Tareh 3 March, Siku Ya Msiba Mzito Kwa Kuangushwa Dola Ya Kiislam

13

Dola ya Kiislamu ya Khilafah iliyokuwa muendelezo wa Dola aliyoiasisi Mtume SAAW iliangushwa rasmi tarehe 03/03/1924 Miladia   sawa na 27 Rajab1342 Hijiria. Dola ambayo ilidiriki kuzishinda tawala za Uajemi na Warumi (Byzantine) na kubakia kuwa dola kuu mpaka karne ya 18. Makafiri waliweza kuiangusha kufuatia kudhoofika kifikra, kuzongwa na maadui wa ndani na nje pia kampeni kabambe ya madola ya kibepari ndani ya Ulaya na Marekani. Khilafah ilikuwa ikisimamia hukmu za Kiislamu, kuwaunganisha Waislamu, kufunguwa miji nk.

Mara baada ya kuangushwa dola hiyo kulifuatiwa na hali isiyosita ya udhalilifu, majanga na maafa yasiyomithilika kwa Ummah wa Kiislamu kwa kuvamiwa, kuteswa, kuuwawa, kuchukuliwa ardhi zao, kusambaratishwa uhai wa umoja wake, kugawanywa kimadhehebu na kitaifataifa kiasi cha kukosa sauti moja  yenye athari katika anga za kimataifa nk.

Majanga yote leo yanayotusibu kitaifa, kieneo na kimataifa ni matokeo ya kukosa kinga (dola) ya kuwanusuru Waislamu na kudhamini maisha, heshima na usalama wao.

Tunashuhudia kwa macho mawili uvamizi wa makafiri katika miji yetu kama Iraq, Afghanistan, Syria, Yemen, Somalia nk. Aidha, kumeshamiri dhulma kama mateso na ubaguzi wa kidini kama ndani ya Afrika ya Kati, Burma, China, Marekani, Urusi nk. Vita vya kikatili na kidhulma dhidi ya Uislamu na Waislamu kwa jina la ugaidi ni matokeo ya kuanguka dola hiyo. Bila ya kutaja matendo ya kurundikwa Waislamu majela wakipata mateso ambayo hata mnyama hathubutu kumtendea mnyama mwenzake chini ya mikono ya mataifa ya kibepari kama Marekani, Uingereza na hata kutoka kwa watawala wa nchi changa duniani kote ikiwemo maeneo yetu.  Leo suala la kukashifiwa na kukebehiwa dini kuanzia sheria zake kama hijabu, Quran, kumtukana Mbora wa Darja Mtume SAAW yamekuwa ni mambo ya kawaida kila mahala mara baada ya kuangushwa dola ya Kiislamu ya Khilafah iliyokuwa kinga kwa makarne.

Kuvunjwa Khilafah ni mpango kabambe wa nchi za kikafiri za ki-Magharibi kwa ajili ya kuendeleza sera zao za kigeni, kuuvuruga mfumo wa Kiislamu, kunyakuwa rasilmali zake na kumakinisha mfumo wao batil wa kibepari.

Kufikia malengo hayo walitumia mikakati mbalimbali ikiwemo vibaraka kama Sharrif Hussein, Kamal Atarturk, Ibn Saud nk. Pia kuunga mkono harakati za kujitenga kwa maeneo yaliokuwa chini ya Khilafah kwa guo la ‘uhuru’ ili kuimega mamlaka ya Khilafah. Itakumbukwa pia Uingereza, Ufaransa na Urusi zilikubaliana mkataba wa siri wa Sykes-Picot Agreement ili kugawana ngawira ardhi za dola ya Khilafah.

Katika Vita Vikuu vya Kwanza malengo ya kuivunja Khilafaha yalikwenda kwa haraka zaidi. Nchi washirika baada ya kushinda zilinyakua maeneo muhimu ya Khilafah. Chini ya uongozi wa Uingereza zilimlazimisha Khalifah, kiongozi wa dola ya Kiislamu kusaini mkataba hapo tarehe 30 Oktoba 1918 ulioitwa wa amani ukiwa na lengo la kuipunguza nguvu dola hiyo.

Uingereza kwa kushirikiana na kibaraka wake Yahudi muovu na msaliti Mustafa Kamal aliyekuwa Kamanda wa kijeshi wa Uturuki walianzisha uasi dhidi ya Khilafah. Mnamo tarehe 1 Machi 1924 Mustafa Kamal alitoa agizo bungeni la kuvunjwa Khilafah, na asubuhi ya tarehe 3 Machi 1924 ilitangazwa rasmi kuvunjwa dola hiyo na kutenganishwa dini mbali na serikali.

Mkataba wa Lausanne (Lausanne Treaty) ukasainiwa tarehe 24 Julai 1924 ukifuatiwa na kutambuliwa rasmi uhuru wa Uturuki. Uingereza ilitoa zawadi kwa makubaliano na Mustafa Kamal kujiondoa katika maeneo yote iliyoyakalia ya Uturuki na kuutambua rasmi uhuru wa dola hiyo.

Mmoja wa wabunge ndani ya Bunge la Uingereza alipinga hatua ya nchi yake kutambua uhuru wa Uturuki. Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Lord Curzon alifafanua na kumliwaza mbunge huyo kwa kumjibu bungeni :

     “Suala ni kwamba Uturuki imeshabomolewa na haitokuja juu tena, kwa kuwa tumevunja nguvu yake ya kiroho: Khilafah na Uislamu.”

Enyi Waislamu,

Hivi ndivyo dola yenu Tukufu ya Khilafah ilivyoangushwa, na majanga ya kuangushwa kwake yapo mbele ya macho yenu waziwazi kitaifa na kimataifa. Kumbukeni Khilafah hata katika zama za kudorora na ikiwa ukingoni mwake bado iliwajali na kuwahurumia Waislamu kiasi cha kutuma kikosi maalumu Afrika Mashariki chini ya Kamanda Ali Bey kusaidia kuwakomboa Waislamu na wakaazi jumla wa maeneo haya na dhulma  na ukatili wa Wareno.

Aidha, chini ya Khilafah makafiri walisafiri kwenda kusoma katika vyuo vyake vikuu, wayahudi na wengineo wakiomba hifadhi kukimbia mateso  ya wakatoliki na ubaguzi uliokita ndani ya Ulaya, bila ya kutaja namna wakristo wa Syria na Jerusalem walivyopigana bega kwa bega upande wa jeshi la Khilafah kuwatimua makruseda/maswalibiyina (wakiristo wenzao) kutokana na insafu, wema, uadilifu  wa dola ya Khilafah.

Hivyo, sisi Waislamu tuna wajibu mkubwa na dhima kubwa mbele ya Mola wetu kushiriki katika mchakato wa kuirejesha tena dola hiyo ya kilimwengu kwa kutumia njia ya Mtume SAAW ya mivutano ya kifikra na kisiasa bila ya kuhusisha nguvu wala mabavu, ili dola hiyo ianzie katika nchi kubwa ya Kiislamu kisha kuziunganisha na kuzikomboa ardhi zote za Waislamu na ulimwengu mzima.

Tubebeni jukumu hili kwa ikhlasi kuikimbilia bishara ya Mtume SAAW ya kurejea tena kwa dola hiyo yenye nuru na neema.

..ﺜﻢﺘﻌﻭﺩﺧﻼﻓﺔﻋﻟﻰﻤﻨﻬﺎﺝﺍﻟﻨﺑﻭﺓ

….’.Kisha itarudi tena Khilafah kwa njia (manhaj) ya Utume

03 Machi 2017 Miladi / 3 Jumada al-thani 1438Hijri

https://www.facebook.com/HtTanzaniaa/

13 Comments
  1. Hao says

    I’m really enjoying the design and layout of your blog. It’s a very easy on the eyes which makes it much more enjoyable for me to come here and visit more often.
    Did you hire out a designer to create your theme? Superb work!

  2. Asiyejulikana says

    This post is truly a good one it assists new internet viewers, who are wishing for blogging.

  3. Rhys says

    I don’t know whether it’s just me or if everybody else experiencing issues
    with your website. It looks like some of the written text on your content are running off the screen. Can someone else please provide feedback and
    let me know if this is happening to them too? This could be a problem with my web browser because I’ve had this happen before.
    Cheers

  4. Elmo says

    It’s amazing designed for me to have a web page, which is useful in favor of my experience.
    thanks admin

  5. 우리카지노추천 says

    Plus, with cryptocurrency accepted and generous bonuses obtainable, mBiit Casino is the excellent
    destination for your gamkng pleasure.

    Check out my web blog 우리카지노추천

  6. 카지노사이트추천 says

    Each and every bet you make should be much less than $10 of yopur starting stack.

    My homepage 카지노사이트추천

  7. Tamika says

    At this time I am going to do my breakfast, once having my breakfast coming over again to read more news.

  8. Carin says

    Hey there! This is my 1st comment here so I just wanted
    to give a quick shout out and tell you I genuinely enjoy reading your
    blog posts. Can you recommend any other blogs/websites/forums
    that deal with the same subjects? Thanks!

  9. Asiyejulikana says

    Somebody necessarily assist to make significantly articles I’d state.
    That is the very first time I frequented your website page and thus
    far? I amazed with the analysis you made to create this particular put up incredible.

    Fantastic job!

  10. Asiyejulikana says

    Hello, this weekend is good for me, as this
    occasion i am reading this impressive informative
    piece of writing here at my home.

  11. Asiyejulikana says

    I’m extremely inspired together with your writing talents
    and also with the format in your weblog. Is that this
    a paid subject matter or did you modify it your self? Either way stay up
    the excellent high quality writing, it’s uncommon to see a nice weblog like this one today..

  12. viagra says

    Since it’s difficult to be precise, many online glasses retailers have made taking a
    PD measurement even simpler, offering tools within their browser and mobile apps to take these measurements, typically based on webcam or phone
    camera photos.

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.