Omar Salum Bumbo: Aachiwe Huru, Apewe Dhamana Au Kesi Yake Isikilizwe Mara Moja

بسم الله الرحمن الرحيم

Jina: Omar Salum Bumbo
Miaka : 52
Kazi: Fundi mjenzi
Makaazi : Tandika Relini, Dar es Salaam
Mahala anaposhikiliwa : Gereza la Lilungu, Mtwara
Muda wa kuwa mahabusu : Karibu miaka 4 sasa
Alinyakuliwa tarehe 27/10/2017 na kutekwa na wanaoaminika kuwa ni maafisa wa usalama, baada ya mmoja wa maafisa hao kwa ujanja kumpigia simu kwamba angetaka kumpatia kazi ya ujenzi, kisha Omar Bumbo alipofika eneo aliloahidiwa kukutana na mteja huko Tabata alitekwa na wanaoaminika kuwa maafisa usalama, kumsweka garini, kutoweka nae kusikojuulikana, sambamba na kumtisha dereva wake wa bodaboda aliyemfikisha Omar Bumbo eneo hilo, kuondoka mara moja.
Baada ya Omar Bumbo kutoweka, na familia kufuatilia katika vituo mbali mbali vya Pilisi kwa karibu mwezi, hatimae Omar Bumbo akapelekwa Mtwara na kubambikizwa kesi ya ugaidi: PI NO. 9 OF 2017 na mnamo tarehe 5/12/2017 kimya kimya akaanza kupelekwa Mahkama ya Wilaya ya Mtwara kwa ajili ya kutajwa kesi yake.
Kwa sasa ni karibu miaka 4, bado yupo kizuizini katika Gereza la Lilungu, Mtwara huku kesi yake ikikosa ushahidi, hakuwa akiletwa mahkamani kwa mwaka mzima na miezi kadhaa mpaka hivi karibuni tarehe 20 Mei 2021ndio kesi yake imeanza kutajwa tena.
Mpaka sasa anaendelea kunyimwa haki zake msingi ikiwemo Magereza kuzuiya kupelekewa chakula, kutembelewa na familia nk.
Tunavitaka vyombo vya kusimamia haki Omar Salum Bumbo aachiwe huru, apewe dhamana au kesi yake isikilizwe mara moja

Maoni hayajaruhusiwa.