Ukiishi Mpaka Rajab, Utaona Maajabu
بسم الله الرحمن الرحيم
عش رجبا ترى عجبا
Huu ni msemo wa kale wa Kiarabu unaotafsirika kama “ishi mpaka (mwezi) Rajab, utaona maajabu”. Asili ya msemo huu maarufu ni kutoa tahadhari ya mambo yanayoweza kutokea baada ya muda fulani na hivyo kutaka watu wachukue hatua kujiepusha na madhara yanayoweza kutokea. Kwa munasaba na mwezi uliosemwa, yaani mwezi wa Rajab ambao ni mwezi wa saba katika kalenda ya Kiislamu, hakika kuna maajabu mengi ambayo ummah huu umeyashuhudia bila kutarajiwa.
Yamekuwa maajabu kwa sababu ni mambo ambayo lau yangesemwa au kipindi yanasemwa kuwa yanaweza kutokea yalionekana ni ndoto na hayawezekani kabisa kutokana na uhalisia wa kipindi hicho, lakini baada ya karne na karne hatimaye yalitokea na kuleta uhalisia mpya katika historia ya ummah huu mtukufu wa Kiislamu.
Baadhi ya matukio muhimu yaliyobadilisha historia ya Uislamu ni pamoja na safari ya israi na miiraj.Hii ilikuwa ni safari ambayo Allah alimpeleka Mtume wake kimiujiza baada ya kuondokewa na watu nyeti na kumpa nguvu kufuatia upinzani wa Maqureishi. Pia ilikuwa ni kama bishara ya ushindi ambapo mara baada ya kurudi alipewa baayah ya kwanza iliyozaa baaya ya pili iliyopelekea kupata nusra. Tukio lingine ni ukombozi wa Al-Quds na Sallahudin Ayoub.Baada ya Msikiti mtukufu wa Baiutil Muqadas kuwa chini ya Makruseda kwa miaka mingi, Waislamu waliweza kuukomboa na kuurejesha tena katika mamlaka yao chini ya kamanda Sallahudin Ayoub (Allah Amrehemu) katika Tarehe 27 Rajab.
Tukio kubwa, baya kabisa kutokea katika mwezi wa Rajab ni kuangushwa rasmi kwa serikali ya kiulimwengu ya Kiislamu yaani Khilafah. Khilafah ya mwisho, Khilafah ya Bani Uthumaniya (The Ottoman Caliphate) iliangushwa tarehe 28/Rajab/1342H sawa na tarehe 03/March/ 1924M katika Uturuki chini ya Mustafa Kemal Ataturk.
Mtume wetu(SAW) alituhadharisha akatuambia:
عَنْ ثَوْبَانَ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ” يُوشِكُ الأُمَمُ أَنْ تَدَاعَى عَلَيْكُمْ كَمَا تَدَاعَى الأَكَلَةُ إِلَى قَصْعَتِهَا ” . فَقَالَ قَائِلٌ وَمِنْ قِلَّةٍ نَحْنُ يَوْمَئِذٍ قَالَ ” بَلْ أَنْتُمْ يَوْمَئِذٍ كَثِيرٌ وَلَكِنَّكُمْ غُثَاءٌ كَغُثَاءِ السَّيْلِ وَلَيَنْزِعَنَّ اللَّهُ مِنْ صُدُورِ عَدُوِّكُمُ الْمَهَابَةَ مِنْكُمْ وَلَيَقْذِفَنَّ اللَّهُ فِي قُلُوبِكُمُ الْوَهَنَ ” . فَقَالَ قَائِلٌ يَا رَسُولَ اللَّهِ وَمَا الْوَهَنُ قَالَ ” حُبُّ الدُّنْيَا وَكَرَاهِيَةُ الْمَوْتِ ”
“Mataifa yanakaribia kuitana dhidi yenu kama vile watu wanavyoitana watu kwenye sahani ya chakula. Akasema mwenye kusema je ni kutokana na uchache wetu zama hizo? Akasema laa bali nyinyi zama hizo mtakuwa wengi lakini mtakua kama povu la mafuriko.. hapo MwenyeziMungu ataondoa kwenye mioyo ya maadui zenu khofu juu yenu na kutia kwenye nyoyo zenu Wahn… akauliza mwenye kuuliza: ewe mtume wa MwenyeziMungu na nini wahn? Akasema ni kupenda dunia na kuchukia kifo.” [Sunan ya Abi Daud]
Kisha akatutahadharisha na kutupa bishara njema Mtume (SAW) pale alipotuambia:
»تَكُونُ النُّبُوَّةُ فِيكُمْ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً عَاضّاً فَيَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ «ثُمَّ سَكَتَ.
“Utume utakuwa kwenu kwa muda atakao Mwenyezi Mungu kisha atauondoa atakapo kuuondoa, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume itakuwepo kwa muda atakao Mwenyezi Mungu kisha ataiondoa atakapo kuiondoa, kisha utakuwepo ufalme wa kurithishana utakuwepo kwa muda atakao Mwenyezi Mungu kisha atauondoa atakapo kuuondoa, kisha utakuwepo utawala wa kiimla utakuwepo kwa muda atakao Mwenyezi Mungu kisha atauondoa atakapo kuuondoa, kisha itakuwepo Khilafah kwa Njia ya Utume”
Katika maneno haya matukufu katika hadith hizi mbili kuna mazingatio makubwa, katika hadith ya kwanza Mtume anawaambia masahaba kuwa itafikia muda ummah huu utaonewa na kudhalilishwa na kudhulumiwa licha ya wingi wao. Kwa masahaba kwao ilikuwa ni kama ndoto na jambo likilokuwa haliwezekani kutokea. Ilikuwa haiingii akikini kuwa kwa nguvu walizokuwa nazo inaweza ikafikia siku wakawa madhalili kiasi hicho.
Katika hadith ya pili Mtume anatahadharisha kuwa kutakuwa na utawala wa kuumiza, muovu, wa kikafiri utakaowaua, kuwatesa na kuwadhulumu Waislamu kisha akatupa bishara njema kuwa itarejea tena serikali ya kiulimwengu ya Kiislamu Khilafah kwa njia ya Mtume.
Na hatimaye maneno yakatokea, kwa msaada wa kafiri mkoloni, wanafiki wa Kiarabu na Kituruki wakaangusha Khilafah na zikaanza kuenea dhulma na mauaji katika biladi zetu. Kisha ukatawala ulimwengu utawala wa kikatili, wa kikafiri, usiojali watu, utawala wa Kibepari. Tangu muda huo ulimwengu umetapakaa muda za Waislamu. Mauaji ya kutisha dhidi ya Waislamu yametokea na dhulma za kila aina.
Kwahiyo kama msemo unavyosema, hakika tumeshuhudia maajabu katika mwezi huu wa Rajab, maajabu ya kuangushwa kwa Khilafah na kutumbukia ummah katika udhalili wa kutisha. Hali hii inatilia nguvu juu ya kufanya juhudi kurejesha tena nguvu yetu, ngao yetu, serikali yetu, dola yetu, Khilafah Rashidah ya pili na ya mwisho kwa njia ya Mtume na kuukomboa ulimwengu na walimwengu kutokana na dhulma za Ubepari kama ambavyo tumepewa bishara njema na Mtume wetu (SAW) aliposema:
ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ «ثُمَّ سَكَتَ
“…Kisha itakuwepo Khilafah kwa Njia ya Utume”
Risala ya Wiki No. 127
17 Rajab 1443 Hijri /18 Februari 2022 Miladi
Afisi ya Habari – Hizb ut Tahrir Tanzania http://hizb.or.tz/
#WahyiChimbukoLaThaqafaYetu
#KataaUislamuMamboLeo
Maoni hayajaruhusiwa.