Kupuuzwa Kwa Elimu ya Dini ni Athari ya Fikra za Kibepari
بسم الله الرحمن الرحیم
Katika nidhamu ya kibepari kipimo Ni maslahi tu, Hufanywa Jambo au huachwa kwa mujibu wa faida kubwa itakayopatikana kwa muhusuka pia huachwa Jambo kwa kuhofia kupata ghasara katika Jambo hilo.
Kumezuka tatizo kubwa ambalo limeota mizizi katika jamii ya Kiislamu kuhusu watoto wa Kiislamu kutokuisoma dini yao ipasavyo na kukimbilia katika kusoma masomo ya secular zaidi.
Na Jambo hili lina msukumo katika upande wa serikali moja Kwa Moja kwa kuwaaminisha na kunasibisha elimu ya secular na upatikanaji wa ajira na riziki Jambo ambalo limewaathiri mpaka wazazi wa Kiislamu wakasahau kwamba riziki anaetoa ni Allah
Lakini pia elimu ya dini haijapewa uzito katika mabongo ya watoto wa Kiislamu kifikra chukulia mfano mtoto anapokwenda shule muonekano wake na anapokwenda madrasa ni tofauti kabisa
Shule atapewa nguo nzuri, begi, viatu hata pesa ya kununua chochote atakapokuwa shule atapewa lakini anapokuwa anaelekea Madrasa hata nguo zake achilia mbali kuwa hazikunyooshwa hata kufuliwa pia hazikumbukwi, Hali kama hiyo kifikra mtoto lazima apendelee sana kwenda shule kuliko Madrasa
Pia katika Suala la ufuatiliaji upande wa wazazi utakuta mtoto asipokwenda shule ataulizwa na hata kuadabishwa na akifanya vibaya katika masomo pia lakini Madrasa haulizwi lolote.
Na upuuzwaji mwingine wa masomo ya dini upo katika kuwapuuza na kuwadharau Walimu wa madrasa, unakuta ada ya mtoto madrasa ni ndogo lakini hapewi na mzazi kwenda kumpatia Mwalimu wa madrasa Jambo ambalo linamrudisha nyuma mwalimu katika ufundishaji kwasababu yeye kama binadamu ana mahitaji yake ya msingi inabidi ayapate lakin kaamua kutenga muda wake kusomesha dini haileti maana nzuri ikiwa hata kile kidogo asikipate .
Hayo yote yanaukumba ummah wa Kiislamu kutokana na kufuata kipimo cha mabepari cha maslahi.
Historia ya Kiislamu inaonyesha kuwa Uislamu ulipiga hatua kubwa katika maendeleo ya Elimu na hayo yalifikiwa baada ya Dola ya Kiislamu kuweka sera ya Elimu iliyowapata Wachamungu na Wasomi katika Nyanja zote Mfano Imam Abu Hanifa katika Nyanja ya fiqh, Ibn Al Haytham katika Fizikia n.k
Serikali ya Kiislamu pekee ndio inayoweza kuweka mfumo mzuri wa elimu na watu wakaweza kuwa wasomi katika Nyanja zote
Bin Rama
Maoni hayajaruhusiwa.