMungu kuanzia Abu Bakar (ra) mpaka Khalifa wa mwisho Abdulhamid wa Pili; hakuna aliyejaribu kuwaotesha kidole Waislamu au Uislamu wao.

Lakini hivi leo Uislamu hautawali hakuna ngao ya Waislamu ili kuwaunganisha Waislamu chini ya twaa ya kiongozi mmoja. Kinyume chake kila mmoja amebakia kujifunga na utaifa wake kwa mujibu wa mipaka iliyochorwa na wakoloni wamagharibi na kuzama ndani ya hisia za kizalendo kiasi kwamba Muislamu aliyeko Tanzania/Pakistan/Libya/Syria anamuona wa Kenya/CAR/Afghanistan/Palestina ni mgeni na kamwe hana ukuruba naye; na matatizo yake ni yake wala hayamuhusu! Ilhali Ummah huu ni Ummah Mmoja sawa na Mwili Mmoja:

“Waumini katika kuhurumiana kwao ni kama mwili mmoja. Wakati kiungo kimoja kinaumwa, mwili mzima unashughulishwa kwa kuupelekea kuwa na homa na kukosa usingizi.” [Bukhari na Muslim]

Kwa hivyo hatuna budi kuitikia Mwito wa Kurudisha Maisha ya Kiislamu kupitia kurudisha tena serikali ya Kiislamu ya Khilafah kwa njia ya Utume. Hakika kupitia kufanya kazi hii ndiko kunakopelekea mwanadamu kupata ladha ya maisha na utulivu wa nafsi. Kwani ni kupitia kurudi kwa Khilafah ndiko kutakako hakikisha  kunaondosha udhalimu na maonevu wanayopitia Waislamu na wasiokuwa Waislamu ulimwenguni chini ya mikono na sera fisadi za wamagharibi wakoloni kutokana na mfumo wao wa kisekula wa kirasilimali na nidhamu zake angamivu ikiwemo demokrasia n.k.

يَـٰٓأَيُّہَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱسۡتَجِيبُواْ لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمۡ لِمَا يُحۡيِيڪُمۡ‌ۖ

“Enyio mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfaal: 24]

Ni jukumu letu Waislamu wote hususan viongozi katika Ummah wapatilize msimu huu na kuwatangazia Waislamu Uyatima waliokuwa nao na Ufaradhi wa Kurudisha Khilafah ili kuuondosha uyatima huo! Ama kwa walio na nguvu miongoni mwa majeshi katika watoto Mukhlisina Waislamu ndani ya nchi za Waislamu mfano Pakistan, Misr, Iraq, Jordan n.k waitiekie mwito huu kwa kutoa Nusrah na wajue kuwa malipo yao ni Pepo kama vile walivyoahidiwa Khaws na Khazraj (Ansar) wachangamke na kwa hakika wataingia katika historia kama alivyoingia katika historia Sa’d ibn Mu’adh (ra) kutokana na dori kubwa aliyocheza katika kuunusuru Uislamu na Waislamu na ikapelekea:

“Kiti cha enzi ya Mwenyezi Mungu kimetikisika kutokana na kifo cha Sa’d ibn Mu’adh.”

[Bukhari na Muslim]

Hitimisho; kila anayesheherekea kuzaliwa kwa Mtume (saw); ajiulize “Je Qur’an na Sunnah ndiyo Muongozo/Mfumo wetu Katika Maisha Jumla (Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi, Kielimu n.k)? Na awe mkweli katika jibu lake na ajue kuwa atakwenda kuulizwa Siku ya Kiyama mbele ya Mwenyezi Mungu “Je ulicheza dori gani wakati Qur’an na Sunnah zilikuwa SIO Muongozo Katika Maisha Jumla?” Wakati ni sasa kujiunga na kufanyakazi katika safu iliyobeba kheri kubwa kuliko kheri zote nayo ni safu ya Ulinganizi wa Kurudi tena Khilafah kwa Njia ya Utume. Safu isiyopaka mtu mafuta wala kupinda aya kwa ajili ya maslahi au kuogopa vitisho vya wanaotishia! Bali daima kila siku safu hii inaelekea kufikia bandarini kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu kwani Yeye ndiye huumpa Ushindi Amtakaye.

Ali Nassoro Ali

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya

http://hizb.or.ke/sw/2018/11/16/rabiul-awwal-mwezi-wa-upambanuo-baina-ya-batili-na-haki/

Maoni hayajaruhusiwa.