Corona Yadhihirisha Zaidi Uovu wa Ubepari

بسم الله الرحمن الرحيم

Rais wa Marekani, Donald Trump, amewataka wananchi wa nchi hiyo kurejea katika biashara na shughuli zao za kila siku haraka iwezekanavyo, akidai kuwa idadi ya watu watakaojiua kutokana na msongo wa mawazo nchini humo itakuwa kubwa ikilinganishwa na ile ya wanaokufa kutokana na ugonjwa wa covid-19 (corona).

“Karibuni tutalegeza agizo la kuwataka watu wazingatie masafa baina yao katika jamii, ili kuzuia vifo vingi vitakavyotokana na msongo wa mawazo utakaosababishwa na mdodoro wa uchumi na msukosuko wa kijamii nchini. Vifo hivi huenda vikawa vikubwa zaidi ya Corona yenyewe.” Alisisitiza Rais Trump wiki hii.

Raisi Trump akiwa kiongozi wa dola kubwa ya kibepari anadai kuwa uchumi unapovurugika, nchi huwa inakodolea macho kesi za watu kujiua kutokana na matatizo za kisailokojia. (Parstoday)

Maoni

Huu ndio mfumo wa kibepari, mfumo thaqili na adui mkubwa kwa wanadamu ulivyo. Dola kubwa kinara wa ulimwengu kama Marekani licha ya utajiri wote walionao wanashindwa kuwaacha raia wao kuwasaidia kimaisha ili waendelea kuwa katika karantini ya maradhi mabaya ya Corona. Na badala yake raia wanatakiwa watoke wakafanye kazi. Marekani inashindwa kuhimili kuwahudumia raia wao kwa miezi michache ilhali watu hawa wamekuwa wakilipa makodi miaka yote.

Kunatakikana aina gani ya ushahidi juu ya uovu na kutofaa kwa mfumo wa kibepari.

25 Machi 2020

Masoud Msellem

Maoni hayajaruhusiwa.