Mfumo wa Kisekula Hauwezi Kupambana na Virusi vya Korona
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mfumo wa kibepari uliojengwa juu ya itikadi ya kisekula unafichuliwa na janga la virusi vya Korona. Wanasiasa, wanauchumi na wakereketwa katika vyombo vya habari wanasukumwa kutoa suluhisho za kuaminika huku wakidumisha kisingizio cha utunzaji wa watu.
Urasilimali daima huwajali matajiri na wenye madaraka pekee, huku watu wengine wa kawaida wakitumika kikamilifu kutoa huduma kwa manufaa yao ya kibinafsi. Siasa katika jamii ya kisekula ni huhusika kwa uchache katika kutunza watu, na huhusika zaidi katika kutunza maslahi ya mabwenyenye, huku wakijifanya kujali kila mtu mwengine.
Huku kirusi chenyewe kikiwa hakibagui kati ya matajiri na maskini, huduma ya afya iliyopo yabagua. Zaidi ya hayo, sera za kusimamia kuenea na matibabu ya ugonjwa huu zinaweza ima kuzingatia afya ya watu, au uchumi. Wanasiasa wa kisekula leo wanaweka wazi kipi wanachokijali zaidi. Hakika, trillioni za dolari zinawekwa kuzuia masoko yasianguke, huku sehemu ndogo pekee ya hizo ni kwa ajili ya huduma ya matibabu iliyo ongezeka.
Fikra ya Malthus [1] kwa mara nyengine tena inanyanyua kichwa chake kibaya, pamoja na manufaa ya kuwaangamiza wazee na wahitaji yakitangazwa waziwazi katika vyombo vikuu vya habari. Kwa Warasilimali, wasiwasi wa jumla ya shida za wanadamu huzingatiwa kwa uchache.
Chumi za kirasilimali za Wamagharibi zimekuwa zikiyumbayumba ukingoni mwa kuanguka kwa muda sasa, lakini watetezi wa kisekula, kwa kutapatapa hutia kiraka vazi lililo chakaa, isije watu wa ulimwengu wakazikataa kwa pamoja, wanaonekana kupata kisingizio kuficha dosari za sera zao, kupitiliza kwao, na mfumo wenyewe.
Uislamu haufadhilishi maslahi ya matajiri juu ya mahitaji ya watu. Maana halisi ya siasa, ambayo ni kusimamia mambo ya watu, inaweza kupatikana pekee na Khalifa ambaye anatawala kwa sheria ya Kiislamu, ambayo Mwenyezi Mungu akipenda ulimwengu karibuni utaishuhudia kwa kurudi kwa Khilafah kwa njia ya utume.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ameripotiwa akisema:
«أَلاَ كُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ فَالأَمِيرُ الَّذِى عَلَى النَّاسِ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ»
“Kila mmoja wenu ni mchungaji na kila mmoja wenu ataulizwa juu ya aliyo yachunga, Kiongozi anaye tawala juu ya watu ni mchungaji na ataulizwa juu ya raia wake.”
Yahya Nisbet
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Uingereza
[1] Thomas Malthus alikuwa ni mwanauchumi wa Kingereza aliye sema kuwa hakuna chakula cha kutosha kwa kuongezeka idadi ya watu duniani
#Covid19
#Korona
Maoni hayajaruhusiwa.