Enyi Ummah wa Kiislamu Kote Ulimwenguni: Pokeeni Salamu Zetu

بسم الله الرحمن الرحيم

1. Umma wetu uko katika ufukara, umaskini, vita na kila aina ya dhulma na udhalilishwaji, licha ya nchi zetu kuruzukiwa kila aina ya kheri na neema kuanzia, rasilmali watu, maliasili, nguvu za kijeshi kutuhami nk. Lakini zimekosa usimamizi wa ikhlasi na uchamungu na badala yake watawala vibaraka wamezitumbukiza katika nyumba ya maangamizi ( daara lbawar)

Masoud Msellem – Mwakilishi kwa vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir Tanzania akitoa salam za Eid el-Fitr kwa ummah wa kiislamu

2 Shawwal 1441 H – 24 Mei 2020 M

.

Allahu Akbar Allahu Akbar Allahu Akbar

Hizb ut-Tahrir Tanzania inawapongeza Waislamu dunia nzima kwa kuingia siku tukufu ya Idd ul Fitri na kumalizika Ramadhani.

Tunamuomba Allah SW atukubalie ibada zetu za funga, visomo vyetu vya Qur-ani, Qiyamul-layli, swadaqa na amali nyengine, pamoja na kuturuzuku fadhila zote za mwezi mtukufu na pia kutulipa lililo bora zaidi nalo ni radhi Zake.

Pia tunawakumbusha Waislamu kutekeleza faradhi ya Zakatul-fitri na sunna zote za idd-ul-fitri kuanzia kutanguliza iftar kabla ya swala, Swala ya idd, kujipamba kwa mapambo halali, kutembelea ndugu, jamaa na kuisherehekea Iddi kwa namna zote halali.

Pamoja na kuwa Idd kuwa ni furaha, tunawakumbusha Waislamu kuwa wao ni sehemu ya Ummah mmoja kote duniani, na hivyo tuna wajibu wa kuwafikiria Waislamu wenzetu ambao wanaingia katika Idd hii hali ya kuwa wanadhulumiwa kama vile dhulma za wayahudi huko Palestina, mauaji ya Syria, Yemen, Somali, Myanmar, Afghanistan nk. Bila ya kusahau ndugu zetu waliowekwa vizuizini katika magereza kwa kisingizio cha sheria ya kibaguzi ya ugaidi hapa Tanzania na duniani kote.

Kadhalika Waislamu wasiache Ibada na wakarejea katika maasi, kufanya hivyo ni kuharibu lengo la Funga, pia tuwakumbuke wajane mayatima, wagonjwa na wasiojiweza, na tuwe karibu na Ndugu zetu.
Aidha, tunaukumbusha Ummah wa Kiislamu kuwa idhlali hii na unyonge kama huu hautoondoka ila kwa kuwepo Mfumo wa Kiislamu Khilafah na kuulingania kwake ni faradhi kama zilivyo faradhi nyengine kama Swala, Funga, Zaka, nk.

Tunawalingania Waislamu wale waliopo katika Nchi kubwa za Waislamu kusimamisha serikali ya Kiislamu (Khilafah) ili tuweze kusheherekea Idd kwa furaha kwa Ummah wote na pia kuzitekeleza hukmu zote zilizobakia kwa ukamilifu wake.

WA KULLU ‘AAMUN WA ANTUM BIKHAIR.

01 Shawal 1441 Hijri/ 23/05/2020

Sheikh Mussa Kileo
+255 684 39 39 96
Mwenyekiti Kamati ya Mawasiliano Hizb ut Tahrir Tanzania

#UislamuNdioUfumbuziSahihi

Maoni hayajaruhusiwa.