Fadhila za Masiku Kumi ya Dhul-hijjah

Karibuni InshaAllah tutaingia katika siku kumi tukufu za Dhulhijjah. Kwa jinsi zilivyokuwa na utukufu mkubwa siku hizo kumi Allaah (Subhaanah wa Ta’ala) Ameziapia katika Qur-aan Anaposema:
وَالْفَجْرِ 
وَلَيَالٍ عَشْرٍ
Naapa kwa Alfajiri Na kwa masiku kumi [Al-Fajr: 1-2] Wanavyuoni wafasiri wa Qur-aan wamekubaliana kwamba zilozokusudiwa hapo ni Siku kumi za Dhul-Hijjah. Siku za manufaa na kumkumbuka Allah Taala Inapasa kumdhukuru mno Allaah (Subhaanah wa Ta’ala) katika siku hizo kwa kukumbuka neema Zake zisizohesabika: Allah Taala Anasema: لِيَشْهَدُوا مَنَافِعَ لَهُمْ وَيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ فِي أَيَّامٍ مَعْلُومَاتٍ “Ili washuhudie manufaa yao na kulitaja Jina la Allaah katika siku zinazojulikana” [Al-Hajj: 28]. Ibn ‘Abbaas ra. kasema: “Hizo ni siku kumi za Dhul-Hijjah” . Manufaa ya Akhera yanajumuisha kupata Radhi za Allaah SW na manufaa ya vitu vya dunia inajumuisha wanyama wa kuchinjwa na biashara. [Tafsiyr Ibn Kathir]. Ubora wa amali katika siku hizo. Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) kasema kwamba : Mjumbe wa Allaah SAAW Amesema: “Hakuna siku ambazo vitendo vyake vyema Anavipenda Allaah (SW) kama siku kumi hizi. (siku kumi za mwanzo wa mwezi wa Dhul-Hijjah) Akaulizwa, je, hata Jihaad katika njia ya Allaah? Akajibu SAAW : Hata Jihad katika njia ya Allaah isipokuwa mtu aliyekwenda na nafsi yake na mali yake ikawa hakurudi na kimojawapo [Al-Bukhari]. Masiku haya yamejumuisha Ibada muhimu kama Swalah, Swaum, Swadaqah, Hajj na Umra, wala hazijumuiki hizi wakati mwingine. Kufunga siku hizi, hususan Siku ya Arafa. Kutoka kwa Abu Sa’iydil-Khudhwriyy (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: ((Mwenye kufunga siku ya Arafa kwa ajili ya Allaah, basi Allaah Atamuokoa uso wake kutokana na moto kwa umbali wa miaka sabini)) [Al-Bukhari na Muslim]. Amesema pia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) “Kila Amali njema ya mwanaadamu inalipwa mara kumi na inaongezewa thawabu kutoka kumi hadi mia saba, na Allaah Anasema isipokuwa Swawm, kwani hiyo ni kwa ajili Yangu na Mimi” Ndiye nitakayemlipa) [Al-Bukhari na Muslim].

Maoni hayajaruhusiwa.