Ufisadi Wa Mayahudi na Maangamizi Yao Kwa Mujibu Wa Quran

بسم الله الرحمن الرحيم

Suratul Bani Israil inabashiri mwisho wa kijidola bandia cha Israil na kuangamia kwake. Jambo hilo linatupa imani, matumaini na kupunguza machungu na huzuni nyoni hususan wakati huu, ambapo unyama, ukatili na ushenzi unaofanywa leo ndani ya eneo tukufu la Aqsa, kibla cha kwanza cha Waislamu umeshtadi na kuruka mipaka.
Sura hii imetanguliwa na Suratul Annah’li, na mara nyingi huwa kuna uhusiano wa siyaq (chain) kati ya mwisho wa sura na mwanzo wa sura inayofuatia. Aya za mwisho wa Suratul Suratul Annah’li zikimtaka Mtume Muhammad SAAW na Waumini kuzidisha subra kutokana na hali tete aliyomkumba yeye na maswahaba zake. Kwani wao walipitia maudhi na mazito kutokana na vitimbi vilivyofanywa na washirikina wa Makka kwa kuwaadhibu maswahaba zake, kuwaua, kuwafilisi na wengine kulazimika kuhama makazi yao kwa muda kutokana na dhulma walizokuwa wakifanyiwa na washirikina wa Kiquraishi.
Kutokana na hali hiyo tete waliopitia Waumini na Mtume Muhammad SAAW ndipo Mola aliteremsha aya hizi za mwisho ndani ya Suratul Annah’li:
وَاصْبِرْ وَمَا صَبْرُكَ إِلاَّ بِاللَّهِ وَلاَ تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَلاَ تَكُ فِي ضَيْقٍ مِمَّا يَمْكُرُونَ (النحل: 127
‘Na fanya subra na kusubiri kwako kusiwe ila kwa ajili ya Mwenyezimungu tu wala usihuzunike kwa ajili yao(wanayoyatenda) wala usiwe katika dhiki kwa sababu ya hila wanazozifanya.’ (TMQ 16:127)
إِنَّ اللَّهَ مَعَ الَّذِينَ اتَّقَوْا وَالَّذِينَ هُمْ مُحْسِنُونَ (النحل: 128
‘Kwa hakika Mwenyezimungu yupo pamoja na wale wanaomcha na wale wafanyao wema’ (TMQ 16:128)
Baada ya aya hizo zikafuatiwa na aya za mwanzo wa Suratul Bani Israil ambazo zimeweka bayana ushindi wa Waumini na kuangamia kwa mayahudi.
Sura hii (Bani Israil) iliteremka wakati Waislamu wakiwa katika hali tete, Mtume SAAW na maswahaba zake wakitaabika kwa vitimbwi, maudhi na idhilali za maquraishi. Pia wakati sura hii inateremshwa hapakuwa na mwingiliano wa moja kwa moja kati ya Mtume SAAW na jamii ya kiyahudi iliyokuwa ikiishi Madina na viunga vyake, ilhali sura hii iliteremka kabla ya Mtume SAAW kuhamia Madina.
Lakini kwa kuwa Mtume wetu SAAW alikuwa amebeba ujumbe wa kiulimwengu, na mayahudi ni moja kati ya jamii ya kibinadamu ambayo Mola SWT aliwachagua kabla ya kuja Mtume SAAW, Mola SWT akamteremshia Mtume SAAW aya hizi ili kumfungulia na kumuonyesha kuwa ujumbe alioubeba hauishii kwa maquraishi wa Makka pekee, bali ni ujumbe wa ulimwengu mzima.
Sasa tukija katika Surat Bani Israil namna ilivyotueleza juu ya maangamizi ya wayahudi, tukumbuke kuwa Quran ni muujiza pekee wenye kukhabarisha kwa uhakika matukio yatakayotokea (future), yapo yaliyotokea katika uhai wa Mtume SAAW na yapo mengine yalijoiri na yatajiri wakati ujao baada ya kufa kwake.
Mola SWT anasema:
وَقَضَيْنَا إِلَى بَنِي إسْرائِيلَ فِي الْكِتَابِ لَتُفْسِدُنَّ فِي الأَرْضِ مَرَّتَيْنِ وَلَتَعْلُنَّ عُلُوًّا كَبِيرًا (الإسراء: 4).
‘Tukawafunilia Bani Israel katika kitabu chao (Taurat) bila shaka nyinyi mtafanya ufisadi (mkubwa) katika nchi mara mbili, na kwa yakini mtatakabari kutakabari kukubwa.’ (TMQ 17:5)
Kwa mujibu wa aya hiyo mayahudi watafanya ufisadi mkubwa mara mbili:
Akaendelea Allah Taala kutueleza:
فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ أُولاَهُمَا بَعَثْنَا عَلَيْكُمْ عِبَادًا لَنَا أُولِي بَأْسٍ شَدِيدٍ فَجَاسُوا خِلاَلَ الدِّيَارِ وَكَانَ وَعْدًا مَفْعُولاً
‘Basi itakapofika ahadi (ya kulipwa kwa ajili ya uharibifu) wa kwanza katika hiyo miharibifu (miwili), tutakuleteeni watu wetu wenye mapigano makali nao wataingia mijini mwenu kila upande na hii itakuwa ni ahadi itakayotimizwa. (TMQ 17:5)
Ufisadi wa kwanza wa Mayahudi ni ule walioutenda pale Mtume SAAW alipoingia Madina baada ya kuasisi serikali yake ya mwanzo ya Kiislamu. Wakati ule Mayahudi walidhihirisha uadui mkubwa kwa Uislamu na Waislamu kiasi kwamba waliweza kupinga maneno ya Mola SWT wazi wazi ilhali ukweli wakiujua kama watoto wao, kuwafitini Waumini, kuwadhalilisha ndani ya viunga vya Madina kama walivyofanya mayahudi wa Buni Qainuqai kwa mwanamke wa Kiislamu ndani ya soko, wakila njama na maqureishi na waarabu wengine kumpiga vita Mtume SAAW, wakivunja mikataba kama walivyofanya Bani Quraiza, walifanya jaribio la kumuuwa Mtume SAAW nk. Ndipo Mtume SAAW yeye na maswahaba wake wakawapiga kipigo kikali na kuwafurusha Mayahudi ndani ya Madina, na baada yake wakafurushwa kwa agizo lake hadi nje ya Bara Arabu kamwe.
Ikumbukwe kuwa kabla ya Mtume SAAW kuhamia Madina Mayahudi walikua na ushawishi na dori kubwa hasa katika mustakbali wa siasa na uongozi ndani ya Madina. Makabila mawili makubwa ya Madina ya Aus na Khazraj walikuwa wakipigana wao kwa wao mara kwa mara kutokana na fitina ua uchonganishi wa mayahudi. Hivyo, makabila hayo licha ya ukumbwa wao hawakuwa na dori thabiti katika kutawalia na kushikilia mambo ya utawala pamoja na kuwa wao ndio waliokuwa na hatamu, nguvu na nusra katika mji huo.
Amma ufisadi wa pili wa Mayahudi umetajwa na Mola SWT katika aya hii:
إِنۡ أَحۡسَنتُمۡ أَحۡسَنتُمۡ لِأَنفُسِكُمۡ‌ۖ وَإِنۡ أَسَأۡتُمۡ فَلَهَا‌ۚ فَإِذَا جَآءَ وَعۡدُ ٱلۡأَخِرَةِ لِيَسُـۥۤـُٔواْ وُجُوهَڪُمۡ وَلِيَدۡخُلُواْ ٱلۡمَسۡجِدَ ڪَمَا دَخَلُوهُ أَوَّلَ مَرَّةٍ۬ وَلِيُتَبِّرُواْ مَا عَلَوۡاْ تَتۡبِيرًا
‘Mkifanya wema (enyi mayahudi) mnajifanyia nafsi zenu, na mkifanya ubaya mnajifanyia nafsi zenu wenyewe, na itakapofika ahadi ya malipo ya uharibifu wa mwisho (wa pili) tutakuleteeni watu wenye nguvu wazidhalilishe nyuso zenu na wauingie msikiti kama walivyoingia mara ya kwanza, na wawangamize muangamizo mkubwa [17:7TMQ]
Ufisadi wa pili wa Mayahudi katika aya hii ni ufisadi unaofanywa na Mayahudi leo katika mji mtukufu wa Quds na ardhi ya Palestina kwa ujumla.
Ikumbukwe kuwa eneo tukufu la Quds na Palestina kwa ujumla ni eneo ambalo Waislamu walilifungua na kuliingiza katika himaya ya Kiislamu wakati wa Khilafah ya Umar bin Al-Khattab (ra.)
Wakati huo eneo hilo lilikuwa chini ya dola ya wakristo wa kiRoma iliyojulikana kama Byzantine Empire ambao waliwatoa mayahudi karne nyingi kabla ya hata ya Mtume SAAW. Eneo hili liliweza kunyakuliwa tena na waingereza mwaka 1918, kisha kwa msaada wao wakaanza kuwapatiwa Mayahudi, na jambo hilo likafanywa rasmi mnamo mwaka 1948 kwa kuasisiwa kijidola bandia cha mayahudi (Israel). Yote hayo yamejiri kutokana na kukosekana ulinzi na usimamizi baada ya kuanza kudhoofika dola ya Kiislamu ya Khilafah Uthmania hadi kufikia kuanguka kwake huko Istanbul mwaka 1924.
Leo Israeli amekalia kimabavu na kulichukua eneo lote, hutenda atakalo katika kuuwa, kupora nyumba na mali ndani ya Palestina akipiga mabomu na kuangamiza watoto, wakinamama, wazee na kuunajisi msikiti mtukufu wa Aqsa.
Lakini kwa bishara ya Quran, pia na kwa Hadithi za Mtume SAAW ufisadi huu utaondolewa na waja wa Mwenyezi Mungu, waja wenye nguvu, licha ya nguvu hasa msaada wanaoupata mayahudi kutoka kwa madola ya kimagharibi hususan Marekani. Pindi muda wa kuangamia kwao utakapofika, Mola SWT Atawaleta waja wenye nguvu ambao watawaangamiza mayahudi, kuwatoa ndani ya Quds na Palestina na kulikomboa eneo lote kwa ujumla na wataurejeshea hadhi na haiba yake Msikiti Mtukufu na eneo lote kama ilivyokuwa mwanzo. Jambo hilo kwa Allah Taala ni sahali.
Kwa bishara hii ya Quran na kutoka ‘nass’ nyingine, ni wajibu Waislamu kutuliza nafsi zetu kutokana na ushindi tulioahidiwa. Lakini hilo ni kwa upande wa kiimani. Katika upande wa matendo (hukmu sharia) wakati tukiwa na yakini juu ya ushindi na nusra hiyo huwajibika kutenda yaliyo katika mzunguuko wa kibinadamu kama tulivyoagizwa na sharia, na tusipotenda tutakuwa tunatenda dhambi. Na yaliyo katika amri tuliyoamrishwa ni kufanya kazi ya ulinganizi ili kurejesha tena Khilafah itakayoanzia katika nchi kubwa za Waislamu, ambayo hakuna shaka yoyote ndio itakayokomboa, kuwafurusha mayahudi na kurejesha furaha ya kweli kwa Waislamu na walimwengu kwa jumla.
Issa Nasibu
Risala ya Wiki No. 103
16 Dhu al-Qi’dah 1442 Hijri / 20 June 2019 Miladi
Afisi ya Habari – Hizb ut- Tahrir Tanzania

Maoni hayajaruhusiwa.