Jana ilikuwa, Shuafat na Silwan, Leo ni Wadi Al-Homs, na Orodha inaendelea…!!
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
(Imetafsiriwa)
“Vyombo vya habari viliripoti picha za wanawake na watoto wakipiga mayowe wakati majeshi ya uvamizi yalipofurusha familia za Wapalestina kutoka majumbani mwao ili kubomoa majengo kadhaa katika eneo la Wadi al-Homs ambalo liko chini ya udhibiti wa Mamlaka ya Palestina pembezoni mwa Jerusalem iliyovamiwa wakidai kwamba walikuwa karibu na ukuta wa ubaguzi wa rangi.”
Umbile la Kiyahudi linaendeleza ukandamizaji na uasi wake dhidi ya Waislamu na kile kinachoitwa sheria za kimataifa kwa kupora ardhi zaidi, kuvunja nyumba na kuwahamisha watu wake ndani ya Palestina yote iliyovamiwa hususan ndani ya mji wa Jerusalem na viunga vyake, ili kuweza kupanua udhibiti wa maeneo mengine. Inajaribu kuondosha kila kitu ambacho kinaweka kikwazo dhidi ya utekelezaji wa mpango huu kama ilivyotokea ndani ya Shuafat, Beit Hanina, Al-Ram na eneo la Silwan ambalo wanaliita “Bonde Takatifu” ambalo liko wazi zaidi kwa Uyahudi na ufurushwaji kwani nyumba 657 zinatarajiwa kufanywa za Kiyahudi kwa kisingizio cha kuwa hazina leseni. Sasa wanataka kuwaondosha watu kutoka katika eneo la Wadi al-Homs ambalo liko karibu na Ukuta wa Ubaguzi wa Rangi na ambao uko chini ya udhibiti wa Mamlaka ya Palestina kwa sababu ni kikwazo cha upanuzi wa makazi. Ili tangazwa siku chache zilizopita kwamba Mchoro wa Kahawia (gari moshi nyepesi) ambao utazinduliwa kutoka wilaya ya Gilo na kupitia maeneo ya Sur Baher, Mukher, Silwan, Bab El Amud na kuishia Kalandia ambayo yote yataunganishwa na kuharibu ardhi zote na majumba yaliyopo njiani inapopitia.
Kama kawaida, lau kama ambaye wamesamehewa kosa la kuitelekeza Palestina na Jerusalem, maafisa wa Mamlaka ya Palestina na harakakati nyingi zimekemea vitendo hivyo na kuvitaja kuwa ni uhalifu wa kivita na utakaso wa kikabila, wakiitaka ile inayoitwa jamii ya kimataifa, taasisi za kimataifa na mashirika ya haki za kibinadamu kuweza kutatua uondoshwaji wa lazima ambao unatekelezwa kwa uungwaji mkono na utawala wa Marekani. Rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, ametuma barua kwa mashirika ya kimataifa ya haki za kibinadamu na diplomasia ili kuwataarifu kuhusu maendeleo hayo hatari yanayolenga kuwang’oa Wapalestina kutoka katika ardhi zao na kupendekeza kuwa wasimame na raia ambao nyumba zao zimelengwa. Alitaka ushikamano na kupambana na hatari ya makazi ambayo inatokea katika maeneo ya Palestina, lau kama ambaye alikuwa na wasiwasi na kuyajali!!
Enyi Waislamu:
Hichi ni kibla chenu Quds (Jerusalem), na hii ni Aqsa yenu; zote zimo katika hatari ya kudumu ya Uyahudi na majaribio ya kuharibu sifa zake za Kiislamu. Watu hawa ambao hawakujihami wanafurushwa kwa baraka ya Amerika na Magharibi, wakiwa na hakika kuwa hakuna katika watawala Ruwaibidhat watakao wapinga lakini kinyume chake wanabariki hatua hizo kama walivyo bariki Makubaliano ya Karne ili kuwaridhisha Mayahudi na Amerika na kuhifadhi mamlaka na viti vyao…
Enyi Watu wa Palestina na Jerusalem Tukufu:
Hakuna miongoni mwenu mwenye akili timamu? Kivipi bado munafanya subra kuhusiana na njama na utepetevu huu?! Mwasubiri nini zaidi? Hamuja choshwa na maneno matupu na urongo na kauli za vibaraka watiifu wa Mamlaka ya Palestina, wamiliki wa shirika la usalama, ilhali iliidhinisha na kutia saini vigezo vyote vya makubaliano na miradi ambayo ndio iliyopelekea kwa haya yanayotokea ya kuvunjwa kwa nyumba zenu, kuporwa kwa ardhi zenu na kufurushwa kwenu!
Ukombozi wa Jerusalem, al-Aqsa na Palestina hautapatikana kwa kuzielekea mahakama za kimataifa, ambazo kiasili ni washirika, wala fidia ya pesa ambazo mutapewa kwa baadhi ya waliyowafika. Sio kupitia makubaliano ya aibu wala nyinyi kusimama nyuma ya wale wanaoweka mikono yao katika mikono ya adui wenu, wakiamkiana na kupanga njama nao. Bali ni kupitia kuikata mikono hii na vichwa ambavyo vinapanga kuifanya Palestina kuwa ya Kiyahudi, kuivunja al-Aqsa na kuasisi linalodaiwa kuwa ni hekalu. Hili litafanywa na majeshi ya Ummah chini ya uongozi wa Imamu wa Waislamu ambaye wanapigana na kujilinda nyuma yake.
Hivyo basi, ondosheni vazi la khofu, uoga na kujisalimisha kwa tawala zilizopo na badala yake zihesabuni kwa kuendeleza utepetevu wa kuwaacha wanadamu kuporwa ardhi na hadhi zao na linganieni majeshi ya Waislamu na sio mashirika ya kimataifa. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
﴾وَلاَ تَرْكَنُواْ إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُواْ فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللّهِ مِنْ أَوْلِيَاء ثُمَّ لاَ تُنصَرُونَ﴿
“Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, wala tena hamtasaidiwa.” [Hud: 113].
Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
21 Dhu al-Qi’dah 1440 Na: 1440 H / 037
Alhamisi, 01 Agosti 2019
Maoni hayajaruhusiwa.