Tangazo La Mijadala Ya Wazi
Tangazo La Mijadala Ya Wazi Kwenye Mitandao Ya Kijamii
Wadau Wote Wa Fikra Za Dini Mseto (Interfaith Dialogue), Dini Za Kiafrika, Imani Za Mizimu, Upagani Nk.
Harakati ya Hizb ut Tahrir Tanzania inatangaza kutaka mijadala ya wazi kwa yeyote na kundi lolote katika wadau wanaoshikilia fikra za Mazungumzo baina ya dini tatu – Dini Mseto (Interfaith Dialogue), Dini za Kiafrika, Upagani, Imani za mizimu n.k.
Mijadala hiyo iwe kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii ya hao wadau au ya kwetu.
Mijadala hiyo itakua kwa hoja za kiakili na kidini na itaendeshwa kwa murua na ustaarabu wa mijadala ya wenye akili na maarifa.
Kwa wale wote wenye nia au kuwa tayari kushiriki katika mijadala hii nasisi Hizb Ut Tahrir, wawasiliane nasi kupitia mitandao yetu ya kijamii au kupitia wawakilishi wetu wa Afisi yetu ya Habari au Afisi yetu ya Mahusiano ya Umma ili kuratibu jambo hilo kwa ufanisi.
Ni matumaini yetu kwa wadau, waumini na wanaounga mkono fikra hizo, hususan wanaozipigia chapuo katika mitandao ya kijamii na penginepo watatumia fursa hii adhimu ya kushiriki mijadala ya aina hii.
Masoud Msellem
(Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari)
0778 87 0609
Sheikh Mussa Kileo
(Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya Umma)
0684 393 995
Maoni hayajaruhusiwa.