Umarufu Wa Cristiano Ronaldo Na Lionel Messi
Cristiano Ronaldo na Lionel Messi hawa ni wachezaji Maarufu zaidi Duniani katika kipindi cha Miaka kadhaa iliyopita, waliojizolea sifa lukuki miongoni mwa Vijana na Wanamichezo kwa ujumla na kuleta ubishi usiokuwa na Kikomo ni nani Bora zaidi ya Mwingine?
Nguli hawa wameacha athari Kubwa ulimwenguni kote nje na ndani ya Uwanja namaanisha hadi katika maisha binafsi.
Jambo la kusikitisha miongoni mwa Waislamu ni Kuingia katika mkumbo huu huku wakiamini Mesi ama Ronaldo ni Bora zaidi ya Mwingine na kusahau kipimo cha Uislamu juu ya hili.
Kwa Mujibu wa Uislam Mbora zaidi mbele ya Mungu (Allah) ni Mchamungu Pekee (Surat Al-hujuraat aya 13)
Tukiangalia kwa makini hawa Wachezaji wote si Waislamu (Makafiri), Hawana sifa za kutukuzwa wala kuwekwa walau katika ubora kutokana na Kipimo cha Allah juu ya Ubora.
Pia kibaya zaidi Waislamu wamejawa na Mapenzi nao kuliko hata Mwenyezi Mungu (Allah SAAW) na Mtume (SAAW), na kuacha kipimo cha Kisheria juu ya mapenzi baina yetu, kwa mujibu wa Uislamu watu tunatakiwa kupendana kwa ajili ya Allah pekee si Vinginevyo.
Chini ya Nidhamu ya Kidemokrasia Wasanii na wanamichezo wanaowaita kiyoo cha jamii wamepewa nafasi Kubwa sana kwa kupewa kipaumbele huku vyombo vya Habari vikitumika kuwatangaza sana kwani wamebeba fikra msingi ya nidhamu hii fisidifu na Kuharibu jamii.
Serikali ya Kiislamu (Khilafah) pekee ndio itarudisha hadhi ya Wanaostahiki kuwa kiyoo cha jamii kama inavyotuonyesha tarekh wakati uislamu unatawala kwa karne 13 Mtu aliyebeba Uislamu na kuufanyia kazi huyu ndio aliyekuwa kiyoo kwa Ummah Kama Khalifah Omar Ibn Abdul-Aziz.
Turejee kwa Allah subhana ta’allah, na kipimo cha ubora miongoni mwetu kiwe ni Uchamungu na tupendane kwa ajili ya Allah Karim, hakika hivi ndio vipimo sahihi juu ya Ubora wa Wanadamu na Mapenzi miongoni mwao.
Maoni hayajaruhusiwa.