Pole na Karibu Tena Ndugu Yetu Mohammed Dewji

Karibu tena ndugu yetu Mohammed Dewji ( MO) katika maisha ya kawaida baada ya kutekwa kwa siku nane.

Tunakupa pole kwa mtikisiko mkubwa uliokutikisa wewe, familia yako, ndugu zako wa damu, Waislamu wenzako na kila mpenda haki, utu na uadilifu.

Hata hivyo, kubwa zaidi na muhimu ni kuwa upo hai na salama. hatuna budi kusema Alhamdullilah !

Ni kipindi kifupi cha mwezi mmoja tu ndani ya mwezi uliopita wa Muharram kulikuwa na maadhimisho ya tukio la kikatili na huzuni lililomsibu Imamu Hussein ra.

Nataraji tafakur nzito ya tukio lile na tukio hili itaibua mwanga mpya nafsini mwako na wengine.

Karibu tena ndugu yetu huku ukiizingatia kauli ya Imamu Ali ra. isemayo:

‘Mwerevu (wa kweli) ni yule ambae leo yake (huifanya bora ) kuliko jana yake”

20 Oktoba 2018

Masoud Msellem

Maoni hayajaruhusiwa.