Chanzo na Malengo ya Fikra ya Hatari ya ‘Dini Mseto’

بسم الله الرحمن الرحيم

 

Mtume SAAW na makhalifa baada yake waliubeba Uislamu kiukamilifu ukiwa ni haki kutoka kwa Mola wao bila ya kuchanganya haki hiyo na batil, kinyume na inavyopigiwa debe leo kwa kampeni batil ya ;dini mseto’.
Harakati hizi za ‘dini mseto’ zinazomaanisha kuleta ukuruba baina ya dini zilianza rasmi 1932 pale Ufaransa ilipotuma wawakilishi wake Chuo Kikuu cha Azhar ili kuasisi ukuruba baina ya Uislamu, Ukristo na Uyahudi.
Moja kati ya malengo makubwa ya fikra hii ya ‘dini mseto’ ni kutaka kuzuiya sheria za dini kutawala duniani. Na badala yake fikra ya ‘dini mseto’ inapigia debe kutawalisha sheria za kibepari na kidemokrasia zinazotokamana na akili finyu ya wanadamu kupitia mabunge. Yawe mabunge ya Marekani, Ulaya au nchi vibaraka ambazo baadhi tayari yamesharuhusu uovu mwingi kama ushoga, ulevi, utoaji mimba, kodi za kuuwa maskini nk.
Aidha, harakati za ‘dini mseto’ zinalenga kulaani na kuzuiya fikra ya dini yoyote kuwa na sheria na utawala, kwa hoja dhaifu kuwa dini zitaleta fujo na maafa duniani. Ilhali maafa, mauaji, mateso na vita visivyokwisha duniani leo na vilivyotangulia vimesababishwa na ubepari na demokrasia yake na wala sio dini.
Hata pale kunapokuwa na vita vinavyojidhihirisha kuwa vya kidini, mara nyingi kama sio zote, kwa leo madola ya kibepari ndio waasisi wa vikundi vingi kwa malengo maalumu, na pale wanapoona wavimalize vikundi hivyo, huviangamiza. Basi kwanini wanaolingania fikra hizi wasingelaani mfumo huu wa kibepari wenye maafa, badala yake wanapambana na kitu ambacho wanakhofu tu ikiwa kitapatikana kitaleta maafa? Mbona wanajitia upofu katika jambo lililowazi?
Malengo hayo ya’dini mseto’ ya kuhubiri sheria za kidini zisiruhusiwe kumuongoza mwanadamu madamu tu kwa kuwa dini zingine hazina sheria za siasa na kiutawala sio tu ni hoja dhaifu, bali ni wazi kuwa hapa mlengwa mkuu ni Uislamu, kwa kuwa ndio dini pekee yenye sheeia na miongozo katika nyanja ya utawala. Na mchakato wa harakati hizi zina dhamira ya kuungamiza kijanja kwa kuonesha dini mseto wanakabili dini zote.
Uislamu haukubali kamwe kuhoji sharia zake, bali hauruhusu kabisa kushirikiana na dini zingine katika mambo ya kiimani na kidini. Bali Uislamu unaruhusu Waislamu kushirikiana na wasiokuwa Waislamu katika miamala binafsi ya kijamii na kiuchumi kama ujirani, biashara, kusaidiana nk. Lakini sio kuungana kidini na kiimani na watu wa dini zingine, kama tunavyoona leo baadhi ya masheikh wakiingia makanisani na baadhi ya maaskofu kuingia misikitini.
Sisi katika Uislamu tunaamini kuchanganyishiwa Imani yet una Imani nyengine huo ni ukafiri. Na msimamo huu wa kutoshirikiana kiimani pia upo hata kwa dini zingine zisizokuwa Waislamu. Mathalan, kamwe hutosikia makanisa yakipiga marufuku kula nguruwe ili kuungana na Waislamu, japo tunaona wakristo na Waislamu wakisaidiana kwenyo matatizo yao. Basi vipi Muislamu anayeamini Mungu Mmoja, hakuzaa wala kuzaliwa kuungana na mtu anayeamini Mungu alizaa au alizaliwa, alikufa bali alicharazwa viboko kamwe? Hawawezi watu kuungana isipokuwa pale mmoja atakapoacha dini yake na kufuata ya mwingine.
Enyi Waislamu! mabepari wameshindwa kumletea mwanadamu ufanisi, furaha na amani ya kweli, ndio maana wanamtafutia mwanadamu amani ya kufikirika kupitia ‘dini mseto’. Kwa bahati mbaya, baadhi ya madalali wa kampeni hii pia wamo Waislamu ili iwe rahisi kuwarubuni watu wa kawaida.
Tunawazindua Umma juu ya hatari, fitna na balaa la ‘dini mseto’. Aidha, tunawadharisha Waislamu na wanadamu lkwa jumla juu ya amani ya kufikirika, huku wafadhili wa kampeni hiyo ya ‘dini mseto’ wakiendelea kuwarundika Waislamu magerezani kwa dhulma, mateso na kumwaga damu zao kila mahala.
Basi simamaeni imara enyi Waislamu kuifedhehi na kuikosoa vikali fikra hii ya hatari na ya kikafiri. Tunawalingania na kuwaita kwa ikhlasi Waislamu kuja katika uwajibu wa kurejesha tena dola ya Kiislamu ya Khilafah itakayodhamini kuulinda Uislamu na kila adui wa kivitendo au kifikra
Risala ya Wiki No. 211
9 Muharram 1447 Hijri / 04 Julai 2025 Miladi
Afisi Ya Habari – Hizb Ut Tahrir Tanzania

Maoni hayajaruhusiwa.