Mazingatio Kwa Maji Ya Zam Zam

Wakati kama huu wa kurejea ndugu zetu Mahujaji, wengi wetu amma hupatiwa au huwataka mahujaji watupatie maji matukufu ya kisima kitukufu cha zamzam kilichoko Makkah.

Ni muhimu tufaidike na maji hayo kwa kuwa yana utukufu na kheri kubwa kama tulivyoelezwa na Mtume SAAW.
Hata hivyo, tunahitaji kufungamanisha maji ya kisima cha zam zam kwa mazingatio ya undani. Baadhi ni kama yafuatayo:

1. Bi Hajar, mama wa Nabii Ismail As, wakati mtoto wake (Ismail ) akiwa mchanga aliwekwa jangwani na Nabii Ibrahim As. katika bonde la jangwa la Makka. Wote yeye na mume wake waliipokea jambo lile kwa moyo mkunjufu kwa kuwa ilikuwa ni amri ya Allah Taala. Licha ya kuona kwa kipimo cha binadamu kana kwamba ni usumbufu

2. Bi Hajar, licha ya kumtegemea Allah Sw kwamba yeye na mtoto wake hawatoachwa mkono na Mwenyezi Mungu, lakini bado alihangaika huku na huko kutafuta maji kabla ya Allah Taala kumbubujishia maji ya kisima cha zam zam.
Maana yake ni kuwa, katika kumtegemea Allah Taala lazima Muumini achukuwe hatua katika mzunguuko wake wa kibinadamu.

3. Allah Taala ni Mwenye kufikia jambo lake alitakalo. Ismail As alikulia Makka akaowana na watu wa pale, na kikaendelea kizazi chake mpaka akatoka ndani ya kizazi hicho Mtume wetu Muhanmmad SAAW.

#UislamNiHadharaMbadala

Maoni hayajaruhusiwa.