Miaka 98 Hijria Tangu Kuvunjwa kwa Khilafah: Mpaka Lini Tutabakia Mayatima?
بسم الله الرحمن الرحيم
Wanadamu jumla na hususan Waislamu wanaendelea kupaza sauti za vilio kutokana na tabu na majanga wanayopitia kama mayatima wasiokuwa na mlinzi wala ngao tokea Rajab 1342 Hijria ambapo Dola ya Kiislamu ya Khilafah ilipovunjiliwa mbali na wakoloni Wamagharibi wakiongozwa na dola kubwa na zenye usemi wakati huo: Uingereza na Ufaransa. Uyatima huu unaendelea hadi leo ambapo Marekani ndio kinara wa ulimwengu na anaendeleza njama na mipango ile ile waliyo kuwa wakitekeleza dola kubwa kabla yake!
Kila nyanja ya maisha imekumbwa na sintofahamu na muozo kutokana na utekelezwaji wa mfumo batili wa kisekula wa kirasilimali ambao una thamini maslahi/manufaa kuliko ubinadamu. Kwa mfano Barani Afrika, Ulimwengu wa Waislamu, nyanja ya kisiasa kwa mujibu wa nidhamu ya kidemokrasia imesheheni viongozi vibaraka na walafi wanaotumia damu za watu kama ngazi ya kuingia au kubakia mamlakani. Viongozi watiifu ambao kibla chao ni London, Washington, Paris n.k na ambao daima wanakwenda mbio kutekeleza kwa ukamilifu sheria wanazotungiwa na mabwana zao wakoloni na kisha kuziidhinisha kupitia mabunge au mabaraza yao tiifu wanayomiliki! Sheria hizi kiinje zimekitwa katika sura ya kuinua na kuboresha maisha ya raia jumla lakini kiundani zimelenga kuendeleza ukandamizaji wa raia jumla! Baya zaidi ni kuwa zina kwenda kinyume na matakwa ya Muumba wa viumbe! Umwagaji damu hususan za Waislamu kwa kisingizio cha vita dhidi ya misimamo mikali na ugaidi vinaendelea mpaka leo hii ndani ya China (Xinjiang), Syria, Kashmir, Burma, Afghanistan, Palestina, Pakistan, Iraq, Uturuki, Urusi, Uzbekistan n.k!
Nyanja ya kiuchumi kwa mujibu wa urasilimali imetiwa kitanzi na sera kandamizaji zinazo hakikisha kuwa ardhi zenye rutuba na mali ghafi zimehifadhiwa na kumilikiwa na wakoloni kupitia makampuni yao yanayo pora usiku na mchana. Ilhali makampuni haya ya kikoloni hayatozwi ushuru na lau yatatozwa basi utakuwa ni wa kiwango cha chini eti kwa kisingizio cha kupunguza gharama kwa “muwekezaji” ambaye baada ya uporaji huo hutengeneza bidhaa ng’ambo na kisha kuzileta kutuuzia kwa bei ghali mno! Kuongeza msumari wa moto kichwani kwa raia; badala ya serikali kupatiliza rasilimali ilizoruzukiwa na Mwenyezi Mungu katika ardhi yake wao wanakwenda mbio kuhakikisha inawatoza raia ushuru wa kupindukia kiasi kwamba jukumu la raia ni kama ng’ombe asiyekwenda malishoni lakini kila kukicha anakamwa maziwa!
Nyanja ya kijamii imedidimia na kuwa chini kabisa kuliko hata wanyama. Hii ni kutokana na nidhamu ya kiuhuru/kiliberali inayo lazimisha dola za kisekula kwenda mbio kuhakikisha kwamba uhuru wa kibinafsi na wa kingono umechukua dori kubwa katika mujtama. Leo hii kila mtu afanya apendavyo wakati wowote mahali popote kiasia kwamba tumeshuhudia kwa mfano mahusiano ya kingono: mama na mwanawe, baba na bintiye, ndugu kwa ndugu, wanaume kwa wanaume, wanawake kwa wanawake, watu na wanyama n.k. Ufuska na uhayawani umepelekea ndoa, familia na majumba kusambaratika na wakati huo huo kupelelekea kukosekana kwa furaha miongoni mwa wazazi, watoto na watu jumla kwa kuwa mafungamano yao ni ya kimaslahi/manufaa (madaniyyah) pekee!
Nyanja ya kielimu imekuwa ni sekta ya usanii wa kutengeneza vyeti ili vimilikiwe kwa ajili ya utafutaji wa ajira tu! Lakini sio tena sekta ya kukuza wanafikra na wanamapinduzi wanaokwenda mbio kuhakikisha mujtama na taifa lao linapata suluhusho kwa kila tatizo linalochipuza kwa mtizamo safi wa kindani unaotoka kwa Muumba wa viumbe. Ndio maana leo hakuna tofauti kati ya Professa (shoga) na Daktari (msagaji) n.k wote kiuhalisia ni wajinga kwa kuwa wote hadhi yao iko chini zaidi tukiwalinganisha na wanyama lakini kivyeti ni wasifiwa na wakuigwa kwa kuwa ndio walio kileleni kielimu! Suali ni je, tutarajie natija gani katika mujtama ikiwa hawa ndio mifano ya kuigwa?
Uyatima huu lazima usitishwe kwa ukamilifu, si kwa kutia dua misikitini pekee bali kwa kufanya kazi usiku na mchana kwa hali na mali. Kazi yenyewe iwe ni ya kisiasa ndani ya chama ambacho mfumo wake ni Uislamu na kazi yake ni siasa. Chama chenyewe ni Hizb ut Tahrir ambacho tokea mwaka 1953 kilipotangaza wazi kazi yake ya kurudisha tena maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha Serikali ya Kiislamu ya Khilafah kwa njia ya Utume. Hadi leo ni miaka 66 tangu Hizb ut Tahrir itangaze kazi yake wazi, inaendelea kusonga mbele kwa kasi mno licha ya kelele za wanaolaumu miongoni mwa viongozi mafasihi na wandani wao katika wajinga. Hakika safari ya kuleta mabadiliko kwa Ummah wa Kiislamu na ulimwengu jumla imekaribia ukingoni. Uyatima umekaribia kutiwa ndani ya kaburi la sahau kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu (swt) hivi karibuni kwa kusimama tena Khilafah Rashidah itakayoongozwa na kiongozi Khalifah muadilifu anaye wahurumia na kuwaombea dua njema raia wake nao wakimhurumia na kumuombea dua njema. Khilafah itakayo wakomboa Waislamu na wanadamu jumla popote walipo kutoka katika utumwa wa kumuabudu binadamu kupitia sheria zake anazozitunga kwa akili yake hadi kumuabudu Mwenyezi Mungu (swt) kupitia kutekeleza Shari’ah (Qur’an na Sunnah) yake kwa ukamilifu katika nyanja zote za maisha ikiwemo kiasiasa, kijamii, kiuchumi, kielimu n.k. Hakika Khilafah ndio Mlinzi na Ngao Yetu.
Patiliza fursa usiwachwe nyuma au nje ya mchakato huu adhimu wa kihistoria ambao malipo yake mbele ya Mwenyezi Mungu (swt) ni makubwa mno hapa duniani pamoja na kesho Kiyama. Ilhali usisahau kuwa Kifo na Rizq ziko mikononi mwa Mwenyezi Mungu (swt) na hazitegemei kulingania au kunyamazia haki kattu.
Ali Nassoro Ali
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya
Makala Na.36: Ijumaa, 8 Rajab 1440 | 2019/03/15
Inatoka: http://hizb.or.ke/…/miaka-98-hijria-tangu-kuvunjwa-kwa-khi…/
Maoni hayajaruhusiwa.