Mauaji Ya Waislamu New Zealand: Matokeo Ya Uadui Wa Nchi Za Magharibi Kwa Waislamu Na Uislamu

Hizb ut Tahrir Tanzania tunalaani kwa nguvu zote mauaji ya kigaidi, dhulma na ya kikatili ya Waislamu 40 na majeruhi wasiopungua 20 wakiwa ndani ya Misikiti miwili, Masjid Al Noor na Msikiti wa Linwood yote ya mjini Christchurch, nchini New Zealand.

Kwa kuwa Ummah wetu ni Umma mmoja tunaungana na ndugu zetu Waislamu wa New Zealand kwa kuwapa mkono wa ta’azia kwa msiba na janga hili kubwa.

Tunamuomba Allah Taala katika siku hii tukufu, ndani ya mwezi huu mtukufu Awaingize madhluom wote (waliodhulumiwa) katika pepo ya darja ya juu ya Firdaous. Pia na majeruhi nao Awape shifaa. Amiin

Japo matukio haya yametendwa na watu binafsi, na litakaririwa sana na vyombo vyao vya habari kuwa watendaji ni wabaguzi wa siasa kali, lakini ukweli utabakia kwamba wao wametenda hayo kutokana na msukumo wa matendo ya uadui ya madola yao na madola ya kimagharibi kwa jumla, pia na fikra za kiuadui dhidi ya Waislamu zinazopandikizwa kila mahala chini ya uongozi wa Marekani kwa kushirikiana na nchi mbalimbali ikiwemo New Zealand na Australia (ambayo mmoja wa watuhumiwa wa mauaji haya ni raia wao)

Fikra za uadui dhidi ya Uislamu na Waislamu huenezwa na wanasiasa wao, vyombo vyao vya habari nk. na kimsingi zimeathiri kila mahala mpaka nchi zetu changa ikiwemo Tanzania ambapo leo kuna mahabusu Waislamu kwa mamia kama sio maelfu kwa kesi za kubambikiziwa kwa dhulma kwa kudandia farasi wa sheria ya ugaidi, kesi ambazo hazisikilizwi.

Vipi raia wa nchi za magharibi na kwengineko wataheshimu Uislamu na Waislamu ilhali anaona wazi namna nchi zao zinavyodhalilisha Waislamu, kuwaua , kudhalilisha wakimbizi wa Kiislamu, kuwafutia uraia Waislamu, kuvunja misikiti yao, kubariki kupigwa na kudhuriwa kwao kama ndani ya Yemen, Palestina nk, kuwavunjia heshima zao, bila ya kusahau kuvamia na kupora ardhi za nchi zao, kama ndani ya Iraq, Afghanistan, Somalia nk.

Matukio haya kiuadui nchini New Zealand na dunia nzima ni yenye kutarajiwa kutokana na propaganda chafu za nchi za magharibi dhidi ya Uislamu. Na kauli za viongozi wa nchi za magharibi kulaani mauaji haya si chochote bali ni machozi ya mamba, au kauli ya Waziri mkuu wa New Zealand bi. Jacinda Ardern kusema :
“Leo ni siku nyeusi kwa New Zealand” ni kejeli kwa Ummah wetu na kamwe kauli hizo hazitowatakasa na ukatili huu mpaka pale watakapobadilisha sera na uoni wao wa kiuadui kwa Waislamu na kubadilisha siasa zao za nje katika maamiliano yao na Waislamu na nchi zao.

Katika mwezi huu wa Rajab ulioangushwa dola ya Kiislamu ya Khilafah, msiba huu wa mauaji haya ni kumbusho ziada juu ya unyonge na udhaifu wetu kwa kukosekana ngao yetu.

Inna llilahi wainna ilayhi rajiuun

15 Machi 2019

Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Tanzania

Maoni hayajaruhusiwa.