Kuangazia Mitazamo Juu Ya Tukio La Vita Ya Gaza
بسم الله الرحمن الرحيم
Tangu mujahidina wa Hammas ambao wanapigana jihadi ya kujihami (difai) wawavamie Mazayuni wa Kiyahudi mnamo tarehe 7 Oktoba 2023 na kuuwa wanajeshi zaidi 1200 wa jeshi la Israel pamoja na kuwateka kadhaa miongoni mwao, kumeibuka mitazamo na misimamo kadhaa kutoka miongoni mwa Waislamu na wasikuwa Waislamu wakija m na masuluhisho kumaliza mgogoro huo.
Kundi la kwanza la Waislamu ni wale wanaotaka kusitishwa kwa mapigano na kufungua njia kupelekwa misaada ya kibinadamu, kama alipokutana Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Blinken na Waziri wa Saudia Faiswal Farhan tarehe 14 Oktoba na kufanya mazungumzo yaliyosisitiza kuwepo kwa uwezekano wa kufikisha misaada ndani ya Gaza.
Udhaifu wa Mtazamo na suluhisho hili huu ni kuwa hautatui tatizo la msingi na haufikii hitimisho lenye tija juu ya suala la Gaza na Palestina kiujumla. Kwa sababu halilengi kabisa kukomesha mauaji ya halaiki ya Wapalestina na kuondoa uvamizi wa Mazayuni katika ardhi ya Palestina ulioanza mwanzoni mwa miaka ya 1900 mara tu baada ya kukosa nguvu na kuvunjika kwa Dola ya Kiislamu ya Kiuthmani mwaka 1924 iliyokuwa mlinzi wa Palestina na biladi zote za Kiislamu
Kuna la wale wanaotaka suluhu ya uwepo wa nchi mbili, yaani nchi huru ya Israel na Palestina zinazotambulika na jumuiya ya kimataifa na Umoja wa Mataifa. Mfano mzuri katika hili ni Waziri wa Mahusiano ya Kimataifa wa Muungano wa Falme za Kiarabu (Imarati) Riim Ibrahim Al-Haashimiy katika kikao cha Baraza la Usalama cha Umoja wa Mataifa mnamo tarehe 24/10/2023 alisisitiza kuhusu suala hili
Mtazamo huu kama ulivyokuwa mtazamo wa mwanzo si mtazamo sahihi na hauna tija pia. Hii ni kwa sababu ni mtazamo unaegemea upande mmoja wa wavamizi.Kwa sababu inatoa haki ya wavamizi Mazayuni waliokwapua ardhi ya Palestina na kufanya mauaji yasiyosemekana kutambulika na kifutika maovu yao kana kwamba uvamizi wao si kitu cha kuzingatia. Huu ni mtazamo usiofaa na usiotoa haki kwa Wapalestina
Kundi lingine ni la vigeugeu, wanaojifanya kana kwamba hawana mtazamo maalumu. Hawa ni wale ambao mwanzo walikuwa wakijiliza na kutoa matamshi ya hapa na pale, huku wakijikita zaidi kwenye dua, kiasi kwamba ungeweza kuhisi wapo kidhati na watu wa Gaza. Kundi hili lilibadili mtazamo na kuanza kulaani, kukataza na kuharamisha maandamano, misaada na uungwaji mkono wowote kwa watu wa Gaza. Mfano wa watu katika kundi hili ni Imamu wa Masjid Qubaa mjini Madina Sheikh Sulaiman Alrahiil alisema “Ni haramu kupeleka msaada (Gaza) ila kwa idhini ya mtawala wa nchi yako” na Sheikh Salim Twawiil yeye akaenda mbali zaidi na kusema “Kwanza, Aqswa kwetu siyo muhimu, hakuna agizo toka kwa Mtume (SAAW) na ndio sababu hata yeye mwenyewe Mtume SAAW maisha yake yote hakuwahi kwenda Aqswa (zaidi ya siku ya Israa na Miraaj)”
Kundi hili wamesimama kidete kuwashambulia Hamas kwa kila aina ya mashambulizi. Lakini hawawagusi Mayahudi Mazayuni wavamizi ila kwa juu juu tena kama historia tu. Hawa wanataka mambo ya Palestina yasitushughulishe. Kundi hili na mtazamo wake ni hatari kwa Umma wa Kiislamu, kwani ni la Waislamu wanaofanya khiyana dhidi ya ndugu zetu wa Gaza na Palestina kwa kutumia uongo ili kukwepa majukumu ya ukombozi wa Aqswa, Gaza na Palestina kiujumla
Kundi la mwisho tutakaloliangazia kwa sasa ni kundi la wale linaolotaka majeshi ya nchi za Waislamu yaende kuwanusuru watu wa Gaza na kuwaondoa wavamizi za Kizayuni na hatimaye kuleta mwanzo mpya kwa watu wa Palestina na bara Arabu kwa ujumla. Mwanzo mpya wa kutawaliwa na sheria zinazoendana na itikadi yao na historia yao, yaani sheria za Kiislamu. Aidha, kundi hili linayataka majeshi katika ulimwengu wa Kiislamu hususan ya karibu na Palestina kama vile Misri, Jordan na Lebanon yaingie Gaza mara moja kuwatia adabu Mayahudi, kuikomboa Palestina yote na kuitwahirisha ardhi tukufu kutokana na najisi ya Mayahudi
Huu ndio mtazamo sahihi kuliko mitazamo yote. Kwa sababu nyingi ikiwemo kutoa suluhu ya uvamizi wa Mazayuni ambayo ni kuwaondoa moja kwa moja Mazayuni wavamizi katika ardhi ya Palestina. Pia unatoa uwiano wa kinguvu na kijeshi katika utatuzi wa tatizo.Katika vita hii ya Gaza, majeshi ya Israel, Marekani, Uingereza, nk. yanapigana dhidi ya kikundi kidogo cha watu cha Hammas, kimsingi inahitajika jeshi lenye weledi la kinchi kama ilivyo kwa upande wa wavamizi wanavyopata msaada wa nchi za magharibi hivyohivyo Hammas wanahitaji msaada kutoka katika nchi za Waislamu. Bila shaka iwapo hili litafanyika ni wazi ushindi kwa Waislamu na Hammas ni jambo linalotarajiwa.
Zaidi ya yote mtazamo wa kundi hili unaendana vilivyo na hukmu ya Kiislamu kuhusu uvamizi wa ardhi ya Waislamu ambapo inakua ni wajibu, (fardh ‘ayn) kupigana na mvamizi na kumuondoa katika ardhi ya Waislamu. Uwajibu huu unaanza kwa Waislamu wa maeneo ya karibu na ardhi iliyovamiwa, bali kimsingi unaenea kwa Waislamu wote.
Mtazamo huu unalazimisha zipatikane hatua za kivitendo za kijeshi kutoka kwa majeshi ya nchi jirani za Waislamu kuwanusuru Waislamu wa Palestina kutokana na dimbwi la ukatili na dhulma kutoka kwa mayahudi.
Aidha, mtazamo huu unawajibisha Umma wa Kiislamu kujifunga na suala nyeti la kurejesha tena dola ya Kiislamu ya Khilafah ambayo itatabikisha sharia zote za Allah Taala ikiwemo ya kutoa majeshi kwa ajili ya kupambana na wavamizi iwe ndani y a Palestina, Kashmiri nk.
Ni kwa kukosekana kwa Khilafah ndiyo kumetoa mwanya kwa Mazayuni na maadui mbalimbali wa Uislamu kuvamia, kuuwa, kutesa na kupora rasilmali nk. bila ya kuwajibishwa na yoyote.
Ni wajibu kwetu Waislamu katika kuangazia qadhia ya Gazza na nyengine zote kujifunga na suluhisho la Kiislamu tu, na kushiriki katika mchakato wa kulirejesha suluhisho hilo kivitendo.
“Damu ya Gaza inaendelea Kumwagwa”
Risala ya Wiki No. 181
16 Dhu -al Qidah1445 Hijria | 24 Mei 2024 Miladi
Afisi Ya Habari – Hizb Ut Tahrir Tanzania
Maoni hayajaruhusiwa.