Jee Unatamani Na Wewe Kuwa Sheikh?
بسم الله الرحمن الرحيم
Leo Masheikh wamegawika makundi haya:
a. Kundi la kwanza, wenye maisha mazuri ya raha mustarehe. Hawa ni wale wanaoramba nyayo za wanasiasa, na kila muda kubadilisha fatwaa zao kwa matakwa ya wanasiasa na matajiri, leo husema haramu kesho halali.
b. Kundi la pili, masheikh duni na njaa kali. Hawa huishia kufungwa jela kwa misimamo yao thabiti ya dini, na mwisho kutiwa maradhi na kuuliwa kinyama.
c. Kundi la tatu, waganga wa kienyeji, waongo, matapeli, wapiga ramli na dua za kuuza kwa kupatana. Utamsikia anayeitwa sheikh anamuuliza mteja unataka uombewe dua ya shilingi ngapi?
d. Kundi la nne, wachache wasio na umaarufu mbele ya watawala na hawana kundi la watu wengi nyuma yao. Hawa maisha yao ni kama ya wengine, ima watakuwa nacho au watakuwa hawana. Kundi hili ni wale ambao wamesoma dini kwa ikhlasi, na hawakuifanya ndio kazi yao ya maisha. Bali wamesoma dini kama jukumu na ibada tu.
Leo wengi wanaosoma dini wanatafuta kuwa kwenye kundi la kwanza. Hao utawaona wanachotafuta ni umaarufu kwa nguvu zote, kujipendekeza, kujipenyeza kwa watu wenye ulua, kuwasifu watawala na kutukana masheikh wenzao. Misimamo ya masheikh wa kundi hili ni kwa mujibu wa upepo unakoelekea. Hapo ndio hutoa fatwa, wapi Waislamu waelekee.
Kundi hili (la kwanza), ndio maulamau waovu ambao Mtume SAAW kasema wao na kundi la tatu ndio wa mwanzo kuwashiwa moto wa Jahiim.
Amma kundi la pili na la nne, hao ni wa kuombewa dua ili wapate mwisho mwema (husnu khaatima)
Khilafah itakaposimama, vitabu, makala, video na makabrasha ya masheikh wa kundi la kwanza yatachomwa moto, isipokuwa zitahifadhiwa nakala chache (kutokana nayo) kwenye sehemu malum, ili kuoneshwa vizazi vijavyo katika somo la historia: kwamba kilipita kipindi kibaya cha uzorotevu wa Umma wa Kiislamu kiasi kwamba baadhi ya masheikh walifikia uduni na udhalili wa kumilikiwa na kununuliwa na wanasiasa wa kikafiri, Waislamu waovu na matajiri mafasiki.
Imeandikwa na Ustadh Ramadhan Moshi (Agosti 2015)
Allah Taala Amkomboe kutoka katika mikono ya madhalimu -Amiin
Maoni hayajaruhusiwa.