Unyeti wa Tukio La Hijra

Tukiwa katika ijumaa ya mwisho katika mwaka huu wa 1439 Hijria karibuni InshaAllah tutaingia mwaka mpya wa Kiislamu.

Lazima tukumbuke kwamba Masahaba katika zama za Khilafah ya Umar bin Khatwaab kwa umoja wao waliwafikiana kuanza kuihisabu kalenda ya Kiislamu kwa kuanzia tukio la Hijra. Ndio maana kalenda yetu ya Kiislamu hadi leo inaitwa kalenda ya Hijria.

Pamoja na kuwepo matukio mbalimbali makubwa na matukufu katika tareekh ya Kiislamu kama kuzaliwa Mtume SAAW, . kupewa Utume, Israi na Miiraj, Vita vya mwanzo vya Badr, Fathi Makka nk. Lakini yote hayo masahaba waliyawacha wakachagua tukio la Hijra kuwa ndio nukta kianzio ya kuihisabu kalenda ya Kiislamu.

Hii ni kwa sababu Hijra ndio tukio lililoutoa Uislamu kutoka kuwa katika nadharia na kuuwezesha kusimamia Umma kivitendo kwa kuasisi dola ya mwanzo ya Kiislamu.

Mpaka leo kalenda yetu imebakia na jina hilo la Hijria ikiwa ni ujumbe kwetu tuliobakishiwa mpaka Siku ya Kiama juu ya unyeti wa na uwajibu wa suala la utawala wa Kiislamu.

Hii ni dhima kubwa kwetu.

Katika mwezi wa Muharram ambao ndio mwezi wa mwanzo wa Kiislamu ni muhimu Waislamu kukumbushwa kwa ufafanuzi tukio la Hijra, yaliyojiri katika maandalizi ya tukio hilo na lengo lake kwa upana. Lisizungumzwe tukio la Hijra kama hadithi tu.

#UislamuMfumoMbadala

Masoud Msellem

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir Tanzania

Ijumaa 27 Dhulhijjah 1439 Hijria / 07 Septemba 2018

Masjid Rahmah- Buguruni Madenge

Maoni hayajaruhusiwa.