Tuzo Ya Nobeli Kwa Gurnah Sio Fakhari Kwa Tanzania Wala Uingereza
بسم الله الرحمن الرحيم
Tuzo ya Nobeli ya Amani kwa Uandishi (Nobel Peace Prize for Literature) kwa msomi Abdulrazak Gurnah, mwenye asili ya Zanzibar sio kitu cha kujifakhiri Tanzania wala Uingereza bali ni fedheha kwao kamwe!
Uingereza ndio iliyoleta siasa za chuki na ubaguzi Zanzibar, zikapigiwa debe na Nyerere na kufanyiwa kazi kibubusa na chama kilichoundwa na Uingereza cha Afro Shirazi Party.
Siasa hizo za kijinga za ‘ugozigozi’ zimepelekea kukimbia kwa wasomi, watu wenye upeo na uwezo mkubwa wakiwemo masheikh kama Al- Marhum Sheikh Abdullah Farsy (Allah SWT Amrehemu). Hao ilibidi waondoke kwa kuwa hawakuwa na namna ila kukimbilia ughaibuni.
Siasa hizo za ubaguzi, uwe wa kieneo, kidini, kikabila nk. bado zinaendelezwa, na mfano hai ni kuendelea kushikiliwa kwa chuki mamia ya mahabusu Waislamu kwa kisingizio cha kutokamilika ushahidi.
Tuzo hii kwa msomi Abdulrazak Gurnah, ambaye alikimbizwa na siasa hizo isikumbatiwe kama fakhari, bali ni guo la fedheha linalopaswa kuleta tafakuri mpya na kubadilisha mwelekeo wetu.
12 Oktoba 2021
Masoud Msellem
Maoni hayajaruhusiwa.