Kamati ya Mawasiliano ya Hizb Ut Tahrir Yamtembelea Mwanahistoria Nguli Nchini Tanzania Mohammed Saidi
بسم الله الرحمن الرحيم
Juzi Jumatano tarehe 20/1/2021 Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir Tanzania Sheikh Mussa Kileo nikiambatana na Mjumbe wa Kamati hiyo, Ibrahim Kachema na Mjumbe wa Majlis Wilaya Suleiman Ame (Ticha Sule) tulifanya ziara ya kumtembelea Mwanahistoria nguli nchini Tanzania ndugu Mohd Saidi nyumbani kwake Magomeni Mapipa, Dar es Salaam.
Mohammed Said ni mwanahistoria mahiri anayejikita katika kuandika vitabu vya kuibua na kusahihisha mchango wa Waislamu nchini Tanzania
Katika kubadilishana nae mawazo, Sheikh Mussa Kileo nilikumbusha namna harakati za Kiislamu zinavyohitaji muundo na njia sahihi ili kuweza kuleta ufanisi kinyume na hali ilivyo sasa.
Aidha, ujumbe huo katika kubadilishana mawazo zaidi na Mwanahistoria Mohammed Said ulifafanua kuwa kadhia za Waislamu Tanzania ndio kadhia ya Waislamu wote ulimwenguni. Kwa kuwa Waislamu ni Umma mmoja
Mwisho, ujumbe ulikumbusha kuwepo haja ya Waislamu kutafakari kwa upana hali ya Umma wa Kiislamu na namna ya kufanya ili kuondokana na hali duni iliyopo kwa mujibu wa muongozo wa Qurani na Sunna
Kwa upande wake Mwanahistoria Mohamed Said ameonyesha kufurahishwa sana na ziara hiyo na akadokeza kuwa amekuwa akiijuwa Hizb ut-Tahrir kwa muda mrefu.
Kabla ya kuagana Sheikh Mussa Kileo nilimkabidhi ndugu Mohammed Said vitabu kadhaa vya Hizb ut Tahrir ikiwemo ‘ ‘Utangulizi juu ya Hizb ut Tahrir’ ‘Thinking’ na ‘Warm Call’
Sheikh Mussa Kileo
Mwenyekiti Kamati ya Mawasiliano
Hizb ut Tahrir Tanzania
+255 658 393 995
Maoni hayajaruhusiwa.