Janga la Hiroshima Na Nagasaki— Marekani Gaidi Namba Moja.

بسم الله الرحمن الرحيم

Ilikuwa Agosti 6, 1945 Marekani ilitumia bomu la atomiki kuiangamiza miji miwili ya Japan na watu wake. Kitendo ambacho hakikuwahi kutokea kabla yake na hata zama hizi.
Kwa kutumia ndege ya kivita aina ya B-29 bomber, Jumatatu ya tarehe 6, Agosti 1945 Marekani iliiangamiza kabisa mji wa Hiroshima, Japan kwa bomu lenye urefu wa futi 10 ambalo lilitapika tani 20,000 za mionzi ya TNT na kwa mkupuo mmoja ilitosha kuiyeyusha Hiroshima, takriban kwa pamoja na robo tatu ya majengo 90,000, watu 350,000 na kila kilichokuwepo wakati ule kiliangamia.
Kwa hivyo, ndani ya dakika 3 Hiroshima ikawa imevurugika. Kama tukio hilo halitoshi ndani ya masaa matatu baadae Marekani ikatupa bomu jengine la aina hii hii katika mji mwengine wa Nagasaki.
Leo dunia imesheheni malimbikizo na shehena kubwa za silaha za maangamizi na maelfu ya vituo vya nishati vyenye kutumia nishati ya nyuklia, itapotokea ajali au vita na dola moja ikatumia mabomu haya au ajali itayoripua mabomu ya nishati hii au kuripuka vituo vingi kwa wakati mmoja, dunia itakuwa vipi? kama lile shairi la Jane Franklin “nani amcheke nani “.
Dunia isisahau miripuko midogo tu ya vituo vya nishati za nyuklia vya Chernyobyl, Ukraine mwaka 1986 na ule wa Fukushima, Japan mwaka 2011 jinsi ulivyoleta madhara makubwa kwa mali na maisha ya wanadamu.
Hata hivyo, Marekani ndiyo yenye shehena kubwa zaidi kwa sasa duniani na ndiye iliyowahi kutumia silaha za aina hii za maangamizi. Pamoja na hayo inatumia uwezo wake wa kiuchumi kuongeza shehena hizi na kuzitisha na kuzibana dola nyengine dhaifu atakavyo ili zisimiliki silaha aina hii au kama tayari wanamiliki basi waziangamize.
Lau dola ya Khilafah inasimama itapaswa kumiliki silaha kama hizi ili kuzitishia nchi za makafiri, kwa kuwa kuwatishia makafiri ambao ni maadui wa Allah Taala ni amri kutoka kwa Muumba.
Aidha, kwa upande wa pili, Marekani dola gaidi namba moja na Washirika wake pamoja na mfumo waliobeba ni wajibu wanyang’nywe usimamizi wa dunia kwa mbadala wa mfumo wa haki na uadilifu ili wasije wakawadhuru wanadamu zaidi kama walivyofanya na wanavyoendelea sasa. Na hilo litawezekana kwa kuwa dola ya Kiislamu ya Khilafah kimaumbile ipo juu ya misingi ya haki na uadilifu.
Katika juhudi za kuuondoa mfumo wa kibepari na wanaoung’ang’ania tusitishike na silaha na nguvu zote walizonazo makafiri. Sisi tuna Mwenye nguvu zisizoshindwa ambaye ni Allah SWT, Kamnusuru Mtume wake SAAW na Waislamu katika vita vingi vikiwemo vita vigumu vya makundi (Al-Ahzab), kattu Allah SWT hatoshindwa kutunusuru sisi kwa zama hizi. Allah Anatukumbusha yaliyojiri katika Vita vya Ahzab kwa kusema:
وَرَدَّ اللَّهُ الَّذِينَ كَفَرُوا بِغَيْظِهِمْ لَمْ يَنَالُوا خَيْرًا وَكَفَى اللَّهُ الْمُؤْمِنِينَ الْقِتَالَ وَكَانَ اللَّهُ قَوِيًّا عَزِيزًا
(الأحزاب:25 )
“Allah Aliwarudisha nyuma makafiri juu ya ghadhabu zao na hawakupata kheri yoyote. Allah Amewatosheleza Waumini katika vita. Na Allah ni mwenye nguvu na uweza” (TMQ Ahzab: 25)
Tichaa Suley

Maoni hayajaruhusiwa.