Kuukumbatia Mfumo Wa Kirasilimali Ni Kama Kujidunga Mwiba
Husikika malalamishi mengi kutoka pembe zote duniani kuhusu kudhalilishwa na kunyanyaswa kwa wanawake. Wengi hujitokeza kuzungumzia mwanamke mara husemwa anatumiwa vibaya kwa kufanywa mtumwa wa nyumbani na mara anadhulumiwa haki zake. Haikuishia tu misemo bali kukaundwa tume mbali mbali za kuweza kumtetea na ati kumkomboa huyu mwanamke chini ya kauli mbiu ‘haki za mwanamke’. Mbali na haya, kuawekwa tarehe maalumu duniani nayo ni tarehe 8 Mwezi March kila mwaka ijulikanayo siku ya wanawake. Kwenye siku hiyo makongamano huandaliwa kuzungumzia Mwanamke. Mara nyingi huambiwa kuwa lazima mwanamke apewe nafasi ya kisiasa na kiuchumi na kadhalika hivyo akapewa mpaka nafasi katika serikali kinyume na ilivyokuwa hapo awali.Licha ya tume hizi nyingi na nafasi waliopewa ya kuwa na wawakilishi wao katika serikali, malalamishi haya bado ni yenye kuendelea.
Matatizo yanayomkumba mwanamke ni kwa kukosa kwake fadhila,mwanamke amekuwa mwizi wa fadhla.Ni matatizo haya haya aliyopata mwanamke katika zama za kijahilia, idhilali hizi hizi aliweza kupitia mwanamke kutoka kwa wanaume na jamii kwa jumla.Mwanamke aliteswa kuteswa na Majahili.Lakini Mtume (SAW) alipokuja na nuru (Uislamu) katika jamii,nuru iling’aa sana kwa mwanamke na kutoka katika giza la idhilalai lililokuwa limemgubika.
Fikra matata “Gender equality” –usawa wa kijinsia ati mwanamke ni sawa na mwanaume hupigiwa mnada na wamagharibi na wanawake wengi wameinunua. Fikra hii humaanisha kuwa mwanamke asiwe na mipaka katika mambo yake ashindane na mwanaume kwa kupigania ngazi za utawala, afanye kazi na kadhalika. Kulingana na mfumo wetu wa Uislamu ni kuwa ameweka wazi majukumu ambayo jinsia zote hutekeleza kama waja wa MwenyeziMungu pasina na kuangalia ujinsia. Mwanamke anawajibika kuswali, kutoa zaka, kuhiji na kufanya daawa kama inavyowajibika kwa mwanaume. Hata hivyo, kimaumbile Mwenyezimungu akamvua mwanamke kwa baadhi ya majukumu Fulani kama uongozi hawezi mwanamke kuwa mtawala. Kulea watoto tokea kushika mimba, kunyonyesha na mfano wa hayo hizi ni hukumu maalumu kwa wanawake. Ama masuala ya kufanya kazi ni kuwa Uislamu hakumharamishia mwanamke lakini jukumu la kusimimamiwa malazi, lishe na nguo limetwikwa wanaume wa Kiislamu. Hivyo ndivyo Uislamu ulivyomlinda na kumuekea haki sahihi kulingana na maumbile yake.
Wanawake waliotutangulia walijifahamu wao ni kina ani,wanatoka wapi na ni wapi wanakoelekea.Walipotambua ni wapi wanapoelekea walijitahidi kujiandaa nako.Ndio maana baada ya kufwata sheria za Allah na Mtume saw hatukusikia tume yoyote imeundwa kwa ajili ya kumtetea mmwanamke haki zake. Walitoshekwa na sheria za Allah.Kinyume na Mwanamke leo, amezipuuza sheria za Allah na kujigubika katika giza totoro la utwaghuti.
Giza ambalo hata kukawashwa taa ngapi”tume”,halitabadilika na kuwa nuru. Wanawake wa sasa wamekuwa wezi wa fadhila, baada ya kukombolewa na kustiriwa na Uislamu,leo wanafanya mambo kinyume na Uislamu huo. Shida,dhiki na mateso ya ujahiliya yamemrudia huyu mwanamke, lakini ujahilia wa zama hizi na matazizo yake,mwanamke amejitakia. Ameona njia mbili na akaamua mwenyewe kufuata njia ya kombo na kuacha iliyonyooka akiiona kuwa ndefu sana,huenda ikamchelewesha katika safari yake au kutomfi kisha kabisa.
Aidha wanawake wa zama hizi wameathiriwa na tamaduni mbovu za kimagharibi. Chini ya miito potofu ya kisekula kama vile ‘my dress my choice’ , uhuru wa kutangamana, pamoja na uhuru wa kibinafsi imewafanya wawawake leo kutojitambua wao ni kina nani,wanatoka wapi na wanakoelekea. Ama wale ambao kikusudi hawataki kujifunga na mafundisho bora ya Uislamu ndio urasilimali unawadhalilisha kiasi cha kutisha!
Kwa hakika thamani yake mwanamke inabaki kwenye vitabu na hadithi za bwana Mtume (saw) lakini thamani hii mwenyewe Mwanamke haitaki. Na hii ndio maana sisi kama wanawake wa Kiislamu, wanawake wa chama cha Hizb ut-Tahrir, ,tunasema dhiki hizi mwanamke zimesababishwa na kukubali kwetu kuishi chini ya fikra na mfumo hatari wa Kimagharibi wa kirasilimali. Lau hatutojifunga na Uislamu wetu basi ni mwiba wa kujidunga ambao siku zote pole huwa hauna. Tuna imani hakuna tume itakayoweza kumtetea mwanamke na kumuekea haki zake kama zilivyowekwa na Qur’an. Mwanamke aache kujidunisha na arudi katika Kitabu na Sunnah za Mtume (saw) na giza hili litapotea na watang’ariwa na jua na mwangaza wa Uislamu. Allah(swt) ametuonya kuwa mwenye kuacha utajo wake atampa maisha ya dhiki, mwanamke.
Mgeni J. Sali
Inatoka Jarida: 2 https://hizb.or.tz/2017/03/01/uqab-2/
Maoni hayajaruhusiwa.