Tangazo la Majibu ya Kuonekana kwa Mwezi Mpya wa Baraka wa Ramadhani ya Mwaka 1440 Hijria
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
(Imetafsiriwa)
شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِيَ أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ وَمَن كَانَ مَرِيضاً أَوْ عَلَى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ يُرِيدُ اللّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلاَ يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُواْ الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُواْ اللّهَ عَلَى مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ
“Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’an kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi atakaye uona (mwezi mpya) naafunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini basi atimize hisabu katika siku nyengine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru.”
[Al-Baqara: 185]
Sifa zote ni kwa Mwenyezi Mungu na amani na salama zimwendee Mtume wa Mwenyezi Mungu, familia yake, maswahaba zake, washirika wake na wale wote wanaomfuata katika njia yake ya kurudisha Itikadi ya Kiislamu kuwa ndiyo msingi wa fikra na Hukm Shari’ah zao ndiyo kipimo cha vitendo vyao na vyanzo vya kuhukumiana.
Al-Bukhari amevua kutoka katika Sahih yake kutoka kwa Muhammad Bin Ziyad kwamba alisema; Nilimsikia Abu Hurairah (ra) akisema, “Mtume amani iwe juu yake na familia yake, alisema au alisema, Abu Al Qasim (saw) alisema:
«صوموا لِرُؤيتِهِ وأَفْطِرُوا لرؤيتِهِ فإنْ غُـبِّيَ عليكم فأَكْمِلُوا عِدَّةَ شعبانَ ثلاثين» “Anza kufunga kwa kuuona mwezi wa Ramadhani na fungua kwa kuuona mwezi wa Shawwal na lau mbingu itakuwa haing’ari (hauku uona mwezi) kamilisha siku thelathini za Shaaban.”
Baada ya kufanya uchunguzi juu ya mwezi mpya wa Ramadhani baada ya kuchwa kwa jua siku ya Jumapili, kuamkia Jumatatu, tunadhibitisha kuonekana kwa mwezi mpya kwa mujibu wa vigezo vya Shari’ah. Hivyo basi, kesho, Jumatatu ni siku ya kwanza ya mwezi wa baraka wa Ramadhani…
Mwezi huu wenye Baraka unakuja wakati ambapo tunashuhudia ukali wa mizozo kati ya Ummah na magenge ya watawala ambao wako makini kuwatumikia mabwana zao, wakoloni Makafiri Wamagharibi. Wanafanya kila wawezalo ndani ya Algeria na Sudan kuhakikisha kuwa tunaendelea kuwategemea Wamagharibi na kuweka vikwazo ili Ummah usirudi kuwa Ummah mmoja chini ya kivuli cha Shari’ah ya Muumba ambaye ameagiza uungane na ushikamane na neno la Tawheed na ukatae miito ya Sykes-Picot ambayo ina gawanya safu za Waislamu… Ilhali wafuasi wa Wamagharibi katika wanajeshi na wanasiasa kufikia sasa wamefaulu kupeleka kombo wimbi la mageuzi la Bara Arabu ndani ya Misri na Tunisia na kwengineko, sisi katika Hizb ut Tahrir tunaulingania Ummah wa Kiislamu wote kuchukua msimamo mkubwa unaomridhisha Mwenyezi Mungu wao, na kuondosha madhambi, na dhambi kubwa la Ummah na njama ovu dhidi yake, msimamo ambao unaondosha laana kutoka kwake na kurudisha fahari ndani ya ardhi zake.
Tayari tumesema kwa kurudia kuwa ushindi ni kwa “kuangushwa tawala zilizopo” na kusimamishwa kwa utawala mbadala ambao unamridhisha Mwenyezi Mungu au kinyume chake haingii akilini kuwa na nusu ya mapinduzi au mapinduzi yanayoishia pale yalipo anzia kwa kuweka viraka utawala uliokuwepo na kubadilisha sura mpya za magenge yaliyo kuwepo baada ya kuongeza mabadiliko ya kirongo. Tunawalingania Waislamu kuunganisha mikono yao iliyo twahirishwa kwa udhu kwa mikono ya Hizb ut Tahrir ambao wamo ndani ya mvutano wa kifikra na wakisiasa, wakifichua mipango ya kijanja ya Wamagharibi, na kuwaonyesha ukweli wa njia ya Uislamu. Labda Mwenyezi Mungu atatoa ushindi na nguvu kupitia mikono yenu kwa kusimamisha Khilafah na si jengine lolote. Na labda Mwenyezi Mungu atatoa ushindi kwa mikono ya Amiri wa Hizb ut Tahrir mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, ushindi mkubwa nanyi mumpe ahadi ya utiifu kama Khalifah atawale juu yenu kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ya Mtume (saw) nanyi muishi chini ya Khilafah kwa Shari’ah ya kweli ya Mwenyezi Mungu na muubebe ulinganizi wa Uislamu, tochi ya muongozo kwa wanadamu.
Enyi Maafisaa wa Majeshi jueni kwamba Mwenyezi Mungu ataipa Dini Yake ushindi, ikiwa si kwa mikono yenu basi kwa mikono ya wanaume wengine mukhlisina ambao Yeye (swt) amewapa daraja kwa ushindi wa Dini yake. Hivyo basi msipoteze nafasi hii adhimu na unganeni na Ummah ili mpate radhi za Mwenyezi Mungu na mazuri ya duniani na akhera.
Pia nina furaha kuwatumia salamu zangu na zile za Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na wale wote wanaofanya kazi ndani yake kwenda kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah na kwa Waislamu wote kutokana na mwezi huu wa baraka. Twamuomba Mwenyezi Mungu atuepushe na Moto ndani ya mwezi huu wa rehema na msamaha na tunamuomba Yeye (swt) aturuhusu tuishuhudie Laylatul Qadr na atubariki kwa malipo yake…
Ewe Mwenyezi Mungu, Bwana wa Mbingu na Ardhi, tupe izza kwa kupeana ahadi ya utiifu kwa Khalifah wa Waislamu ndani ya Khilafah ya pili iliyoongoka kwa njia ya Utume hivi karibuni na isiwe baadaye… Allahuma ameen ameen ameen.
Wassalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh
Kuamkia Jumatatu, tarehe 1 ya mwezi wa baraka wa Ramadhani ya mwaka 1440 H
Salah Eddine Adada
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
H. 29 Sha’aban 1440 | Na: 1440 H / 031 |
M. Jumapili, 05 Mei 2019 |
Maoni hayajaruhusiwa.