Tangazo La Trump La Kuipora Gaza Na Kufukuza Wakaazi Wake

بسم الله الرحمن الرحيم

 

Raisi Trump ametangaza nia ya kuichukua Gazza na kuigeuza kuwa Riviera ya Mashariki ya kati. Yaani kuigeuza Gaza iwe kama mwambao huo (Riviera) wa Ufaransa na Italya ambao ni mashuhuri kwa utalii. Mpango huo wa Trump utawezekana kwa kuwatimua Waislamu wa Palestina kwa kuwapeleka katika nchi za jirani na hawatokuwa na haki ya kurejea tena.
Baada ya mauaji ya maangamizi na maumivu makubwa ya watu wa Gaza kwa kufa mashahidi watu wasiopungua 50,000, maangamizi yaliyozidi hata vita vya kwanza na vya pili vya dunia. Maangamizi yaliofanywa na Israil na washirika kwa silaha na kila msaada wa Marekani ukiwemo wa kijeshi, kisiasa, kidiplomasia nk. Trump kwa ujasiri kabisa tena bila ya kusitasita ametangaza lengo lake hilo mbele ya ulimwengu na mbele ya Waziri mkuu wa Israil ambaye alikuwa akitabasamu kwa kauli hiyo.
Tangazo hilo halitushangazi bali ni nyongeza ya dhihirisho la hali ya udhaifu iliyofikishwa kwa Umma na vibaraka katika ulimwengu wa Kiislamu. Trump amefikia kutoa kauli hiyo na kuwa na malengo hayo kwa sababu :
a. Ameona wazi namna watu wa Gaza walivyotelekezwa na vibaraka wa nchi za Waislamu
b. Ameona wazi namna vibaraka walivyoisaidia Israil mpaka kuwapelekea vyakula baada ya kuzuiliwa kutumia bahari ya Red sea
c. Ameona namna majeshi ya ulimwengu wa Kiislamu namna yalivyokuwa yamelala usingizi wa mauti.
d. Ameona namna pia masheikh walio wengi ambao miongoni wana sauti kali na wenye kusikika katika mambo mengine ya kinafsia na kibinafsi namna walivyokuwa kimya cha mfu kwa suala la mauaji ya maangamizi ya Gaza.
Kwa hivyo, kitarajiwe nini kwa Trump na wengine kama yeye? kamwe hatosita kutoa kauli au kuwa na ajenda yoyote aitakayo katika ulimwengu wa Kiislamu, kwa kuwa wenyewe (vibaraka) wenye nguvu wamelala kama sio kufa kamwe.
Kauli hii ya Trump inafedhehi na kuonesha yafuatayo:
1.Inafedhehi zaidi dhana ya mfumo wa kibepari ya kutegemea ubeberu na kujitanua kwa mabavu na kwa gharama ya kufukuza na kupora ardhi za watu. Na jambo hili sio geni kwa Marekani na nchi nyengine za kimagharibi, bali linawekwa wazi zaidi na kauli kama hii.
2. Inafedhehi uovu wa mfumo wa kibepari na siasa yake ya kidemokrasia. Na wale wanaopigia debe mfumo wa kidemokrasia na haki za binadamu, wanaona wazi namna kiongozi wa dola ‘kinara’ ya demokrasia anavyotaka kupora eneo lenye wakaazi wake halali na kuwavurumiza mbali kwa ajili tu ya malengo ya kibiashara na maslahi ya kimfumo. Hapa tukumbushe kwamba kila mara tumekuwa tukisema kwa kinywa kipana kwamba mfumo wa kibepari ni wa maslahi tu hauna utu wala hauamini kufanya mambo kwa misingi ya haki na sharia. Tena hawaamini hata taratibu walizotunga wao wenyewe achilia mbali za Mungu.
3. Inefedhehi dhana ya uwongo ya sheria za kimataifa. Dhana hiyo ni debe tupu (empty slogan) isiyokuwa na ukweli wowote. Mataifa makubwa hususan Marekani huzitumia sharia hizo pale tu zinapowafikiana na maslahi yao, na pale zinapopingana huachilia mbali. Hatua hii ya Trump ni dhidi ya sheria zao wanazoziita za kimataifa, bali ni sehemu ya mauwaji ya halaiki. Trump baada ya kauli yake hiyo ya kuipora Gaza na kuwafukuza wakaazi wake, aliulizwa na mwandishi wa habari wa Marekani. “Unaongelea kuichukua ardhi halali ya watu wenye mamlaka nayo. Unataka kufanya hivyo kwa mamlaka gani ya kisheria? Na jee unazungumzia kuichukua milele?
Trump akajibu: “tunataka kuichukuwa na kuwa nayo katika umiliki wetu kwa muda mrefu”
4. Inaonesha wazi zaidi kuwa makafiri ni mila moja, na ni wenye kusaidiana wao kwa wao. Trump alifanya usitishaji wa vita kijanja ili kuikoa kambi yao ya kijeshi inayoitwa Israil ambayo ilikuwa imekwama katika ndoana ikitoja damu kila upande. Israil ikisumbuka katika medani ya kivita, lakini pia kisiasa, kutokana na upinzani wao ndani ya serikali, upinzani wa jamii yao hususan wazazi wa mateka, bali pia kuvurugika haiba yao kimataifa.
Kwa hivyo, mpango wa Trump kusitisha mapigano Gaza japo kwa muda sio kwa malengo ya amani wala utu, na wala sio wa kuaminika. Ndio maana karibuni akasema hana hakika kwamba usitishaji huo kama utadumu.
Aidha, tunamuona Trump huyu huyu amewaondolea vikwazo walowezi wa kiyahudi wanaotesa na kuuwa Waislamu katika Ukingo wa Magharibi (Westbank) ndani ya Palestina ambako kunaendelea dhulma, mateso na mauwaji makubwa. Bila ya kutaja kuwa Trump ameiwekea vikwazo Mahkama ya Jinai ya Kimataifa (ICC) kwa kuwa imetoa waraka wa kukamatwa viongozi wa Israel nk.
Haya yote anayafanya Trump kuwakingia kifua Israil. Wakati Trump akitenda hayo kumuunga mkono Israil wazi wazi, na vibaraka katika ulimwengu wa Kiislamu sio kuwa wataunga mkono Umma dhidi ya mayahudi, bali nao pia hujipendekeza huko huko upande wa Marekani na mayahudi bila ya kuona haya wala vibaya.
Umma wa Kiislamu uchukue msimamo gani na kubeba majukumu gani?:
Kufuatia qadhii hii Umma unapaswa usimamae na msimamo ufuatao:
1. Kuyataka na kutoa mwito kwa majeshi katika ulimwengu wa Kiislamu kuchukua jukumu lao la asili la kuunusuru Umma wa Kiislamu kwa kuwaweka pembeni vibaraka na kulikomboa eneo lote la Palestina kutoka katika mikono ya mazayuni.
Kwa kuwa kwa kadiri siku zinavyokwenda njama, vitimbwi na hila za makafiri zinazidi. Mashaka yanayoendelea kuwafika ndugu zetu ndani ya Palestina, mwazo Gaza, na sasa Ukingo wa Magharibi ni makubwa wasidhani yatapungua.
2. Kuwataka wenye ushawishi katika nchi kubwa za Kiislamu (hususan jeshini) kutoa nusra kwa Umma ili kurejesha tena dola ya Kiislamu ya Khilafah, inayopaswa kuanza katika ulimwengu wa Kiislamu. Dola hiyo ndio pekee yenye uwezo, nguvu na ikhlasi ya kulinda Umma na kuzuiya maadui wetu kivitendo.
3. Kufedhehi dhana ya demokrasia na sheria za kimataifa kuwa ni uwongo tu wa kuingilia kati na kunyonyea nchi changa na kuzikandamiza.
4. Kuwa na hali ya kujiamini na kusimama kidete juu ya msimamo huo kwamba hata kama vibaraka wako na makafiri, bado Umma unasimama thabiti. Kwa hivyo, mipango ya Trump itashindwa kama walivyoshindwa Gaza, Iraq, Afghanistan nk. Na mwisho dola yav Khilafah itarudi wakitaka wasitake. Kwa kuwa ushindi wa Umma ni jambo lililopo kwenye “nass”
5. Umma wa Kiislamu mashariki na magharibi hata katika maeneo yetu ambayo hayana sifa ya kuwa sehemu ya kuasisi dola ya Kiislamu, wanapaswa kupaza sauti dhidi ya dhulma na mipango ya makafiri kwa Umma wetu, kama hili la Trump na mengineyo.
Pia kuwataka wasiokuwa Waislamu katika wapenda haki watafakari kwa kina juu ya uovu wa mfumo wa kibepari na namna ambavyo unaleta mabalaa, sio tu kwa Waislamu bali kwa wanadamu kwa jumla.
Risala ya Wiki No. 200
19 Shaaban 1446 Hijri | 18 Februari 2025 Miladi
Afisi Ya Habari – Hizb Ut Tahrir Tanzania

Maoni hayajaruhusiwa.