Tukio La Septemba 11 Na Uwongo Wa Vita Vya Ugaidi
بسم الله الرحمن الرحيم
arehe kama leo 11/09 2001 ndio siku iliyotokea kinachodaiwa shambulizi la kigaidi la kupigwa majengo mawili (twin towers) ya Kituo cha Biashara (WTO) mjini NewYork- Marekani. Mashambulizi hayo ndio yakafanywa kuwa kisingizio cha uvamizi wa nchi mbali mbali za Waislamu, kumwaga damu zao, kupora rasilmali zao na kuzichukua baadhi ya nchi hizo.
Aidha, tukio hilo likapelekea nchi za magharibi hususan Marekani kuzitenza nguvu nchi changa zikiwemo za Afrika Mashariki kupitisha sheria na kushiriki katika mapambano ya kikatili na kinyama bila hata kujali sheria zao ati kupambana na ugaidi ambapo walengwa wake ni jamii moja ya Waislamu tu.
Pia mapambano haya ya ugaidi yameathiri wengi katika kutekwa, kuteswa, kupotezwa hadi kuuwawa bila hata ya kufuatwa taratibu za ukamataji au wa kimahakama.
Kimsingi, mapambano ya ugaidi yameziingiza nchi changa ikiwemo Tanzania katika mahusiano mabaya na kundi moja la raia wake wengi (Waislamu), yamechochoea ubaguzi, kwa kuwa Waislamu wanahisi kuonewa wazi wazi na wengine wasiokuwa wao kupendelewa, nchi kuingiliwa katika maamuzi na miundombinu yake hususan ya kiusalama kwa kuwa madola makubwa ndio hupanga na kupangua kuhusiana na vita hii, bila ya kujali mamlaka na uhuru wa nchi husika.
Tamko ‘ugaidi’ au ‘irhab’: maana yake ni kutia khofu, au kuogopesha.
Tamko hilo asili halikuwa na maana ya kiistilahi, ambalo kwa lugha ya kiarabu ni: Arhaba, yurhibu, irhaabu.
Kama Alivyolitaja Allah SWT:
تُرْهِبُونَ بِهِ عَدُوَّ اللَّهِ وَعَدُوَّكُمْ
‘ili kuwatia khofu maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu’
(Surah Al-Anfal, Ayah 60)
Kwahiyo, maana hasa ya ugaidi ni kitendo cha kutia khofu au kuogopesha, huo ni upande wa kilugha, na ndio maana yake katika thaqafa ya Kiislamu, ni kilugha tu na si vinginevyo.
KUIBUKA MAANA YA UGAIDI KIISTILAHI NA UDHAIFU WAKE
Maana hii ya kiistilahi haikutokana na thaqafa ya Kiislamu na iliibuka mwanzoni mwa karne ya 20 kutoka kwa wamagharibi. Ilipata hasa mwelekeo mpya katika Mkutano wa Paris 1979, Idara ya Kijasusi ya Marekani na Uingereza wakatafsiri hivi:
“Ni vitendo vya matumizi ya nguvu dhidi ya raia kwa malengo ya kisiasa” matumizi ya nguvu ikiwemo *kuuwa, uharibu mali, kuharibu miundombinu”.
Hadi sasa hakuna maana moja iliyokubaliwa na mataifa yote ulimwenguni juu ya nini hasa ugaidi, na ni kitendo gani ni ugaidi au akitenda nani ni ugaidi.
Hii humaanisha udhaifu wa agenda hii, na kuwa ina lengo ovu na la hatari nyuma yake. Kila taifa au kundi la kimataifa lina mtazamo wake wa nini ugaidi kwa mujibu wa maslahi yake. Kwa mfano:
Marekani alipouliwa Indira Gandhi (1984) ilisema ni kitendo cha kigaidi kwa maslahi yake,lakini kuuwawa kwa mfalme Faisal wa Saudia (1975) Marekani ilikataa kuwa ni kitendo cha kigaidi, kwa kuwa aliofanya hivyo ni mpwa wake ili Mfalme Fahad ashike madaraka
Hivyo hivyo, kuuwawa kwa Rais John Kenedy wa Marekani (1963) Marekani haikusema ni ugaidi, bali ilikiita tu ni kitendo cha jinai.
Aidha, Marekani awali iliuelezea ulipuaji wa Jumba la Idara ya Upelelezi la FBI katika jimbo la Oklahoma (19 Aprili 1995) kuwa ni kitendo cha kigaidi lakini ilipojitokeza wazi kuwa wahusika ni wanajeshi wa Marekani wakabadili mtazamo wao kutoka ugaidi mpaka kuwa tendo hafifu la jinai. (Kitabu cha Fikra Hatari za Kuharibu Uislamu- Hizb ut Tahrir )
Kwa kifupi, kwa upande mwingine kila harakati inayopinga/kwenda kinyume na maslahi ya Marekani na vibaraka wake inachukuliwa ni harakati ya kigaidi na inaingizwa katika orodha ya harakati za kigaidi.
Orodha hiyo inayotolewa na serikali ya Marekani kila mara inahusisha harakati nyingi za Kiislamu zilizomo ndani ya nchi za Waislamu kama Misri, Pakistan, Palestine, Algeria nk.
Kutoka mwaka 1979 Marekani imelazimisha mikutano kadhaa ya mataifa kujaribu kukubaliana juu ya nini ugaidi na hatua za kuchukua dhidi ya ugaidi.
SURA OVU YA UGAIDI YAFICHUKA
Baada ya uripuaji wa Septemba 2001 Marekani na washirika wake wa magharibi walidhihirisha wazi ajenda nyuma ya ugaidi kuwa ni *Vita dhidi ya Uislamu na Waislamu*
*Raisi Bush alisema wazi :
“imma uwe na magaidi (Waislamu) au uwe na sis i(wamagharibi)’, yaani imma uwe Muislamu au kafiri.
Marekani ilihalalisha uvamizi wake dhidi ya Afghanistan,Iraq, Syria nk. kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi/magaidi.
Sasa tarumbeta la ugaidi limechukua majukwaa yote ya kimataifa na nchi zote ulimwenguni zinalazimishwa kukubali wimbo huu na kuucheza
وَلاَ يَزَالُونَ يُقَاتِلُونَكُمْ حَتَّى يَرُدُّوكُمْ عَنْ دِينِكُمْ إِنْ اسْتَطَاعُوا
“Wala hawatoacha kupigana nanyi mpaka wakutoeni katika Dini yenu kama wakiweza. (Surah Al-Baqarah, Ayah 217)
Nchi za Afrika Mashariki nazo zikapokea na kuweka sheria dhidi ya ugaidi, mfano Tanzania, sheria ya kuzuiya na kupambana na ugaidi ikapitishwa mwaka 2002.
MAREKANI NDIO GAIDI NAMBARI MOJA
Hata hivyo, ukweli ulio wazi Marekani ndio gaidi namba moja ulimwenguni.
Raisi Donald Trump ndani ya mwaka 2016 aliweka wazi hili kwa kusema:
*” Marekani imeeneza vurugu Mashariki ya Kati yote, na lilikua kosa kubwa*”
* Pia Trump alisema: “Obama na Hillary Clinton ndio walioasisi kundi la Isis*”
Kauli hizo zadhihirisha wazi kuwa Marekani ndie gaidi mkubwa na ajenda yake chafu, ovu, ya kidhalimu dhidi ya nchi za Waislamu na nchi change (kama za Afrika) ili kupora rasilmali zao na kuingilia katika katika taasisi zao za kiusalama.
Marekani huunda makundi ya kiharamia na kigaidi ulimwenguni kote au kupandikiza chuki baina ya watu hasa katika nchi changa na kulazimisha uvamizi wake ndani ya nchi husika kwa kisingizio cha kuleta amani.
Lakini kumbe ni kuuwa Waislamu na watu jumla na kupora rasilimali. Au Marekani hutumia sheria ya kuzuiya na kupambana na ugaidi ulimwenguni hasa nchi changa kama Tanzania ili kuwadhalilisha Waislamu, kuwatesa, kuwaweka mahabusu muda mrefu, na hata kuwapoteza kwa kuwaua.
Mfano, Tanzania kuna Waislamu wengi kama ilivyoelezwa kwa kirefu katika kitabu cha Sheikh Ponda ambao tayari wamepotezwa. Bali kuna Waislamu walioteswa, walioteseka kwa kusekwa korokoroni kwa muda mrefu kama vile Uamsho na wanachama watatu wa 𝐇𝐢𝐳𝐛 𝐮𝐭 𝐓𝐚𝐡𝐫𝐢𝐫 𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚(ambao Alhamdullilah! wameshaachiwa huru ) na Waislamu wengine bado wapo ndani wanateseka katika mikoa mbali mbali kama Mtwara,Tanga, Arusha nk.
Watuhumiwa hao wanadhalilishwa na kuteswa na familia zao na wakati mwengine mwingi taratibu zote za kusimamia haki huwekwa pembeni. Yote hayo ni kwa sababu ya sheria hii.
وَدَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَوۡ تَغۡفُلُونَ عَنۡ أَسۡلِحَتِكُمۡ وَأَمۡتِعَتِكُمۡ فَيَمِيلُونَ عَلَيۡكُم مَّيۡلَةٗ وَٰحِدَةٗۚ
“Wanataka walio kufuru mghafilike na silaha zenu na vifaa vyenu ili wakuvamieni mvamio wa mara moja” (Surah An-Nisa’, Ayah 102)
MWISHO
Kwa kumalizia, sheria ya ugaidi na mapambano yake ni zao la chuki na uroho wa rasilmali wa nchi za magharibi hususan Marekani.
Hayo yameambatana na ukandamizaji,dhalimu na ajenda ya kibeberu.
Ni wajibu wanadamu na wapenda haki kupaza sauti kupinga dhulma na maonevu kwa kisingizio cha mapambano dhidi ya ugaidi.
Amma Ummah wa Kiislamu licha ya kupaza sauti zao pia wana wajibu wa kidini wa kufanya kazi ya ulinganizi ili kurejesha tena dola ya Khilafah Rashidah inayopaswa kuanzia katika nchi kubwa za Waislamu na kuenea kila mahala ili kwa dola hiyo kuweza kuulinda Ummah wa Kiislamu na ubinadamu kwa jumla.
Risala ya Wiki No. 192
08 Rabi’ al-awwal 1446 Hijri | 11 Septemba 2024 Miladi
Maoni hayajaruhusiwa.