Hizb ut Tahrir / Tanzania Yatuma Ujumbe Maalum Kwa Ubalozi Wa China

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Siku ya Ijumaa tarehe 5 Aprili 2019/ 29 Rajab 1440 Hijri, Hizb ut Tahrir Tanzania ilituma ujumbe maalum kwa Ubalozi wa China nchini Tanzania ili kufikisha barua maalumu kuhusiana na dhulma ya serikali ya China dhidi ya Waislamu wa jamii ya Uyghurs.

Ujumbe huo uliongozwa na Masoud Msellem – Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb Tahrir Tanzania, akiwa pamoja na Said Bitomwa, Mjumbe katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Tanzania, na kuwasili Ubalozini hapo takriban saa 5.45 mchana.

Walinzi wa Ubalozi katika lango kuu la kuingilia walipokea barua iliyokuwa katika nakala nne za lugha ya Kichina, Kiuyghurs, Kiarabu na Kiswahili. Tulipowaomba walinzi hao kutaka kuonana na Afisa yoyote wa Ubalozi huo, walitujibu kwamba taratibu zao ni kupokea barua tu pamoja na anuani za waletaji, na endapo Ubalozi utaona kuna haja ya kuonana na waletaji, basi hupanga miadi kwa jambo hilo.

Kupitia waraka huu, tunatoa msisitizo mkubwa kwa Ubalozi wa China wapange miadi ya kukutana nasi ili kuwasilisha ujumbe wetu kwao ana kwa ana.

Barua iliyofikishwa Ubalozini hapo ilikuwa ni waraka wa taarifa kwa vyombo vya habari uliotolewa na Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir iliyobeba anuani: ”Khilafah Itakomboa Turkestan Mashariki Na kuwanusuru Waislamu wa jamii ya Uyghur kutokana na dhulma na uhalifu wa China.”

Ambapo sehemu ya taarifa hiyo ilitamka yafuatayo:”
“Wakati utawala wa China ukiendelea kuwanyanyasa Waislamu wa Uyghur kwa kutumia kila mbinu za kikatili ikiwemo kuwazuilia wasitekeleze ibada zao, wasihudhurie misikitini kwa kuifunga misikiti hiyo, kuwalazimisha wasifunge katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, na kimsingi kuwazuilia ibada zote za Kiislamu, hadi karibuni wamezindua kambi kubwa za kuwafunga na kuwafanya mahabusu Waislamu zaidi ya milioni 1, ati ni kampeni inayodaiwa “kupambana na ugaidi” kwa kisingizio cha urongo cha “mafunzo mafupi ya kitaaluma” na huku ikiwashikilia wasomi, wanasayansi, wanafikra na maprofesa wa vyuo vikuu. Yote hayo ili kueneza khofu na vitisho katika nyoyo za Waislamu hao ili wanyenyekee hali ya kutoshikama na na Dini yao ya Kiislamu.”

Kisha waraka huo ukakhitimisha kwamba, ni dola ya Kiislamu ya Khilafah Rashidah (Khilafah iliyoongoka) kwa njia ya Utume, ambayo itasimama karibuni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu ndio itakayoleta ushindi kwa ndugu zetu wanaodhulumiwa (madhloum) ndani ya Turkestan Mashariki, na itachukua hatua thabiti dhidi ya wahalifu wote waliosimama dhidi ya Waislamu hao.
Mtume (saw) anasema:
«إِنَّمَا الإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ»
“Hakika kiongozi ni ngao, mtapigana nyuma yake, na mtajilinda kwae”

Na wakati huo, si China wala mwengineo atakayethubutu kumdhuru Muislamu, kwa sababu watajionea wazi wazi kuwa chochote watakachowatendea Waislamu (katika dhulma) kitarejeshwa kwao maradufu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye Nguvu na Asiyeshindika/Aziz.

Na Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Tanzania
Kumb: 1440 / 05
Jumamosi, 30 Rajab 1440 AH
06/04/2019 CE

Maoni hayajaruhusiwa.