Ubepari huzalisha bidhaa feki na bandia

2

Vyombo vya habari vya Tanzania na vile vya kimataifa hivi karibuni viliripoti shutuma zilizotolewa Bungeni na mbunge wa Wawi (CUF) Ahmed Ngwali mnamo Mei 11 kwamba serikali imeshindwa kabisa kudhibiti uingizwaji wa bidhaa feki. Mbunge huyo akenda mbali zaidi kwa kuvituhumu vyombo vya usalama kuhusika na uovu huo kwani bila ya wao uingizwaji huo usingewezekana.

Maoni :

Uingizwaji wa bidhaa bandia nchini Tanzania na kwingineko ni tatizo  lililokosa suluhisho la uhakika maadamu mfumo wa ubepari ndio unaotabikishwa/ kutekelezwa.

Hii ni kwa sababu ubepari kimaumbile hujenga mazingira kwa uovu na ufisadi kushamiri. Matokeo ya kushangaza kutoka kwa utafiti uliofanywa na Shirikisho la Viwanda nchini Tanzania mwaka 2016 umeonesha kwamba asilimia khamsini (50%) ya bidhaa zote zinazoingizwa nchini ni feki.

Matokeo haya ambayo ni fedheha kubwa yamepatikana kwa kuwahoji walaji 250 nchini kote na wazalishaji 47 kisha kujumuisha takwimu kutoka kwao na kutoka kwa wahusika wengine. Bidhaa feki huwa ni pamoja na madawa ya binadamu, vyakula, vifaa vya ujenzi na vitendea kazi vingine. Imetajwa kwamba bidhaa hizi huingia kipitia viwanja vya ndege na mipakani.

Bidhaa feki na bandia ni tatizo la kiulimwengu linaloathiri makampuni, viwanda na walaji. Hili ni mojawapo ya majanga miongoni mwa majanga lukuki ya mfumo huu wa kibepari/kidemokrasia unaoangamiza na ambao msingi na kipimo chake ni ‘maslahi’ ukipuuza kila kitu mpaka hata kama kina madhara. Maadamu watu wataendelea kutawaliwa na mfumo uliobuniwa na wanadamu, kuendeshwa kwa matamanio bila ya fikra ya kumwogopa Allah (swt), kamwe mfumo huo hauwezi kuzalisha watu wenye kuwajibika, wakweli na waadilifu.

Uislamu utakapotabikishwa na Khilafah utamaliza kabisa mara moja tatizo la bidhaa za ghushi, feki na bandia.

Imeandikwa na Ramadhani Said Njera

Mjumbe wa Afisi ya Habari

Hizb ut Tahrir Tanzania

Kwa ajili ya Afisi kuu ya Hizb ut Tahrir

2 Comments
  1. Davidson says

    Amazing issues here. I’m very glad to see your post.
    Thank you a lot and I am looking forward to contact you.
    Will you please drop me a mail?

  2. Hokicoy login says

    I have been exploring for a little bit for any high-quality articles or weblog posts on this kind of space .
    Exploring in Yahoo I ultimately stumbled upon this web site.
    Reading this information So i am happy to express
    that I have a very excellent uncanny feeling I discovered just what I needed.
    I such a lot undoubtedly will make certain to don?t overlook this web site and give it a glance regularly.

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.