Risala Kutoka kwa Mwanachuoni Mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah Katika Siku Kuu ya Idd ul-Adha Yenye Baraka ya Mwaka 1439 H Ikiafikiana na Mwaka 2018 M
بسم الله الرحمن الرحيم
Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha Ila Allah, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Wa lilah Alhamd
Kwa Umma wa Kiislamu ambao Allah ameukirimu na kuusifu kama:
[كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ]
“Nyinyi ni Umma bora uliotolewa kwa watu munaamrishana mema na kukatazana maovu na munamuamini Mwenyezi Mungu”
[Al-i-‘Imraan: 110].
Kwa wabebaji ulinganizi, Mashabaab na Mashabaat wa Hizb ut Tahrir, wabebaji ulinganizi wasafi na wachaMungu, ingawa hatumtakasi yeyote mbele ya Allah, wale wanaozungumza maneno ya kheri na kutenda vitendo vyema, na kisha kama natija yake Allah akawasifu wale wenye sifa hizi:
[وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِمَّنْ دَعَا إِلَى اللَّهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِين]
“Na ni nani aliyembora katika maneno kuliko yule alinganiaye kwa Allah na kutenda mema na akasema: “Hakika mimi ni miongoni mwa Waislamu”
[Fussilat: 33].
Kwa wale watukufu wanaozuru ukurasa wa Facebook ambao huuzuru kwa ajili ya haki na ukweli, wakitafuta kheri inayobebwa nao, kwa hivyo Allah awalipe kheri…
Kwa wote hao,
Assalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh
Nawapongeza katika siku kuu hii ya Idd ul-Adhaa na Allah awakubalie amali zao njema. Namuomba Allah Subhaanahu kuikubali Hajj ya wale wenye kuitekeleza na kuifanya kuwa Hajj yenye kukubaliwa, na juhudi yenye kupokewa vyema na dhambi zenye kusamehewa. Na pia namuomba Allah Subhaanahu kuwapa Tawfiq wale ambao hawakufanya Hajj mwaka huu ili wafanye mwakani pamoja na kheri juu ya kheri, na Allah Sunbhaanau ndio mlinzi wa walio wema.
Kaka na dada zangu wapendwa: Idd inakuja mwaka huu huku kukiwa hakuna Khilafah. Hivyo basi makafiri wakoloni na vibaraka wao wanatucheza karata dhidi yetu na kuchochea mauwaji na umwagikaji wa damu katika nchi zetu. Uhalifu wao wa kinyama umeenea kuanzia katika mabomu mpaka katika makombora yenye maangamivu hadi katika silaha za kemikali … yote haya kupitia mikononi mwao na wakati mwengine kupitia mikononi mwa vibaraka wao. Kila uangaliako utaona damu ya Waislamu ikimwagwa kwa dhulma kutokana na uvamizi … Upande wa Mashariki ni Burma, na mnajua nini kuhusu Burma, hali ya Waislamu huko ni ya kuumiza moyo, kutokana na uhalifu wa Mabudha na unyama wao ambao hata mazimwi wa mwituni hawawezi kuyafanya hayo … Na mnaona Kashmir na uhalifu wa India huko … Upande wa Kaskazini mnaona Chechnya na Caucasus na kisha Crimea ambayo inaangamizwa kupitia mikono ya Urusi, ambayo imeizamisha katika uhalifu na damu … mkitembea upande wa mashariki hadi Turkestan Mashariki, mtaiona China na aina zake tofauti tofauti za ukandamizaji … mkitembea kusini na kufika katika ufuo wa bahari yake, mtakipata kitovu cha ardhi za Kiislamu, Ardhi Tukufu, Palestina, Qibla cha kwanza kati ya Vibla viwili mtawaona Mayahudi wakiinyakua na kufanya uhalifu na mauwaji, na kusikia maumivu ya Msikiti huo ukilalama kutokana na donda kubwa linaloufanya kusikika kana kwamba unapumua pumzi zake za mwisho.
Kisha Ash-Sham na mnajua nini kuhusu Ash-Sham, damu ina mwagwa katika kila upande, mauwaji ya kinyama yameenea takribani katika kila barabara na mitaa kutokana na dhalimu wa Ash-Sham, na nyuma na mbele yake ikiwa ni Amerika na wafuasi na waungaji mkono kutoka Urusi hadi Iran na kisha wanamgambo … Wote hawa ndio wanaochochea moto, mauwaji na umwagaji damu kwa kila mbinu ovu za mauwaji … Na hapa mauwaji ya Idlib yanazidi kasi kupitia umiminaji mabomu kinyama katika pande zote, na halaiki ya madhalimu kudhamini hilo, kwa mchanganyiko wa khiyana inayoizunguka … Kisha Iraq, dada ya Ash-Sham katika majanga na maafa … Mkienda upande wa kusini hadi Yemen, ambayo mwanzoni ilikuwa na furaha, mtaiona imekuwa na huzuni kutokana na majanga ya mapigano yaliyoanzishwa na nchi za kikafiri za kikoloni, ziliyoifanya kama uwanja wa mashindano baina yao juu ya mafuvu na damu zetu … mukielekea upande wa machweo, mtaiona Libya na mapigano kati ya Waislamu wenyewe kwa wenyewe. Kisha mukielekea Afrika ya Kati, mtaona kuwa Waislamu wamepata mateso na uharibifu na kumwagwa damu zao isiyokuwa na hatia; kuvurugwa kwa matukufu huko hakuelezeki … Kisha jirani yake Sudan, eneo lake la kusini limetenganishwa na kaskazini, ikiiwacha kidonda chake kikivuja damu. Kisha Somalia inayolia kutokana na uchungu mwingi na mapigano makali kwa miaka.
Majanga yote haya yako katika ardhi za Waislamu, ambazo miaka ya nyuma zilikirimiwa kwa Uislamu, bendera ya Uislamu, Adhana ya Uislamu, na uadilifu wa Uislamu … Lakini baada ya kuvunjwa Khilafah na kuondoka kwa Imam, ngao (al-Junnah), hali ilibadilika, Umma ukateseka na wakoloni makafiri na vibaraka wao watawala madhalimu wakashuka na kushirikiana nao dhidi yake. Pasi na kutaja majanga ya Waislamu katika nchi za makafiri, ni mengi mno, mataifa hayo yanataka kuwatoa Waislamu kutoka katika ngozi yao (kitambulisho), kwa hivyo wanalishambulia vazi la Wanawake wa Kiislamu, na wanataka kunyamazisha sauti yao ya Adhana, na wanaeneza chuki dhidi yao katika mujtamaa zao, asasi zao za kijamii na hata juu ya barabara zao … Ni janga tangu kukosekana Khilafah, moja baada jengine, majanga yaliyo kusanyika yanayo muacha aliye mgonjwa kuchanganyikiwa.
Kaka na dada zangu wapendwa: majanga haya lau yangelisibu taifa lolote lingeporomoka, au lingekata tamaa na maisha, lau kungali kuwepo na maisha yaliyosalia … Ama kwa Umma wa Kiislamu, uko na Kitabu cha Mola wake na Sunnah za Mtume wake na hata miujiza ya viumbe ya usiku na mchana, ambayo yanaufanya kuwa mkakamavu wakati wa matatizo na subra yake haidhoofiki kwa migogoro, lakini huongeza nguvu juu ya nguvu na huongeza subra juu ya kujizatiti kwake na kufanya kazi yake kwa imara na njia bora na kumtegemea Mola wake kwa ikhlasi:
* Kutoka katika Kitabu cha Mola wake: aya ziko wazi katika hili:
[فإِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا * إِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا]
“Kwa hakika, pamoja na uzito ni wepesi* Hakika, pamoja na uzito ni wepesi”
[Ash-Sharh: 5-6],
[حَتَّى إِذَا اسْتَيْأَسَ الرُّسُلُ وَظَنُّوا أَنَّهُمْ قَدْ كُذِبُوا جَاءَهُمْ نَصْرُنَا فَنُجِّيَ مَنْ نَشَاءُ وَلَا يُرَدُّ بَأْسُنَا عَنِ الْقَوْمِ الْمُجْرِمِينَ]
“Mpaka walipokata tamaa Mitume na kudhani kuwa wamekadhibishwa iliwajia wao nusra yetu, na tukamuokoa kila tuliyemtaka. Na wala hakuna wa kuirudisha adhabu yetu kwa watu waovu”
[Yusuf: 110],
[أَمْ حَسِبْتُمْ أَنْ تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَأْتِكُمْ مَثَلُ الَّذِينَ خَلَوْا مِنْ قَبْلِكُمْ مَسَّتْهُمُ الْبَأْسَاءُ وَالضَّرَّاءُ وَزُلْزِلُوا حَتَّى يَقُولَ الرَّسُولُ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ مَتَى نَصْرُ اللَّهِ أَلَا إِنَّ نَصْرَ اللَّهِ قَرِيبٌ]
“Je, mwadhani kuwa mutaingia Peponi kabla haujawafikeni mfano wa wale waliokuwa kabla yenu? Walipatikana na shida (ufukara) na madhara (mwili) na wakatingishwa mpaka Mtume na waumini pamoja naye wakasema, ‘ni lini nusra ya Allah?’ Pasi shaka, nusra ya Allah iko karibu.”
[Al-Baqara: 214]
* Katika Seerah ya Mtume wake: yale yaliyomtokea Mtume wa Allah (saw) wakati wa mwaka wa huzuni, pindi Khadija (ra), mama wa Waumini alipofariki, na kisha kifo cha Abu Talib, aliyemsaidia Mtume wa Allah (saw). Kisha majibu mabaya kutoka kwa watu wa Taif, yaliyomuacha Mtume wa Allah (saw) akivuja damu. Na kisha mgogoro huu kuongezeka na kuafikiana kumuua Mtume wa Allah (saw). Kisha wao (Maquraysh) kumwandama hadi kwenye pango la Thaur, alipokuwa amejificha pamoja na rafikiye Abu Bakr, Allah awe radhi naye. Wao (Maquraysh) walisimama mbele ya mlango wa pango huku masafa kati ya Mtume wa Allah na wao yakiwa ni shubiri moja au machache zaidi … hii ilikuwa katika mkesha wa kuamkia siku hiyo, na siku moja au mbili baadaye Mtume (saw) akasimamisha dola mjini Madina na kuunyanyua muundo wake kuujaza ulimwengu kwa nuru na kutangaza Haki …
* Ama miujiza ya viumbe ya usiku na mchana, kukolea kwa giza la usiku hufuatiwa na mwanga wa macheo ya kweli, na hiyo ni alama kwa watu wenye akili.
Hivyo basi, Umma wa Kiislamu haukati tamaa na rehema ya Allah, na hutambua kwamba baada ya uzito huja wepesi, baada ya shida huja suluhu, na mwanga wa asubuhi hufuatwa na giza la usiku … Kwa hivyo hautingishwi na mitetemeko, bali unafanya kazi na kufanya kazi kwa ikhlasi kwa ajili ya Allah na ni mkweli kwa Mtume wa Allah … Haudhuriwi na wale wanaopotoka kutokamana nao au kupotea; wengi wao hawakubali lolote isipokuwa Uislamu kama badali …
Kaka na dada zangu wapendwa: makafiri wale wameshusha pumzi za afueni baada ya Khilafah kuangushwa, kwa hivyo wanafanya uhalifu wao huku wakisalimika, hakuna anaye simama dhidi yao au kuwazuia kutokana na uhalifu wao au kuwarudisha kwao … Wanafahamu kuwa ngao ya Waislamu imeondolewa, na wanafanya kila juhudi yao kuzuia kurudi kwake. Hii ni kwa sababu wanajua kwamba mtengezaji wa ngao hii ni Khilafah, hapa ndipo pale hifadhi na heshima ya Waislamu ilipo. Hii ndio sababu wanawaandama wafanyikazi wanaofanya kazi ya kusimamisha tena Khilafah.
Hivyo basi, Hizb ut Tahrir imekuwa ndio shabaha ya mishale ya makafiri wakoloni na vibaraka wao watawala katika mataifa ya Waislamu. Hizb imetiwa katika misukosuko tofauti tofauti na mateso yaliyopelekea Shahada kama natija ya njama za makafiri na majasusi wa madhalimu na chuki za waovu. Hizb imepigwa marufuku na kuzuiwa katika ulimwengu wa Kiislamu hata katika zile nchi ambazo ziko wazi kwa vyama vyenye muundo tofauti tofauti mithili ya Indonesia; chama kimepigwa marufuku huko! Pamoja na zile biladi zilizofungua milango yake kwa vyama vya kila aina, hata vile vipotofu, mithili ya Tunisia, chama hiki kilipigwa marufuku! Ama kwa wanachama wa chama hiki, wafungwa wa madhalimu wanazungumzia mateso yao. Wanateswa katika magereza membamba, na katika magereza mapana wanadhalilishwa. Sasa ni kwa nini haya? Ni kwa sababu ya kuzungumza neno la Haki, ambalo chama inalitangaza, na huwachoma zaidi kushinda upanga, kwa sababu hawana hoja ya kusimama mbele ya neno la haki. Allah awaangamize, wamepotoka kiasi gani?
Kaka na dada zangu wapendwa: majanga haya yaliyousibu Umma huu na wafanyikazi wa Khilafah ni mabaya mno, na lau kama Allah hakuifanya Idd iwe chimbuko la furaha na njia ya raha na furaha nyoyoni mwa Waislamu, na mafungamano mazuri ya kizazi, na Umma kueneza salamu na heri njema ndani yake. Lau si kwa ahadi ya Allah (swt) kwamba izza na utukufu itarudi tena kwa Umma huu … Na lau kama si kwa bishara ya Mtume (saw) ya kurudi kwa Khilafah … Na lau kama si kwa kuwepo kwa chama chenye ikhlasi kwa Allah (swt), chenye ukweli kwa Mtume wa Allah (saw), kinachofanya kazi mchana na usiku, kikilingania na kumuomba Allah kufungua kupitia mikononi mwao wawe ndio wenye kusimamisha Khilafah na kurudisha izza ya Uislamu na Waislamu … pasi na mambo haya manne; ingekuwa vigumu kutabasamu, kwa sababu kuna donda moyoni, na tezi kooni, kutokana na majanga mengi yanayo wazunguka Waislamu mbele na nyuma, kulia na kushoto; Khilafah imetoweka kwa muda wa takriban karne moja. Waislamu wametawanyika na kugawanyika wakitawaliwa na wajinga (Ruwaibidha). Bila ya kutaja uvamizi wa wakoloni makafiri na washirika wao ndani ya mataifa na watu wake, kana kwamba nchi za Waislamu ni uwanja wa mizozo ya kumwaga damu zetu na kuchafua matukufu yetu.
Lakini, kwa ubaya wa majanga haya, Hizb ut Tahrir imedhaminiwa nusra ya Allah na kutimizwa kwa ahadi Yake na bishara ya Mtume Wake (saw). Haikati tamaa na rehema za Allah maadamu inafanya kazi ya kheri kwa idhini ya Mola wake. Chama hiki kinatambua kwamba wakati wa Khilafah umeandikwa Kitabuni. Kila siku inapopita inaifanya hii siku kukaribia zaidi. Chama mithili ya hiki hakiruhusu ukataji tamaa moyoni mwake na azma yake haidhoofiki na kujikakamua kwake hakuvunjiki, kwa idhini ya Al-Aziz Al-Hakim, bali mazito hukiongezea nguvu yake, kwani mazito ni katika mitihani ya wanaume, na wanachama wa chama hiki ni wanaume wa kikweli wanaomuomba Allah (swt) kuwafanya miongoni mwa wale ambao Allah (swt) amewazungumzia:
[رِجَالٌ لَا تُلْهِيهِمْ تِجَارَةٌ وَلَا بَيْعٌ عَنْ ذِكْرِ اللَّهِ وَإِقَامِ الصَّلَاةِ وَإِيتَاءِ الزَّكَاةِ يَخَافُونَ يَوْمًا تَتَقَلَّبُ فِيهِ الْقُلُوبُ وَالْأَبْصَارُ]…
“[Ni] wanaume ambao haiwashughulishi biashara wala mauzo kutokana na kumkumbuka Allah na kusimamisha swala na kutoa zaka wanaiogopa siku ambayo nyoyo na macho yatageuka [kwa hofu]” [An-Noor: 37]
Wanabeba ulinganizi huu kwa imani yao pamoja na baraka kutoka kwa Allah, na kwamba ulinganizi huu utainuka mikononi mwao, InshaAllah, na hapo ndipo ahadi ya Allah (swt) na bishara ya Mtume Wake zitakapotimia katika vigawanyo vitatu kwa Tawfiq (mafanikio) na nusra ya Allah:
* Kwanza: kurudi kwa Khilafah kwa njia ya Utume baada ya utawala huu wa kutenzana nguvu: Imam Ahmad, na At-Taylasi katika Musnad yake kutoka kwa Hadith ya Hudhayfah, amesema: “Mtume wa Allah (saw) amesema: «… ثُمَّ تَكُونُ جَبْرِيَّةً، فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»… “Kisha utakuwepo utawala wa kutenzana nguvu, na utakuwepo apendavyo Allah uweko, kisha atauondoa anapopenda kuuondoa, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume”
* Pili: kupitia kuing’oa dola ya Kiyahudi kwa mizizi yake. Muslim anasimulia katika Saheeh yake katika riwaya ya Abu Hurayrah, Allah awe radhi naye: Mtume wa Allah (saw) amesema:
«لَا تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى يُقَاتِلَ الْمُسْلِمُونَ الْيَهُودَ، فَيَقْتُلُهُمُ الْمُسْلِمُونَ…»، “Kiyama hakitasimama mpaka Waislamu wapigane na Mayahudi, na Waislamu watawauwa…” Na katika riwaya nyengine, Yeye (saw) amesema: «تُقَاتِلُكُمُ يَهُودُ، فَتُسَلَّطُونَ عَلَيْهِمْ» “Mayahudi watapigana na nyinyi, na nyinyi mutawatawala.”
* Tatu: Katika kufunguliwa Roma, kwa idhini ya Allah,
Ahmad amesimulia katika Musnad yake na Al-Hakim, na ilirekebishwa na kuidhinishwa na Az-Zahabi kutoka kwa Abi Qabeel, aliyesema: Tulikuwa na Abdullah bin Amr ibn al-Aas: Akasema: Tulipokuwa pambizoni mwa Mtume wa Allah (saw) tukiandika, Mtume wa Allah (saw) akaulizwa: “Ni upi kati ya miji miwili utafunguliwa mwanzo: Kostantiniya au Roma?” Mtume wa Allah (saw) akasema: «مَدِينَةُ هِرَقْلَ تُفْتَحُ أَوَّلًا، يَعْنِي قُسْطَنْطِينِيَّةَ»“Mji wa Hiraqla ndio utafunguliwa mwanzo, yaani Kostantiniya”. Kostantiniya ishafunguliwa, na Roma itafunguliwa, InshaAllah.
Kaka na dada zangu wapendwa: kwa kutafakari hayo ya juu kwa akili timamu na ufahamu wenye hekima ni matarajio baada ya uchungu, na raha na bishara njema baada ya uhalisia wenye huzuni, na wepesi baada ya uzito, na furaha baada ya mateso ya muda mrefu, na kushuka kwa dua na rehema za Allah baada ya “Sisi ni wa Allah na Kwake Yeye tutaregea” … Kisha kheri na nusra … kheri na nusra … kisha kheri na nusra.
[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]
“Na siku hiyo watafurahia waumini. Kwa nusra ya Allah, humnusuru amtakaye na Yeye ndiye Mwenye nguvu Mwenye rehma” [Ar-Rum: 4-5]
Kwa kutamatisha, namuomba Yeye Subhaanahu kwamba Idd hii yenye kheri na baraka irudi tena hali ya kuwa Umma wa Kiislamu uko chini ya kivuli cha bendera ya Uqab ya Khilafah Rashida, bendera ya Laa Ilaha Illallah Muhammadur Rasulullah
Na namuomba Allah (swt) kwamba wanachama wa Hizb ut Tahrir wawe msitari wa mbele wa Umma huu, wakisimama nao chini ya kivuli cha Khilafah Rashida … Ama kwa wanachama waliofariki kabla ya kurudi tena kwa Idd hii, namuomba Allah (swt) kuwaruzuku sehemu chini ya kivuli chake siku ambayo hakutakuwa na kivuli isipokuwa chake Yeye (swt). Allah ni Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.
Katika tamati yangu ya mwisho, nawatumia salamu zangu, nawaombea Dua ya kheri kwenu nyinyi.
Wasalamu Alaikum Wa Rahmatullahi Wa Barakaatuhu.
Ndugu Yenu
Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah
Amiri wa Hizb ut Tahrir
Usiku wa kuamkia 10 Dhul Hijjah 1439 H
Ikiafikiana na 21/08/2018 M
Maoni hayajaruhusiwa.