Hizb ut Tahrir / Tanzania Inalaani Kutekwa na Kuuwawa Muhammad Ali Kibao

بسم الله الرحمن الرحيم

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

 

Hizb ut Tahrir / Tanzania inatoa mkono wa pole na kuifariji familia na jamaa kufuatia kuuwawa kwa Muhammad Ali Kibao ambaye alitekwa Septemba 6, 2024 na kisha kuuwawa.
Tunalaani vikali utekaji huo na mauaji hayo ya kikatili, kisha tungependa kutamka yafuatayo:
1. Vitendo vya utekaji vinavyopelekea kupotezwa au kuuliwa kikatili si vigeni Tanzania, vimekuwapo kwa muda sasa, ambapo wahanga wakubwa wa ukatili huo ni Waislamu kwa Uislamu wao. Kwa mfano, kuna wahanga zaidi ya 380 hawajuulikani walipo katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji kufuatia kamata kamata ya serikali ndani ya mwaka 2017 iliyoambatana na mateso na mauaji ya kiholela’(The East African, May, 2018)
2. Matukio kama haya sio tu yanaleta khofu,ukosefu wa amani, kuchafuka na kuathirika haiba ya serikali, bali pia ni kielelezo cha wazi cha kukosekana uwajibikaji wa serikali, kwa kuwa dola ndio mdhamini mkuu na mlinzi wa usalama wa raia, mali zao na heshima zao.
3. Aidha, matukio kama haya yanaonesha wazi wazi kushindwa kwa mfumo wa kibepari na demokrasia yake ulimwenguni kote, kwa kuwa mfumo huo unazua machafuko, vurugu na utovu wa amani kwa wanadamu.
Ni wazi ulimwengu unahitaji mfumo wa haki na uadilifu ambao si mwengine bali ni Uislamu. Mfumo huo una uwezo wa kudhamini ulinzi wa raia, maisha yao, mali zao na heshima zao.

Maoni hayajaruhusiwa.