Kampeni ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir: “Janga la Korona Baina ya Uislamu na Urasilimali!”
بسم الله الرحمن الرحيم
Virusi vya korona (Covid-19) vimeenea ulimwenguni mashariki na magharibi, vimesimamisha mambo ya kimaisha ya kila siku, na watu wenyewe wametii kujifungia ndani majumbani mwao kwa hofu ya maambukizi, swala za Ijumaa na jamaa zimesimama, hata Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu (Msikiti wa Makkah) na msikiti wa Mtume wake (saw) iko mitupu bila ya wafanyaji Umra wala wanaoswali, hali ambayo hawezi akaifikiri mchambuzi mahiri na mtafiti bora duniani! Yote haya ili ithibiti kauli ya Mola wetu mwenye izza na utukufu: “Na mwanadamu ameumbwa kuwa ni dhaifu”
Hakika ya walimwengu wote wanakabiliana na janga hili na wana haja kubwa sana ya uangalizi wa uhakika kutoka kwa Dola yenye kushughulikia kikweli mambo ya watu, ambao wana haja ya Dola yenye kushughulikia ubinadamu na sio mada na faida tu. Binadamu leo anahitaji Khalifah atakaye yachukulia maradhi kuwa ni kadhia ya kibinadamu awali kabisa bila ya kuangalia dini zao, madhehebu yao na asili zao. Na sio kadhia ya kiuchumi yenye manufaa yenye kutegemea katika utatuzi wake upeo wa manufaa ya nchi binafsi, kama ilivyotokea katika nadharia ya “Kinga ya Watu” ambayo Uingereza ilitaka kuifanyia kazi katika janga hili la korona.
Dunia leo inahitaji uongozi mpya wa kiulimwengu ili kuwatoa watu kwenye kiza na kuwapeleka kwenye nuru na kutoka katika jeuri ya usekula na urasilimali wake na kuwapeleka kwenye uadilifu wa Uislamu na Dola yake (Khilafah ya Uongofu ya pili kwa njia ya Utume). Na hakika muda wake umefika kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu zisizoshindwa na Mwenye kuhimidiwa, na hasa baada ya kupita miaka 99 tangu kufutwa kwa nidhamu ya Khilafah ambayo ilikuwa ikitumiwa na Dola ya Uthmaniyya, na hilo sio zito kwa Mwenyezi Mungu. “Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kutimiza jambo lake, hakika Mwenyezi Mungu amejaalia kila kitu kwa kadari maalumu”.
Na katika ukurasa huu wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir tutafanya kampeni pana kwa ajili ya kila kinachochapishwa na Hizb ut Tahrir ulimwenguni kuhusiana na janga la virusi vya korona (Covid-19). Na Mwenyezi Mungu (swt) ndiye Mwenye kuwafikisha, Mlinzi mzuri na Mwenye nusra nzuri.
Ijumaa, 3 Shaaban 1441 H sawia na 27 Machi 2020 M
Maoni hayajaruhusiwa.