“Wanataka kuizima nuru ya Allah kwa midomo yao, lakini Allah ni Mwenye kutimiza nuru yake, hata kama makafiri watachukia.”
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
﴿يُرِيدُونَ لِيُطْفِئُوا نُورَ اللَّهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَاللَّهُ مُتِمُّ نُورِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ﴾
“Wanataka kuizima nuru ya Allah kwa midomo yao, lakini Allah ni Mwenye kutimiza nuru yake, hata kama makafiri watachukia.”
(Imetafsiriwa)
Mwishoni mwa mkutano wa 32 wa kamati ya kieneo ya kupambana na ugaidi ya Shirika la Ushirikiano la Shanghai (SCO), uliofanywa mnamo Alhamisi, Aprili 5, 2018 jijini Tashkent, Jenerali Sergev Smirnov, Naibu wa Kwanza wa Mwenyekiti wa Huduma ya Usalama ya Majimbo ya Urusi alisema: “Kwa mtazamo wetu, chama cha Kiislamu cha Hizb ut Tahrir ni hatari kwa sababu ya amali zake na itikadi yake, kwa hivyo, kilitangazwa kuwa chama cha kigaidi, na hiyo ndiyo sababu kimeangaziwa haswa”. Aligusia kwamba wakati wa mkutano huo uamuzi ulichukuliwa kuunda mbinu za kukipiga vita chama cha Kiislamu cha Hizb ut Tahrir.
Haishangazi kwa jenerali huyu kutambua kufeli kwa serikali ya Urusi iliyo asisiwa na mkomunisti Stalin kugandamiza kukua kwa ulinganizi wa Uislamu, ambao hupenya nyoyoni mwa waumini nchini Urusi wanaotafuta ubebaji wa ujumbe wa kheri kwa ulimwengu mzima, na hata mamia na maelfu ya Warusi waliokuwa katika giza la ukafiri wanaingia katika Dini ya Allah.
Ni kinaya kwa jenerali huyu wa kijeshi kunyosha misuli, kujihami kwa wingi wa mashini za kuua, vitisho na ugaidi, katika jaribio la kutapatapa la serikali ya Urusi kuziba jua la ukweli wa itikadi ya Kiislamu iliyo jengwa kwa msingi wa wahyi wa kweli.
Siku za nyuma ulimwengu ulishuhudia kuundwa kwa miungano mikuu ya kijeshi; makubaliano ya Warsaw dhidi ya shirika la kujihami la NATO. Lakini pindi Jenerali Smirnov alipotangaza kuwa itikadi ya Hizb ut Tahrir inaifanya kuwa hatari, huu ni utambuzi ambao yeye na wenzake katika serikali ya Kistalini hawana itikadi sahihi kuhusu maisha, ulimwengu na mwanadamu, licha ya kipindi chao cha mpito kutoka kwa giza la ukomunisti na kwenda katika muozo wa urasilimali, kwani itikadi zote mbili zimejengwa kwa msingi wa batili ambayo ni dhaifu kushinda nyumba ya buibui. Kama kweli wangekuwa na chembe ya tafakari na fikra, wangekubali kukabiliana na hoja kwa hoja, lakini wao ni mithili ya wale waliowatangulia miongoni mwa makatili wa zama za nyuma; hoja yao si nyengine isipokuwa kuua, kukandamiza na kutesa. Allah ibariki itikadi hii ya kweli ya Kiislamu, ambayo watu hawa wanailingania kuwahadaa na kupanga njama dhidi ya vijana wake ambao ni vijana wema wa Uislamu.
Ikiwa twajua kwamba chama hiki kinacho shukiwa kina jumuisha zaidi ya asilimia 60% ya idadi ya watu duniani, tuna haki ya kustaajabu. Je, itikadi ya Kiislamu kweli ni hatari inayo hitaji kukusanywa kwa nguvu zote za nchi hizi? Sisi katika yale tunayoyajua hatujui kwamba Hizb ut-Tahrir ina jeshi,ndege za kivita au bajeti za kijeshi zenye thamani ya mabilioni ya dolari. Ni kwa nini basi watu hawa wanalingania watu dhidi ya Hizb na vijana wake wema ambao silaha yao pekee ni Imani yao kwa Allah Ta’ala Mola wa ulimwengu na kujitolea kwao kuikomboa Dini yao kwa gharama ya damu zao na maisha yao?
Lakini kilicho kibaya na chenye uchungu zaidi ni kuwa wale wanaodai kuwa watawala wa Waislamu (kuanzia Uzbekistan mpaka Kazakhstan mpaka Pakistan waliojiunga na shirika hili mnamo Juni 2017) ni wepesi wa kudhihirisha hamu yao ya “kupigana na ugaidi”!!
Masikitiko ni kuwa mbilikimo hawa hawasomi kutokana na mafunzo ya hatma ya wale waliowatangulia miongoni mwa makatili wa karne zilizo pita.
﴿أفَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنْظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ كَانُوا أَكْثَرَ مِنْهُمْ وَأَشَدَّ قُوَّةً وَآثَارًا فِي الْأَرْضِ فَمَا أَغْنَىٰ عَنْهُمْ مَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴾
“Je, hawajatembea katika ardhi na wakaona namna ulivyo kuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Walikuwa ni wengi kuliko wao na wenye nguvu na wenye ushawishi katika ardhi, lakini hawakutosheka na walivyokuwa wakivichuma.” [Ghafir: 82].
Hivyo basi, Enyi Umma wa Kiislamu!
Furahieni kheri, kwa kuona viongozi wa ukafiri wakitambua kuwa hawana nguvu dhidi ya Aqeeda yenu sahihi, ambayo mbingu na ardhi zimejengwa juu yake. Kwa hivyo, njooni mufanye kazi na Mashabab wa Hizb ut Tahrir wanaofanya kazi kuipa nguvu Dini hii na kusimamisha Dola ya Khilafah Rashidah katika njia ya Utume, ili kumulika miale ya jua la Uislamu kwa wanadamu wote ambao usiku wake umerefuka, na macheo yake mapya yamekaribia, kwa idhini ya Allah, chini ya uadilifu na rehma ya Uislamu.
﴿وَاللهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ﴾
“Na Allah ni mshindi juu ya jambo lake, lakini wengi wa watu hawajui.” [Yusuf: 21]
Dkt. Osman Bakhach
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
H. 20 Rajab 1439 | Na: 1439 AH /020 |
M. Jumamosi, 07 Aprili 2018 |