Enyi Waislamu, Waokoeni Watoto wa Yemeni Wanaouawa

Mnamo tarehe 21/11/2018, taarifa kutoka taasisi ya kiingereza iitwayo (save the children) ilieleza kwamba kiasi cha watoto wapatao 85000 wenye umri wa chini ya miezi mitano wanakadiriwa kupoteza maisha katika kipindi cha miaka mitatu ya vita ndani ya Yemeni. Idadi hii  ni sawa na  jumla ya watoto wa chini ya miaka mitano katika mji wa Birmingham, mji wa pili kwa ukubwa ndani ya British.

Taarifa hiyo haijumuishi  waliouliwa wakiwa umri juu ya miaka mitano na wale waliouliwa kwa mabomu na miili yao kukatwa mapande mapande au wale waliofanywa miili yao ifanane na mashetani  kwa sababu ya njaa na maradhi ya mlipuko.Vipi kama Uingereza, Marekani na nchi za kimagharibi kwa pamoja wangepoteza namba kubwa ya  watoto wao kwa kuuwawa kama walivyouwawa watoto wa Yemenijamii ya kimataifa itasimama upande gani kwenye suala hili la kupoteza watoto.

Lakini watoto wa Yemeni wamekuwa kama yatima mbele ya watu makatili,  hawana yeyote anayewapazia sauti na kuwatetea, wamekuwa kama  sahani ya chakula ambayo mataifa yameikusanyikia, hii ni moja ya sura ovu ya inayofanywa washirika wa Marekanindani ya Yemeni. Kibaya zaidi na chenye kutia aibu ni kwamba wale wanaotumika katika kupambana na kuuwa, kusababisha njaa na kuharibu makazi ya watu waYemeni ni wale ambao wanaudugu  wadamu, imani, lugha na dini. Hizo ni washirika zilizoungana  katika mkakati wa kuuhalalisha utawala wa raisi hadi ni kwa upande mmoja,na upande mwengine kuna Irani ambao wao wapo upande wa jeshi la ma Mahouth, hayo yote hufanywa kwa malengo wa kupata utawala na kuvuna utajiri. Vita nchini Yemeni  inakaribia kutimiza miaka minne tanga kuanza kwake ambapo raia wasio na hatia ndo waathirika wakubwa.

Mwezi  uliopita, umoja wa mataifa ulionya kuwa million 14 ya raia wa Yemeni  wanatarajiwa kukabiliwa na njaa, wakati ambapo Yemeni wanautajiri mkubwa sana kiasi cha kuifanya iwe kama kama lulu ya mashariki ya kati. Yemeni ina hazina kubwa ya miamba muhimu kwa ajili ya matumizi ya kutengenezea malighafi kwa ajili ya ujenzi na pia inautajiri wa chokaa, na ni nchi ya pili yenye hazina kubwa ya gesi ya asili ndani ya Uarabuambapo kwa utajiri huo ingeweza kutatua tatizo hilo la balaa la njaa, magonjwa ya mlipuko, umasikini na kukosa makazi. Madini (dhahabu,silva,mafuta), kilimo/ufugaji na uvuvi vinatosha kuifanya Yemeni  kuwa ni taifa kubwa tishio kiuchumi. Pia kijografia ipo katika  mlango unaounganisha pande mbili za kivuko inayoitwa Bab al-Mandab strait ambacho  kina unganisha mashariki na magharibi kibiashara. Utajiri huu ndo uliopelekea nchi za kimagharibi ziimezee mate kiasi cha kuiharibu na kuisababishia maangamivu, watu wanakufa kwa njaa kila baada ya dakika kumi

Mtume (saw) anasema:

إِذَا مَرَّ بِكُمْ أَهْلُ الْيَمَنِ يَسُوقُونَ نِسَاءَهُمْ، وَيَحْمِلُونَ أَبْنَاءَهُمْ عَلَى عَوَاتِقِهِمْ، فَإِنَّهُمْ «

» مِن ي، وَأَنَا مِنْهُمْ

“Pindi wakiwapitia watu kutoka Yemen wakiwa wameambatana na wanawake huku wakiwa wamewabeba watoto zao mabegani mwao, basi fahamuni hakika mimi nimejaa vifuani mwao na wao wamejaa kifuani mwangu (kwa mapenzi)”

[Ameisahihisha At-Tabarani, na Hasan Isnad]

Hali ya Yemeni na watu wake na juu ya yote yanayowafika  ni hali yennye kuhuzunisha na isiosahaulika, wanauliwa mbele yetu na tunaumia sana kama waislamu, tumeacha mafundisho ya Mtume wa Allah aliyotufundisha katika hadithi nyingi sana ambazo aliwasifia watu/waislam wa yemen nakuwaombea dua mara kadhaa aliposema: اللَّهُمَّ بَارِكْ لَنَا فِيْ شَامِنَاوَيَمَنِنَا  “ewe Allah ibariki miji ya Sham  na Yemeni”

Ni khilafah kwa njia ya utume ndio yenye uwezo wa kupambana na makafiri pamoja na washirika wao nakuziainisha njama zao dhidi ya Yemeni na kuzuia maangamivu wayafanyayo dhidi ya waislamu na raia wa Yemeni na kuizuia mikono ya waislamu kutapakaa damu za waislamu wenzao na kukomesha mapigano  ya waislam wao kwa wao kwa kuondoa visababishi vinavyopelekea vita nakuifanya Yemeni iwe na amani na ubora. Mtume (s.a.w) amesema “Mji umefunguliwa, ushindi kutoka kwa Allah umefika, watu wa Yemeni wamefika. Akasema mtu; ewe Mtume wa Allah niwapi hao watu wa Yemeni? Akasema ; ni watu wenye mioyo laini na mizuri, imani ipo kwao, hekima ipo kwao na fiqh ipo kwao”.

Maoni hayajaruhusiwa.