Kujiuzulu Kwa Spika Wa Bunge La Tanzania Inaonesha Ubatili Na Kushindwa Kwa Demokrasia

بسم الله الرحمن الرحيم

Habari:

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Yustino Ndugai mnamo tarehe 06/01/2022 alijiuzulu kufuatia ukosoaji wake wa wazi kwa Raisi kuhusu mikopo na ukuaji wa deni la taifa.

Maoni:

Tarehe 28/12/2021 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ambaye ni Spika wa 7 wa tangu uhuru alitoa kauli aliyohoji juu ya mwenendo wa mikopo kutoka taasisi za fedha za kimataifa ambapo alidai kuwa Tanzania ipo katika hatari ya kupigwa mnada kutokana na kukua kwa deni la taifa.

Hivi karibuni Tanzania ilipata mkopo wa takribani dolari bilioni 3 ambapo dolari bilioni 2.29 ni kutoka Benki ya Dunia, dolari milioni 567 kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa na dolari milioni 256 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika.

Ukosoaji wa Job Ndugai ulipokelewa kwa upinzani mkubwa hususani kutoka kwa maafisa wa chama tawala(CCM) na wabunge wenzake ambao awali walimlazimisha kuomba msamaha hadharani, lakini msamaha haukukubaliwa . Siku chache baadaye, wakati Raisi Samia Suluhu Hassan akizungumza na baraza la mawaziri, wakuu wa mikoa alitoa kauli nzito dhidi ya Ndugai:

“Nataka niwambie ndicho kinachotokea, kwasababu huwezi kufikiria mtu miliyemuamini, mshika Muhimili aende akasimame aseme yale ni “stress” za 2025” alisema Rais Hassan.

Katika hali hii, Spika Ndugai hakuwa na namna ila kujiuzulu.

Kimsingi kauli ya Ndugai ilikuwa na nguvu japo ilitolewa na mtu mrongo. Kwavile inafahamika vizuri kuwa bajeri ya taifa na uidhibishaji wa mikopo unafanywa na Bunge ambalo Spika anaushawishi na angeweza kuzuia mikopo hiyo kupitia Bunge, lakini yeye pamoja na wabunge wenzake waliishinisha uamuzi wa kukopa.

Zaidi ya hapo, Spika kama mkuu wa mojawapo ya mhimili wa serikali alikuwa na nafasi  na uwezo wa kukutana na Raisi kibinafsi na kujadili kuhusu mwenendo wa mikopo.

Kwa yote haya inaonesha wazi kuwa hana tofauti na wanasiasa wenzake wa kidemokrasia ambao hujifanya kujali jamii lakini kiuhalisia wanacheza na akili za watu ili kufikia malengo yao ya kisiasa ya kibinafsi

Tukio hili linatupa picha halisi kuwa kauli ya “uhuru wa kujieleza” katika demokrasia si kweli, hutumika pale tu ambapo haiathiri maslahi ya serikali na wanasiasa. Kwahiyo madai ya kuwa ni haki ya msingi ya wananchi kujieleza, kupata na kupewa taarifa zinazohusu maisha yao ipo mbali na uhalisia wao

Kwa upande mwingine inaonesha wazi kutokuwepo kwa uhalisia wa mgawanyo wa madaraka na kujitegemea kwa mihilimli ya serikali, yaani Watendaji(Raisi), Bunge na Mahakama. Madai haya ya uhuru wa mihimili yamebakia kuwa ndoto na kukosa uhalisia tangu kuasisiwa kwake na Mfaransa Baron de Montesquieu mwaka 1748 mpaka leo hii.

Juu ya yote, demokrasia kutokana na kujengwa juu ya msingi wa maslahi binafsi, daima itasababisha kutokuelewana, vita vya madaraka, migongano baina ya watu na upinzani baina yao kutokana na watu kupigana usiku na mchana kuhodhi madaraka.

Nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania na watu wote kiujumla wanapaswa kuona ubatili na kushindwa kwa mfumo wa kisiasa wa demokrasia kutatua matatizo ya binadamu. Badala yake wanapaswa kufikiria kuhusu Uislamu ambao una mfumo wa kisiasa mbadala na bora katika kuwasimamia mambo yao na maisha yao na kuokoa wanadamu kutokamana na na matatizo yote ya kisiasa na kiuchumi.

Imeandikwa na Said Bitomwa

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Tanzania

Kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir.

Maoni hayajaruhusiwa.