Aachwe Huru dada Yetu Romana

Ni utawala wa Muamerika wakati ambapo mwanamke muumini anatekwa usiku kutoka nyumbani kwake, eti kosa lake ni kusema mungu wake ni Allah(swt).

Katika masaa ya mwanzo ya tarehe 30 mwezi wa saba 2018, mtu wa usalama alimteka dada Romana Hussain, mwalimu anaeheshimika na mama mwenye watoto wanne. Ambae pia amehitimu katika fani za saikolojia na falsafa katika chuo maarufu cha St.Joseph pia anashahada ya uzamili (masters) katika fani ya masomo ya kiislamu. Pamoja na kutafuta vitabu na machapisho ya Hizb ut Tahrir katika nyumba yake mjini karachi, wahuni hawa walimteka , na walifanya hivyo bila kujali usalama wala ulinzi wa watoto wake. Kitendo hicho cha kinyama na dhalilifu dhidi ya Dada Romana ni mfano wa vitendo vya wajinga na mabedui katika maquraysh, ambao hawakujali heshima kwa wanawake, kwa kumuadhibu Sumayyah (ra) na kupelekea kumua na kuwa shahidi wa kwanza katika ummah wa Rasulillah (saaw). Kitendo hichi kilichofanywa dhidi ya Dada Romana ni kutoka katika maelekezo na maagizo ya marekani, ambae ndio bwana mkubwa wa utawala huu ambao wamekua wakiingia na kutoka katika Pakistani kupitia chaguzi, mapinduzi na mabadiliko madogo madogo. Na vitendo hivi vinaweka wazi ukweli kwamba “hakutakua na Pakistani mpya” na hakutakua na ” dola la madina” hata baada ya chaguzi. Kwa hakika, niwazi kwamba Pakistani itabaki kuwa ni jalala la marekani, wakati ambapo mwanamke muumini hatolindwa katika dini yake.
Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan inatanguliza maneno ya Allah swt na Mtume wake (saaw) kabla ya utawala mpya na waangalizi, labda pengine wanaweza kuwaidhika.
Allah (swt) amesema:

ﺇِﻥَّ ﺍﻟَّﺬِﻳﻦَ ﻓَﺘَﻨُﻮﺍ ﺍﻟْﻤُﺆْﻣِﻨِﻴﻦَ ﻭَﺍﻟْﻤُﺆْﻣِﻨَﺎﺕِ ﺛُﻢَّ ﻟَﻢْ ﻳَﺘُﻮﺑُﻮﺍ ﻓَﻠَﻬُﻢْ ﻋَﺬَﺍﺏُ ﺟَﻬَﻨَّﻢَ ﻭَﻟَﻬُﻢْ ﻋَﺬَﺍﺏُ ﺍﻟْﺤَﺮِﻳﻖِ

“Hakika wale waliowaadhibu waislamu wanaume na wanawake ,kisha wasitubie basi watapata adhabu ya jahannamu na watapata adhabu ya kuungua (barabara) .” [Surah Al-Buruj 85:10].

Mtume (saaw) amesema:
« ﻭﻣﻦ ﻋﺎﺩﻯ ﺃﻭﻟﻴﺎﺀ ﺍﻟﻠﻪ ﻓﻘﺪ ﺑﺎﺭﺯ ﺍﻟﻠﻪ ﺑﺎﻟﻤﺤﺎﺭﺑﺔ ‏»
“Yoyote atakae onyesha uadui kwa vipenzi vya Allah
(mawalii) basi atakua ametangaza vita.”
(imesimuliwa na Hakim kama ilivyopokewa kutoka kwa muadh bin jabal na katika hadithi alquds imesimuliwa hivi:
ﻗَﺎﻝَ ﺭَﺳُﻮﻝُ ﺍﻟﻠَّﻪِ ﺻَﻠَّﻰ ﺍﻟﻠَّﻪُ ﻋَﻠَﻴْﻪِ ﻭَﺳَﻠَّﻢَ : ‏« ﺇِﻥَّ ﺍﻟﻠَّﻪَ ﻗَﺎﻝَ ﻣَﻦْ ﻋَﺎﺩَﻯ ﻟِﻲ ﻭَﻟِﻴًّﺎ ﻓَﻘَﺪْ ﺁﺫَﻧْﺘُﻪُ ﺑِﺎﻟْﺤَﺮْﺏِ ‏»

“Mtume wa allah (saaw) amesema kwamba Allah amesema, ‘yoyote yule atakae wafanyia ubaya au kuwadhuru mawalii wangu natangaza vita dhidi yake’ …”
Bukhari].

Hivyo, Hizb ut Tahrir inawataka viongozi hawa wamuogope Allah(swt), na waache vitendo vyao viovu na wamuache huru haraka iwezekanavyo Dada Romana hussain arudi kwa watoto wake, wamruhusu aendelee na ulinganizi wake wa amani wakusimamisha uislamu kama njia sahihi ya maisha, kwa kupitia urejeshwaji wa Khilafah kupitia njia ya utume. Na viongozi hawa wapya wanaosisitiza kuendelea kuwa watumwa wa marekani wanapaswa kujua kwamba wanajidhalilisha wenyewe kwa kushindwa kujifunza kupitia kwa vibaraka makatili waliowatangulia .
Allah (swt) anasema:


ﺃﻓَﻠَﻢْ ﻳَﺴِﻴﺮُﻭﺍ ﻓِﻲ ﺍﻟْﺄَﺭْﺽِ ﻓَﻴَﻨْﻈُﺮُﻭﺍ ﻛَﻴْﻒَ ﻛَﺎﻥَ ﻋَﺎﻗِﺒَﺔُ ﺍﻟَّﺬِﻳﻦَ ﻣِﻦْ ﻗَﺒْﻠِﻬِﻢْ ﻛَﺎﻧُﻮﺍ ﺃَﻛْﺜَﺮَ ﻣِﻨْﻬُﻢْ ﻭَﺃَﺷَﺪَّ ﻗُﻮَّﺓً ﻭَﺁﺛَﺎﺭًﺍ ﻓِﻲ ﺍﻟْﺄَﺭْﺽِ ﻓَﻤَﺎ ﺃَﻏْﻨَﻰٰ ﻋَﻨْﻬُﻢْ ﻣَﺎ ﻛَﺎﻧُﻮﺍ ﻳَﻜْﺴِﺒُﻮﻥَ
“Hawaja safiri katika ardhi wakaona mwisho uliowapata waliopita kabla yao? Walikua ni wengi zaidi yao na walikua na nguvu katika ardhi, lakini vile walivyonavyo havikuwasaidia chochote.”
[Ghafir: 82].

Ofisi ya habari ya Hizb ut Tahrir
Katika Wilayah ya Pakistan

http://hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/press-releases/pakistan/15787.html

Maoni hayajaruhusiwa.