Ziara Ya Biden Ya Dakika Za Mwisho Afrika: Kuimarisha Ajenda Ya Ukoloni Na Unyonyaji Wa Marekani

بسم الله الرحمن الرحيم

Habari:
Jumatano ya tarehe 04/12/2024 Rais wa Marekani Joe Biden alikhitimisha ziara yake ya siku tatu nchini Angola. Katika siku ya mwisho ya ziara yake, Biden alitembelea mradi wa Ukanda wa Lobito, mradi wa reli inayojengwa kwa ufadhili wa Marekani yenye kilomita 1,3000 inayoanzia Zambia ambapo kwenye utajiri kubwa wa madini ya shaba hadi bandari ya Lobito kusini magharibi mwa taifa la Angola. Pia, Biden alifanya mkutano na maraisi wa Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Zambia na Makamu wa Rais wa Tanzania (VOA Africa 05/12/2024).
Maoni:
Ziara ya Biden nchini Angola inalenga kuimarisha ajenda ya ukoloni pamoja na unyonyaji wa rasilimali za Angola na nchi jirani nyuma ya guo la mpango unaoitwa Uwekezaji wa Kigeni (FDI).
Mnamo Juni 2022, Marekani ilitangaza lengo la kukusanya dola bilioni 200 kupitia PGII (Ushirikiano wa Miundombinu na Uwekezaji wa Kimataifa) kuimarisha miundombinu, nishati, kimwili, kidijitali, afya na miundombinu inayohimili hali ya hewa, kwa lengo la kuimarishwa uwekezaji katika maeneo muhimu ya kiuchumi, ikiwa ni pamoja na Ukanda wa Lobito.
Pia, wakati wa kikao cha Jukwaa la Kimataifa la Ukuaji wa Uchumi(Global Gateway) mwezi Oktoba 2023, Umoja wa Ulaya(EU) na Marekani zilitia saini – pamoja na Angola, DRC, Zambia, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Shirika la Fedha la Afrika (AFC) – Mkataba wa Makubaliano (MoU) unaohusiana na uendelezaji wa Ukanda wa Lobito na Reli ya Zambia -Lobito.
Hakika huu si mradi kwa ajili ya maslahi na maendeleo kwa watu wa Angola na Afrika, bali ni unyonyaji wa kimagharibi na ajenda ya ukoloni.
Reli hii ya Lobito ni njia ya kimkakati itayounganisha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yenye utajiri wa rasilimali nyingi na Angola kupitia Zambia, hadi bandari ya Lobito kwenye Bahari ya Atlantiki likiwa lango kuu la kupeleka rasilimali kwa mataifa ya kikoloni.
Ukanda huo (wa Lobito) ambao kwa kiasi kikubwa uko chini ya Marekani utaruhusu usafirishaji wa haraka wa madini ya kobalti na shaba, miongoni mwa madini mengine, yanayochimbwa kutoka mji wenye utajiri wa madini ya kimkakati wa Kolwezi wa DRC hadi mataifa ya magharibi. Kwa hiyo, mradi huu ni kwa ajili ya kuwezesha maslahi ya kibepari ya kikoloni.
Inaonekana pia sababu nyingine nyuma ya ziara ya mwisho ya Biden kwa Afrika huko Angola kuwa ni jaribio la kudhibiti ushawishi wa China huko Angola, Afrika ya Kati na Afrika kwa ujumla.
Kulingana na Jarida Jornal de Angola, kutoka mwaka 2018 hadi Machi 2022, China ilikua miongoni mwa wawekezaji watatu wakubwa nchini Angola. Umoja wa Falme za Kiarabu uliongoza uwekezaji wa kigeni (FDI) kwa dola milioni 351.7, ikifuatiwa na Uingereza kwa dola milioni 283.1, ilhali China iliwekeza dola milioni 225.
Mnamo Septemba 2024, Shirika la Uhandisi la serikali ya China (China State Engineering Corporation) lilitia saini makubaliano ya kuendesha Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), njia nyingine ndogo ya reli katika ukanda huo wa Lobito ambayo inanufaisha sana wawekezaji wa China na kiungo cha Zambia ya kati na bandari ya Dar-es- Salaam nchini Tanzania.
Kwa hivyo, kwa Marekani kukabiliana na athari na ushawishi wa kiuchumi wa China katika eneo hili inalazimika kufadhili mradi wa Ukanda wa Lobito, na raisi Biden alilazimika kufanya safari katika wiki zake za mwisho kabla ya kuondoka ikulu ya Marekani (Whitehouse)
Marekani haitasitisha miamala yake ya kishenzi ya kibepari nchini Angola, ambapo kuanzia miaka ya 1970, alikuwa akiwaunga mkono waasi wa UNITA ambao walisababisha mauaji, ukatili na uharibifu mkubwa wa Angola hadi miaka ya 2000 pale maslahi ya Marekani yalipopatikana.
Dola ya Kiislamu ya Khilafah ndiyo pekee yenye uwezo na nguvu ya kukomesha unyonyaji wa kibepari wa kikoloni kwa wanadamu. Kurejeshwa kwa dola hiyo utakuwa ni ukombozi wa kihistoria wa ulimwengu wa Kiislamu na mataifa mengine dhaifu yanayoendelea kama vile Angola nk.
Imeandikwa na Said Bitomwa
Mjumbe wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Tanzania
Kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Maoni hayajaruhusiwa.