Waraka wa Kuhadharisha Kampeni Hatari ya Kuritadisha Vijana wa Kiislamu
بسم الله الرحمن الرحيم
Waraka huu ni muendelezo wa kampeni ya miezi miwili ya wanaharakati wa Hizb ut Tahrir Tanzania ili kupambana na fikra za ‘ukafiri mambo leo’ na kulinda usahihi wa Aqida ya Kiislamu. Kampeni hiyo ilizinduliwa mwanzoni mwa mwezi wa Muharram 1447 (27 Juni 2025) na itaendelea mpaka mwishoni mwa Saffar 1447 (Agosti 2025).
Waraka huu unalenga kwa Waislamu wote jumla, na hasi kwa masheikh, maimamu, ma-ustadhi na taasisi zote za Kiislamu.
Dhamira kuu ya Waraka huu ni kuwataka Waislamu kushikamana na wajibu wa kusimama kidete kupinga na kupambana na ukafiri mambo leo unaoshamiri na kupigiwa debe hususan katika maeneo yafuatayo:
1. ‘DINI MSETO’
Fikra hii inamaanishwa kuleta ukaribu wa kiimani na wasiokuwa Waislamu kwa madai yao kuwa dini zote ni za Mungu.
Malengo ya fikra ya ‘Dini mseto’ ni:
1. Kuufanya Uislamu ni sawa na dini zingine ambazo hazina masuluhisho ya maisha kama uchumi, siasa, jamii, utawala nk. Na madam dini hizo hazina mfumo wa maisha wafuasi wake hawaoni tabu kuwa chini ya mfumo wa kibepari, basi na Waislamu nao waone ni sawa kama wao, na hakuna tatizo lolote juu ya jambo hilo. Bali liwe ni kosa kubwa Muislamu kuwaza kuwa chini ya mfumo wa Kiislamu, na mwenye mawazo kama hayo ahisabiwe kuwa mshari anayetaka kuleta fujo na vurugu, kwa sababu wafuasi wa dini zingine pia nao watataka hilo (la dini zao kutawala). Ilhali wanajisahaulisha kwa makusudi kwamba dini hizo hazina mfumo wa maisha
2. Kuwatia shaka Waislamu dhaifu kuamini dini ya haki sio Uislamu pekee, na kuzalisha mawazo batili kwamba dini za haki zinaweza kuwa nyingi.
3. Kuvunja hisia za udugu wa Kiislamu na badala yake kupandikiza hisia za udugu wa kizalendo, kwani udugu wa kidini utaonekana ni ubaguzi
4. Kumakinisha kwa mfumo tawala wa kikoloni wa kibepari /demokrasia kwa kuzitawala, kuzidhibiti na kuziendesha watakavyo dini zote.
5. Kupata nguvu upagani (ukanushaji Mungu) kwani dini zitapoteza mvuto na ushawishi baada ya kuonekana wafausi wa dini bali hata viongozi wa dini hizo wana buruzwa na wanasiasa wa kibepari. Pia kwa kuonekana viongozi wa dini kwa kudandia kwao demokrasia maana yake hawana suluhisho la matatizo ya raia. Zaidi ya hivyo dini zitadharaulika na badala yake upagani utatamalaki kwa nguvu na kuonekana ndio tatuo la matatizo kwa raia.
Baadhi ya Miito hatari inayotumika katika kampeni ‘Dini mseto’
a. Dini tatu za Uislamu, Uyahudi na Ukiristo ni dini za watoto wa Ibarahim (As). Kwa madai haya batili wanakusudia kuwa sote ni wamoja na dini yetu ni moja
b. Dini sio muhimu kuliko nchi na uzalendo
c. Mungu ndio chanzo cha dini zote basi dini zote ni zake yeye
d. Dini zilete amani na sio vita
e. Vita vya kidini ni vibaya sana na hatari
f. Mamlaka yoyote iwe iwavyo, ni amri ya Mungu
Mbinu zinazotumika katika kufanyia kampeni hii ni vikao vinavyohusisha viongozi au wafuasi wa dini mbali mbali, utawanyaji vipeperushi, kuundwa kamati zinazoitwa za amani ambazo huhusisha viongozi wa dini mbali mbali. Pia huendeshwa semina za amani, michezo inayojumuisha hususan viongozi wa kidini, ziara katika majumba ya ibada, kusihirikiana katika dua za kuombea taifa, kushirikishwa viongozi wasiokua Waislamu katika hafla za Kiislamu nk.
Baadhi ya maeneo ambayo kampeni hii ovu imepiga hatua:
a. Kuwashirikisha katika ibada za dini mchanganyiko kama kuomba dua pamoja.
b. Kujengwa majengo rasmi yenye kujumuisha dini zote. Mathalan, nchini Qatar kuna jengo maalum kwa malengo hayo.
c. Katika hafla mbali mbali za kitaifa, kiserikali hutolewa nafasi maalumu kwa watu wa dini mbali mbali kuomba dua za dini mchanganyiko.
Wadau wakubwa wa ‘Dini mseto’ ni:
1. Marekani na nchi zote za magharibi
2. Vatican na Saudia zenye dhamana kama jicho rasmi la kampeni hiyo
3. Serikali zenye raia wafausi wa dini hasa Uislamu, ukristo na uyahudi
4. Kamati mbali mbali zilizoundwa duniani kote kwa jina la kamati za amani au kamati za maridhiano
5. Vyombo vya habari karibu vyote vikiwemo vya kimataifa kama BBC na DW nk. vyenye dhamana kam jicho rasmi la kampeni hiyo.
6. Wasanii, wanamichezo na baadhi ya watu mashuhuri
Hadaa katika ulinganizi wa ‘Dini Mseto’
Wenye kampeni hii huficha malengo yao na kutanguliza mbele miito ya hadaa na uwongo kama amani, upendo kuishi pamoja, kuvumiliana nk. Jambo ambalo limewachota badhi ya Waislamu na kujiunga katika taasisi za kampeni hii wakidhani wanatetea amani na upendo, kumbe uhakika jukumu la kulinda amani ni vyombo vya dola na matawi yake na sio kamati.
Athari mbaya kufuatia kampeni ya ‘Dini mseto’
a. Baadhi ya Waislamu kuona inafaa kuombewa dua na asiyekuwa Muislamu, ilhali jambo hili linamtoa mtu kwenye Uislamu ikiwa mwenye kulitenda anatenda kwa kujua na kuamini.
b. Baadhi ya Waislamu kukufuru bila kujitambua kwa kuona dini zote ni sawa tu.
c. Baadhi ya Waislamu kuvaa alama za dini nyengine bila kujua kufanya hivyo ni jambo la kufru. Jambo hili ni maarufu kwa wanaoitwa wasanii.
d. Baadhi ya Waislamu kushiriki sherehe za ‘Dini mseto’
e. Kukithiri ndoa baina ya Waislamu na wasiokuwa waislamu. Kwa mfano, binti wa Kiislamu kuolewa na asiyekuwa Muislamu, au kijana wa kiislamu kuoa mwanamke ambaye si Muislamu, na hata akiwa ahlul-kitaab hamuoi kwa taratibu na masharti ya Kiislamu
f. Kukithiri kwa watoto wenye wazazi wa dini mchanganyiko, kwa watoto watakao bahatika kuwa Waislamu kuyumbayumba katika Uislamu wao.
Uislamu uko mbali na ‘Dini Mseto’
Hakuna mashirikiano wala umoja na wasiokuwa Waislamu katika masuala ya kiimani. Hii ni fikra hatari sana na tishio kwa Imani ya Kiislamu ambapo lau Muislamu atashikilia fkra na matendo yake kama kuamni kwamba dini zote za Mungu, dua ya mfuasi wa dini yoyote inakubaliwa nk. Basi ufahamu kama huo utasukuma Waislamu kuritad na kutoka katika Uislamu.
Hapa lazima iwe bayana kinachopingwa na Uislamu sio kuishi pamoja na wasio kuwa Waislamu. Mfano, Waislamu na wakiristo sio kosa kuajiriana, kusaidiana, kutembeleana nk, Bali kinachokatazwa na Uislamu ni uhusiano wa kiimani baina ya Uislamu na dini zingine, na hatari zaidi kampeni ya’Dini mseto’ inajenga mahusiano hayo kwa njia ya hadaa na ujanja ujanja.
2. UPAGANI
Hii ni fikra ya kukanusha uwepo wa Muumba na kukataa dini moja kwa moja. Asili huu ni ukafiri mkongwe katika maisha ya wanadamu lakini upagani wa sasa upo katika kiwango cha kimfumo kutokana na historia ndefu ya dhulma za kanisa ndani ya Ulaya kiasi cha watu kuchukia dini na kutokua na haja nayo na kudiriki kujitumbukiza katika upagani wa kukanusha uwepo wa Muumba na dini.
Mapinduzi ndani ya Ulaya yalikuja chini ya mtazamo wa kuifanya dini kuwa kitu duni (usekula) kutokana tareekh ya matendo ya dhulma ya kanisa kwa wananchi.
Katika kipindi cha zama zinazoitwa za ‘Mwamko’ (enlightment era) ndani Ulaya mwishoni mwa karne ya 17 mpaka karne ya 19, kuliibuka wimbi kubwa la wanafalsafa, wanafikra, wasomi na wanamageuzi waliokuja na fikra za ‘uhuru’ za kidemokrasia ambazo zilileta ‘amsha amsha’ na vuguvugu na kuungwa mkono na wanachi hadi kupelekea mapinduzi ndani ya Ulaya mashuhuri zaidi Ufaransa mwaka 1789 na kumakinishwa na kutabikishwa mfumo wao wa kibepari chini ya aqida yake ‘usekula’ ambayo inaidogosha dini. Jambo hili kwa kiasi kikubwa likazalisha wimbi kubwa la mapagani
Hata hivyo, kama tulivyotaja awali pia kuwa fikra ya ‘Dini mseto’ nayo inachangia kuongeza idadi ya mapagani. Kwa sababu watu watakapoona dini zimebakia kuwa watumwa wa mfumo wa kibepari wataona kuna haja gani ya dini?
Udhaifu wa upagani kwa sababu zifuatazo:
a. Kwa kiasi kikubwa upagani umeibuka kutokana na wimbi la historia ya kanisa ndani ya Ulaya, lakini wanafikra na wanamageuzi wa Ulaya kwa makusudi wakajumuisha chuki zao kwa dini zote, licha ya ukweli kuwa Uislamu haukuhusika na jambo hilo.
b. Inapingana na akili, kuwa ikiwa kuna viumbe lazima kuna Muumba.
c. Inapingana na maumbile ya mwanadamu, kwa kuwa ana ghariza/ hisia za ndani za kutaka kunyenyekea na kuabudu kutokana na udhaifu wake na udhaifu wa mazingira yaliyomzunguuka.
Uislamu tofauti na Ukiristo
Uislamu umejengwa kwa msingi imara (aqida) inayoingia akilini na yenye ufafanuzi juu ya Muumba, sifa zake nk. Pia ni mfumo kamili wa Maisha wenye nidhamu za kijamii, kiuchumi, kisiasa nk ukiwa na utatuzi kamilifu wa matatizo yote yawanadamu.
Uislamu upo kinyume na ukiristo ambao umejengwa juu ya:
• Mawazo ya watu
• Msingi wa Itikadi kuwa haueleweki
• Hauna mafunzo yanayoharamisha unyonyaji, ukoloni nk.
• Kutumika katika kueneza fikra chafu: ushoga, nk
• Hauna masuluhisho ya matatizo ya binadamu
3. DINI ZA MABABU (JADI)
Imani za kijadi wafuasi wake hudai kutaka watu warudi kwenye imani za asili za mababu zao (dini za kiafrika)
Lakini cha kushangaza waumini hao wa dini za mababu hawana uwezo wa kuthibitisha madai yao kwamba imani zao hizo ni sahihi na zinamfaa mwanadamu, hasa mwanadamu anayetaka mabadiliko kutoka hali duni kwenda katika hali nzuri ya ustawi wa maisha yake hapa duniani.
Madai makubwa ya waumini wa dini za kijadi yamesimama kwenye mtizamo kuwa:
a. Kufuata Uislamu ni kudharau mababu na mila za mababu.
b. Wanadai kuwa Uislamu ni imani iliyoletewa na waarabu na haituhusu sisi.
c. Pia wanadai kuwa kabla ya Uislamu Afrika walikuwa wanaomba kupitia mizimu na kukubaliwa
d. Wanadai kabla ya Uislamu Afrika ilikuwa na maendeleo.
e. Wanadai kuwa Uislamu umefuta hata majina ya asili ya waafrika
f. Wanadai kuwa Uislamu umeleta vita, vurugu, utumwa, ukoloni nk.
Mlengwa mkuu ni Uislamu.
Hoja za wafuasi wa dini za kiafrika/mizimu, dini mseto, upagani zote ukizizingatia kwa makini japo katika madai yao hayo hutaja na kuzungumzia dini zote kama ukristo nk. Lakini shabaha yao kuu ni Uislamu. Chuki zao dhidi ya Uislamu zimewafanya kuacha kutofautisha kwa makusudi kama masekula wa Ulaya (ambao hawa ni tawi lao) baina ya Uislamu na dini nyingine, licha ya kujua kuwa misingi, miiko na maadili ya Uislamu ni tofauti na dini nyingine.
Udhaifu wa hoja wa waabudu dini za kijadi/kiafrika
a. Wafuasi wa dini za jadi wamechanganyikiwa kiasi cha kushindwa kuweka wazi Uafrika wanaotetea ni kitu gani? Je ni rangi nyeusi au eneo la bara la Afrika? Kama ni rangi basi kuna watu wenye rangi nyeusi wa asili wapo Arabuni, India, Australia nk. Na kama ni bara, basi bara la Afrika kuna waarabu wengi na wanazungumza kiarabu kama Misri, Sudan, Tunisia, Morocco nk. Hivyo, mpaka hapa imekua madai yao haya hayana mashiko na ni wazi hawajui nini wanapinga na nini wanataka
b. Madai yao ya Uislamu kudharau mababu. Uislamu umekuja kuwaweka wanadamu wote sawa, waarabu na wasiokuwa waarabu. Mababu wote wamepewa heshima sawa, na mababu wote ambao wameacha mafundisho sahihi ya Muumba hao watakua wamejiweka katika kundi duni wao wenyewe. Uislamu haujainua mababu wa kiarabu na kuwatupa mababu wa kiafrika, kwani tunaona kuwa miongoni mwa mababu wakubwa wa kiarabu kama Amru Ibn Hisham (Aabu Jahl), yeye sio tu alikuwa katika mababu wa kiarabu bali alikuwa kiongozi wa waarabu (makureishi) na mtu anayeheshimika sana, Uislamu ulimdhalilisha kwa ukafiri wake. Bila ya kusahau mababu wengine wa kiarabu kama Abu Lahab, Walid Ibn Mughira nk. ambao Uislamu uliwazungumza kwa ukali kaisi cha kutangaza maangamizi ya baadhi yao ndani ya kitabu chake cha Quran.Kwa upande mwingine, Uislamu ukawainua na kuwaheshimisha mababu kutoka jamii ya kiafrika na jamii nyengine kama Bilal Ibn Rabah, Salman Al-Fursi nk. Kwahiyo, madai haya ya watu wa dini za kiafrika hayana mashiko wala msingi wowote.
c. Madai kwamba Uislamu ni dini ya “kuletewa”, kitu kinacholetwa ni kutoka kwa watu wengine na kikawa hakina maana. Lakini imani ya Kiislamu ni kutoka kwa Allah (SWT) na Yeye (Allah) ndiye Muumbaji wa wanadamu wote. Ama dini ya Uislamu kuteremshwa kwa kuanzia kwa mtu fulani, hilo ni suala la kutarajiwa na bahati hii ikaangukia kwa Muhammad bin Abdillah (SAAW) ambaye yeye alikuwa muarabu, lakini ujumbe aliopewa haukuwa kwa ajili ya waarabu tu, bali kwa wanadamu wote:
وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا رَحْمَةً لِّلْعَالَمِينَ
“Wala hatukukutuma (ewe Muhammad) ila kuwa ni Rehma kwa viumbe wote” (An-biyaa :107)
d. Madai kuwa kabla ya Uislamu na dini nyingine watu wa Afrika tulikuwa tunaomba katika imani zetu za asili na kujbiwa. Haya ni madai ya kuchekesha sana, ikiwa walinganizi wa imani za kiafrika hawakubali dini za wageni sasa, kwanini leo hawaombi mizimu yao na kujibiwa ili wakoloni waondoke na umasikini uondoke Afrika? Uhakika ni kuwa mizimu haina uwezo wa kujibu chochote, bali mawazo ya mizimu ni uchache wa kufikiri.
إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ
“Hawafuati ila dhana tu, wala hawakuwa ila wanatabiri tu (bila ujuzi wa hakika”(An-aam :116)
e. Madai ya dini kudhoofisha maendeleo ni madai ambayo hayajazingatia uhalisia, pia kwanini hawasemi kuwa waliokuja kupora maendeleo ya Afrika mpaka leo ni mabepari wanademokrasia. Waumini wa mizimu na dini za jadi wanapoacha kutaja waporaji halisi wa Afrika na kukimbilia dini ni wazi wanatumiwa na hao waporaji, wawe wanajua au hawajui. Je katika hii Afrika dini gani ipo ikulu inatawala kwa sheria za dini? Ili iwe hoja kwamba dini hiyo, imewafanya watu wa nchi hiyo kuwa maskini. Lakini ukweli na uhalisia watu wanatawaliwa na sharia za kibepari za kisekula
f. Madai kuwa dini au Uislamu umekuja kufuta majina yetu ya asili. Ukweli ni kuwa Uislamu haujalazimisha mtu kubadili jina anaposilimu bali ni khiyari. Wasichofahamu hawa wapinga dini ni kwamba waarabu wapo Afrika kwa wingi na kwa karne na karne. Uislamu unalazimisha kubadilisha jina kama litakuwa na maana mbaya haijalishi mwenye jina hilo ni mwarabu, mwafrika, mchina, muhindi, mzungu nk. lakini ikiwa mtu jina lake lina maana nzuri halazimishwi kubadili jina.
g. Kudai kuwa dini zimeleta vita na machafuko hii pia si hoja madhubuti. Kwa bahati mbaya waabudu mizimu hawataji hata vita moja au mfano wa vurugu hizo ambazo Uislamu umeleta. Mfano, leo vita ya Congo, Ukraine na Urusi, Msumbiji, Angola, Vita vya Kwanza na vya Pili vya Dunia nk. Je sababu yake ilikuwa dini? Bali wapagani leo hii ndio wanaongoza dunia, na hata kama mtawala atakuwa si mpagani basi atatawalisha fikra na sheria za kipagani na sio za dini yake.
h. Madai kuwa dini kuleta ukoloni na utumwa. Dini ya Kiislamu iliingia Afrika karne ya saba na hakukutokea utumwa wala ukoloni mpaka karne ya 18 walipokuja wakoloni mapagani baada ya kulipindua Kanisa huko Ulaya na kutangaza upagani wa kibepari. Na kama walitumia kanisa kusaidia mambo ya utumwa, basi hilo litakuwa jambo la kanisa sio Uislamu. Na haifai kuhusisha dini katika muktadha wa utumwa, bali uadilifu ni kutaja muhusika moja kwa moja nae ni dini ya ukiristo
Hoja hizi za kupinga dini zinazolenga kupinga Uislamu hazina nafasi kwa upande wa Uislamu, bali zinaweza kuwa nafasi kwa upande wa dini nyingine, kwani Uislamu umetakasika na udhaifu wote uliopo katika dini nyingine.
Wafuasi wa dini hizi za jadi ambazo hazina hoja waachane mara moja na dini ambayo inashindwa hata kujitetea na waje katika Uislamu, dini ya haki inayokinaisha akili na kuwafikiana na maumbile ya mwanadamu.
Mwito kwa Waislamu,
Kama wadau wa Uislamu ni wajibu kuulinda, kuutetea na kuueneza Uislamu kwa mbinu zote ambazo ni halali kwa mujibu wa sheria za Kiislamu. Na ni kosa kubwa na dhimma nzito mbele ya Allah SWT kunyamazia uvamizi dhidi ya suala nyeti la aqida. Basi jee vipi ukiwa mshiriki katika kukuza moja ya ajenda hizi za kikafiri kama ‘Dini mseto’ Upagani au Dini za mababu?
Yafaa Umma wa Kiislamu ukumbuke kwamba vita baina ya haki na batili ni endelevu kinachobadilika ni mbinu na mipango kwa mujibu wa zama, muda, eneo nk. Kama Allah Taala alivyotaja ndani ya Quran Tukufu:
بل نقذف بالحق على الباطل فيدمغه فإذا هو زاهق
“Bali tunailembea haki kwenye batili na ikaiangamiza na tahamaki ikaipoteza” ((An-biyaa :18)
Na jukumu la kubomoa batil linaangukia mabegani mwa waliobeba haki ambao ni Waislamu. Na wajibu zaidi huangukia kwa wasomi au wanaojishughulisha na kuhudumia Uislamu, kama taasisi za kidini nk.
Vita hii haijawahi kusimama tangu zama za Mtume SAAW.
• Ndani ya Makka Makuraishi walisimama kidete kuzuiya Uislamu usichipuke kisha kutaka kuzuiya dola ya Kiislamu isisimame. Mbinu yao ya awali ilikuwa kudharau, kisha propaganda, mateso kwa Waislamu nk.
• Ndani ya Madina, mayahudi, wanafiki, waarabu na washirikina walisimama kidete kutaka kung’oa dola ya Kiislamu na kuzuiya kupanuka kwa Uislamu na dola ya Kiislamu. Walitumia mapambano ya kifikra, unafiki, fitna nk. Na walipo shindwa wakaungana na waraabu washirika katika vita. Mfano, Vita vya Ahzaab
• Kisha zama za Khilafah Rashidah, vita ilikuwa kufarikisha Umma wa Kiislamu, kudhoofisha dola ya Kiislamu na kuiangusha. Maadui walikuwa ni wanafiki wapya waliosilimu kinafiki kutoka miji nje ya Bara Arabu. Walichofanikiwa tu ni kuuwa watawala watatu wa Kiislamu Omar, Othman na Ally (ra)
• Kisha zama za Ummawiya na Abassiya, vita dhidi ya Uislamu ilikuwa ni kuharibu fikra na fahamu sahihi za Kiislamu kwa kutunga Hadithi za uongo na kuzua mijadala kwamba aya za Quran zinagongana nk. Na maadui walikuwa mazandiki
• Kisha zikafutia na zama za uadui wa Vita vya Msalaba na Wamongoli. Wao lengo lao ilikuwa ni kuangusha dola ya Kiislamu na kuwafukuza kabisa Waislamu katika miji yote waliyoifungua. Na mbinu yao ilikuwa ni vita na uharibifu. Hali ikaendelea hivyo mpaka kufikia zama za Khilafah Uthmaniya, na hasa karne ya 18 mpaka 19.
• Vita vya karne 18 mpaka 19 ilikuwa na malengo kuangusha dola ya Kiislamu na adui alikuwa nchi za Ulaya hususan Uingereza. Na hatimaye wakafanikiwa. Mbinu yao kubwa ilikuwa vita vya kifikra, kujitenga miji ya Kiislamu kunako Khilafah ya Uthmaniya, miito ya uzalendo na ubaguzi, kuunda vibaraka katika ardhi za Waislamu nk.
• Ama vita vya karne ya 20, shabaha ya makafiri ni kuzuiya kurudi tena Uislamu kama nguvu ya kutawala dunia kwa kuharibu fikra sahihi za Kiislamu.
Kufikia lengo hilo makafiri wamepanga mambo mengi. Haya ani mfano tu:
1. Kuharibu na kuzikoroga fikra za Umma wa Kiislamu kama:
a. Fikra ya uzalendo ili kuzuiya umoja wa Umma
b. Fikra za kutenganisha dini na maisha, yaani kuutenga Uislamu na utawala
c. Kupiga vita Uislamu wa kisiasa na kuunga mkono Uislamu wa kiroho tu, yaani kuufanya Uislamu kama ukristo
d. Kuasisi harakati za kuungana na wanasiasa katika siasa zao za kidemokrasia.
e. Kuasisi harakati zenye kupambana na Waislamu tu, hasa Waislamu wenye mawazo ya kutaka kurudisha nguvu za Waislamu duniani.
2. Vita vinavyoitwa vya Ugaidi
a. Kuasisiwa kwa makundi ya kigaidi ili kuleta machafuko na kunasibishwa Uislamu na machafuko hayo.
b. Kutumika ugaidi kama bakora ya kufunga midomo Waislamu kuzungumza Uislamu kama mfumo wenye kukusanya roho na mada, imani na maisha, ibada na siasa nk. Hatimae Waislamu wamekuwa wahudumu wa siasa za kidemokrasia, kwani siasa ni maisha huwezi kuiepuka, ikiwa sio ya Kiislamu utashika isiyo ya Kiislamu.
c. Kufanywa ugaidi ni kibali cha kudhulumia Waislamu, yeyote awae, ana kosa au hana kosa, na wengine kuogopa kumtetea.
d. Kudhibitiwa kwa taasisi za Kiislamu, shule hata misikiti kwa kutumia ya tishio la ugaidi
e. Kuvunja ari ya vijana wa Kiislamu kuhudumia dini yao, na kuona afadhali kujiingiza kwenye mambo ya kipuuzi kama michezo, kamari nk.
Wajibu wa kila Mbeba da’awa na Waislamu jumla.
Ni wajibu kwa kila mbeba da’awa kujifunga kibwebwe katika kulinda na kutetea aqida ya Kiislamu, kwani kukaa kimya au kushughulika na mambo madogo madogo au mambo ya ikhtilafaat tu na hali Umma unapotezewa aqida yao ni dhimma kubwa sana Siku ya Qiyama. Na kwa wale waliotumbukia kwenye mtego wa ‘Dini mseto’ tunawapa nasaha wajitoe ili iwe salama kwao Siku ya Qiyama.
Watumishi wa Uislamu na Waislamu jumla wasichoke kujadiliana na wafuasi wa fikra hizo za hatari kwa njia ya kistaarabu, hoja na busara.
Kubwa na nyeti zaidi kwa Waislamu ni kushiriki katika mchakato wa kurejesha tena dola ya Kiislamu ya Khilafah Rashidah ili ije kulinda kikweli aqida ya Kiislamu, na kuuokoa ubinadamu na dini na fikra za kuchanganyikiwa ambazo leo ubepari unazipigia debe na kuzidhamini.
Mwisho
Umetolewa na Wanaharakati wa 𝐇𝐢𝐳𝐛 𝐮𝐭 𝐓𝐚𝐡𝐫𝐢𝐫 𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚
6 Safar 1447 Hijria / 31 Julai 2025 Miladi
“Kataa Dini Mseto, Ukristo, Upagani, Mizimu – baki na Uislamu”
Maoni hayajaruhusiwa.