Mwezi Wa Januari – Kuangushwa Ngome Ya Mwisho Ya Kiislamu Ndani Ya Hispania

Ndani ya Januari mwaka 1492, miaka zaidi ya 500 iliyopita Ummah wa Kiislamu ulikumbwa na msiba wa tukio la kuangushwa kwa ngome ya mwisho ya utawala wa Kiislamu katika visiwa vya Grenada. Kuanguka huko ndiko kukawa mwisho wa utawala wa Kiislamu katika ardhi ya Andalucia/ Hispania.

Uislamu ndani ya ardhi ya Hispania uliingia mwaka 711 milladiya, pale Jemadari Tariq ibn Ziyyad alipovuka bahari akiwa na kundi la mujahidina kuifungua/ fathi rasi ya Iberia. Fathi ya eneo hilo ilikuwa baada ya raia wa eneo hilo ambalo kwa sasa linajumuisha ardhi ya Hispania na Ureno kumuomba Khalifa wa Waislamu awakomboe kutoka kwenye utawala dhalimu chini ya mfalme Roderick

Utawala wa Kiislamu katika ardhi ya Hispania ulipeleka nuru na maendeleo nchi hiyo na kwa Ulaya nzima. Vyuo vya fani mbalimbali vilijengwa katika ardhi hiyo na kuifanya ardhi ya Andalusia kushamiri. Wageni wengi wasiokuwa Waislamu walifurika katika nchi hiyo kwa lengo la kupata maarifa, fani na elimu mbalimbali. Aina mbali mbali za uvumbuzi wa kisayansi ulifanyika na kupatikana vituo vingi vya kisayansi.

Utawala wa Kiislamu ndani ya Andalausia ulileta utulivu na amani kwenye eneo ambalo awali lilikuwa limesheheni mauaji na dhulma miongoni mwa wakaazi wake.
Serikali ya Kiislamu ilikuja kukomesha tabia ya watu wa Ulaya ya kuuwana kutokana na kutofautiana madhehebu yao katika imani yao ya kikristo. Aidha, dola ya Kiislamu ilikuja kuwakomboa mayahudi ambao awali wakiteswa na kudhulumiwa na kanisa kiasi cha kuwafanya kuishi katika hali ngumu sana kabla ya utawala huo.

Historia ya ndani ya ardhi ya Andalusia ni muhimu kwa Waislamu. Lakini muhimu zaidi ni kufanya kazi ya ulinganizi wa Uislamu  ili inshaAlaah ardhi hiyo, siku moja irudi chini ya dola ya Kiislamu ya Khilafah ya Pili.

#UislamuNdioUfumbuziSahihi

Na Kaema Juma

Maoni hayajaruhusiwa.