Kitengo cha Wanawake: Kampeni ya Ramadhan: “Kutafuta Mafanikio Usoni Mwa Matatizo”
بسم الله الرحمن الرحيم
Tunaingia Ramadhan tofauti na Ramadhan nyenginezo tulizo zishuhudia nyuma. Wengi katika kaka zetu na dada zetu kwa huzuni kubwa wamewapoteza wapendwa wao kwa virusi hivi katika muda wa wiki chache zilizo pita, huku wengine wengi wakiwa wako hospitalini kutokana na maambukizi haya. Yote tisa, kumi Ummah wetu nchini Syria, Yemen, Kashmir, Gaza, Myanmar, China na kwengineko wanakabiliwa na janga hili huku wakiwa chini ya mvua ya mabomu na risasi au huku wakiteseka kutokana na hali zisizo vumilika za unyanyasaji, uvamizi au vifo ndani ya kambi za wakimbizi. Ufungiwaji watu majumbani katika nchi pia umesababisha kaka zetu na dada zetu wengi kuteseka kutokana na matatizo ya kifedha, huku wengine wakitenganishwa na familia na marafiki zao. Na wengi wetu wamenyimwa utamu wa kuswali swala za Ijumaa na Taraweh na kufuturu pamoja kama jamii.
Miongoni katikati ya mitihani na giza lote hili, wakati mwengine yameza kuwa vigumu kuona mwangaza wowote. Lakini pamoja na hivyo, hakika sisi kwa sifa yetu kama waumini, dini yetu inatupa habari kuwa mitihani na shida, na kupoteza na madhara hutupa fursa. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
أَحَسِبَ ٱلنَّاسُ أَن يُتۡرَكُوٓاْ أَن يَقُولُوٓاْ ءَامَنَّا وَهُمۡ لَا يُفۡتَنُونَ * وَلَقَدۡ فَتَنَّا ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۖ فَلَيَعۡلَمَنَّ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ صَدَقُواْ وَلَيَعۡلَمَنَّ ٱلۡكَـٰذِبِينَ
“Je! Wanadhani watu wataachwa kwa kuwa wanasema: Tumeamini. Nao wasijaribiwe? Hakika tuliwajaribu walio kuwa kabla yao, na kwa yakini Mwenyezi Mungu atawatambulisha walio wa kweli na atawatambulisha walio waongo.” [Al-Ankabut (29): 1-3]
Hivyo basi, mitihani na madhara haya ni fursa iliyo tujia sisi kama Waislamu ili kumthibitishia Muumba wetu Mtukufu kwamba hakika sisi ni wenye ikhlasi katika imani yetu kwa sifa yetu kama waumini, pindi tutakapoyatumia haya kama njia ya kuvuna nyongeza ya kujikaribisha na kujisalimisha kwa Mola wetu (swt). Hakika hii ni fursa ya kuzitathmini nafsi zetu kama waumini na kama Ummah katika nukta za udhaifu wetu na mapungufu yetu katika kutii Maamrisho yote ya Mola wetu mpaka tuweze kuyashinda na tukithirishe ibada kwa Mwenyezi Mungu. Lakini haya vilevile ni fursa ya kutafakari hali ya ulimwengu ambao tunaishi ndani yake, na nidhamu na mifumo na kanuni ambazo zinahukumu nchi na ambazo zinazidisha ukali wa migogoro ambayo inaathiri watu, ikiwemo janga hili liliko sasa, pamoja na kuwa zinasababisha matatizo makubwa mno ambayo tunawaona wanadamu wakiteseka kwayo; hakika hii ni fursa ya kutafakari namna ya kuyabadalisha yote haya. Kwa hivyo, hakika mitihani na shida ni fursa ya kuleta mabadiliko mazuri ya kihakika ndani ya nafsi zetu na nchi zetu na ulimwengu wetu.
Hivyo basi vipi tutaweza kuitumia Ramadhan hii katika hasara ambayo tunateseka kwayo, au madhara au matatizo mbayo tunakabiliana nayo… ilituibuke wenye nguvu zaidi? Na wenye nguvu zaidi kama Ummah katika sifa yetu na kufikiri kwetu na ufahamu wa Dini yetu hadi tuchukue nafasi anayoitaka Mwenyezi Mungu kwetu katika dunia hii – Mashahidi kwa Watu katika njia ya Dini yake, mpaka tuweze kupata mafanikio katika dunia hii na katika Akhera.
Na sisi katika Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir tutayaeleza maswala haya “Kutafuta Mafanikio Usoni mwa Matatizo” kama kauli mbiu ya mwezi wa Ramadhan ulio barikiwa wa mwaka huu wa 1441 H.
Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Ijumaa, 01 Ramadhan Iliyo Barikiwa 1441 H sawia na 24 Aprili 2020 M
Maoni hayajaruhusiwa.