Hizb ut Tahrir Tanzania Yazuru Ubalozi wa Pakistani Kuitaka Kukomesha Utekaji wa Kimabavu wa Naveed Butt

بسم الله الرحمن الرحيم

Kufuatia kampeni ya kilimwengu inayoendelea ya kunyakuliwa Naveed Butt, msemaji wa Hizb ut Tahrir, Wilaya ya Pakistan ambaye alitekwa nyara na  Shirika la kijasusi la Pakistani zaidi ya miaka 9 iliyopita.

Jana tarehe 29 Juni 2021, Hizb Ut Tahrir Tanzania ilituma ujumbe kwa Ubalozi wa Pakistani jijini Dar es Salaam ulioongozwa na Masoud Msellem, Mwakilishi Kwa Vyombo vya Habari akiwa pamoja na Said Bitomwa, Mjumbe wa Afisi ya Habari, kwa dhamira ya kupeleka risala rasmi ya Hizb ut Tahrir yenye anuani: “Mwito wa Kukomesha Utekaji nyara wa Kimabavu wa Naveed Butt nchini Pakistani”.

Risala hiyo imeitaka Pakistani kumuachia huru mara moja mhandisi Naveed Butt aliyetekwa mnamo tarehe 11 Mei 2012 kimabavu na kihalifu na mchana kweupe mbele ya watoto wake.  Tangu muda huo mpaka leo familia yake imebakia gizani wakiwa hawajui alipo Naveed.

Baada ya kusawazisha taratibu za kiusalama katika Ubalozini hapo, ujumbe ulikutana na Bwana Nafees Wahab, Afisa Utawala, ambapo ujumbe ulijitambulisha kwake na kumueleza lengo lao. Katika hali ya kuonesha mashirikiano Afisa huyo (wa ubalozi) akapokea nyaraka za ujumbe, kuzikagua na kuutaka ujumbe uketi kwa subra huku akiratibu mkutano baina yao na mkubwa wake (balozi)

Ujumbe ulikutana na Bwana Azam Bihan, Makamo wa Balozi, ulizungumza nae kuhusiana na qadhia ya kutekwa Naveed, na ukataka kukomeshwa mara moja kutekwa huko kwa mabavu. Majibu ya Bwana Bihan yalikuwa, akiwa kama mwakilishi wa  serikali ya Pakistani amepokea risala ya ujumbe huo, na ataifikisha kwa serikali yake, endapo atapokea majibu yoyote juu ya qadhia hiyo kutoka serikalini , atawasiliana na ujumbe huo kwa kutumia anuani zao.

Muda umefika kwa mukhlisina ndani ya mamlaka za Pakistani na kwa wale wote wenye athari na ushawishi kubeba jukumu la kufedhehi tendo hili la aibu na kusimama thabiti na Uislamu na haki, wasimame kwa kupinga vikali dhulma na uvunjaji haki wa serikali ya watawala wa kihuni na vibaraka  pamoja na  mabwana zao wa magharibi, ili achiwe huru Naveed Butt ili arudi kwa  familia yake baada ya miaka  ya maumivu na kuwa kizuizini.

Masoud Msellem
Mwakilishi Kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Tanzania

KUMB: 1442 / 09 Jumatano, 19 Dhul Qi’dah 1442 H 30/06/2021 M

Maoni hayajaruhusiwa.