Inatosha Kuwadanganya Watu…Nani Anaenufaika na Ugaidi ?!
Tangu dakika ya kwanza ya mashambulizi ya mabomu mnamo jumatatu, ambayo ililenga zaidi walinda usalama wa katikati ya mji, na kabla ya kusubiria uchunguzi wowote ambao ungebaini wanaohusika na malengo yao, kundi la waandishi wa habari na baadhi ya watu wakatengeneza vijimaelezo vya tukio hili na kutumia kupiga uislamu, wakati huo serikali ya Tunisia na mihimili yake wakawa dhidi ya uislamu mfano shule au madrasa zinazofundisha qur-an sunnah (hizi ni shule maalum ya kidini)
Sisi Hizb ut Tahrir / Wilaya ya Tunisia tumewaonya watu wetu nchini Tunisia, tangu mwanzo wa matukio haya ya kihalifu, kwamba wanalengwa na hali ya joto la kisiasa, ili waonekani kama wao ndio sababu ya viongozi kufeli na kushindwa katika utawala, au kutengeneza hali ya mgawanyiko. Tunaweka wazi mara nyingine tena kazi hii mbovu na kutumia matukio haya katika siasa kwa ajili ya kutengeneza mazingira ya ongezeko la kiulinzi nchini dhidi ya watu na sio kwa ajili ya kuuhami ummah kitu ambacho kimeendelea kua ni mzizi wa ufisadi na utegemezi.
Na hivyo sasa tunawaonya wanasiasa kwa kufeli kwao na kushindwa kuleta mbadala wa kuondoa matatizo ya watu. Na kikubwa kilichobakia kwao ni kutengeneza mazingira ya kuendelea kula na kuishi kwa kuwafanyia uadui na kuwapiga watu na uislamu, na kutumia sheria za uhalifu kama daraja la kufanyia mambo yao, na tunathibitisha kwamba siku ya hesabu ipo karibu, kwa sababu damu ya waislamu katika ulinzi na wasiokua na hatia (raia) haiwezi kumwagika bure, kwa sababu:
«لَزَوَالُ الدُّنْيَا أَهْوَنُ عَلَى اللَّهِ مِنْ قَتْلِ رَجُلٍ مُسْلِمٍ»
“Kuondoka kwa ulimwengu ni jambo dogo mbele ya Allah kuliko kumua muislamu”
[Tirmithi].
Media Office of Hizb ut Tahrir in Wilaya ya Tunisia
Jumatano , 22nd Safar 1440 AH – 31/10/2018 CE
No.: 1440 / 05
Imetafsiriwa kutoka:
https://www.facebook.com/646683775466624/posts/1452617178206609/
Maoni hayajaruhusiwa.