Tunakataa Mapatano na Katili na Mchinjaji wa Ash-Sham, na Tunamuachia Allah Mwisho Wake.

(Imetafsiriwa)

Habari zinaeendelea kusambaa na kuvuja muda baada ya muda kwamba kuna mawasiliano kati ya viongozi wakubwa wa Lebanon na viongozi wakubwa wa utawala wa Syria ! hakuna uthibitisho wala upingaji wa wazi kuhusu mawasiliano hayo kutoka kwa wahusika ! Hii inahusu zaidi waislamu wa waliopo lebanon kuhusu muelekeo wa serikali yao na utawala wake katika ngazi za juu pia ni kuhusiana na utawala wa Baath na familia ya Assad na watu wake wa karibu, ambao uhalifu wao haujathibitishwa ndani ya Syria pekee, bali uhalifu wao umethibitishwa nchini lebanoni kupitia viongozi na wanasiasa. Pia imebainika kwamba wanapeleka watu lebanon wakiwa wamebeba milipuko wakiwa na mipango ya mauaji, mpango huo hujulikana kama “mpango wa samaha-mamluki.

Kwakua jambo hili bado ni uvumi, sisi katika Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Lebanon tunaionya dola ya lebanon kutojaribu kuliendea jambo hili ambalo ni kama  kuijaribu nguvu ya maji kama jambo hili litarasimishwa…habari hizi zimeonekana ni nzuri kwa kuzingatia harakati za kinchi ambazo zimekua zikilalamikia uadui wao dhidi ya Assad na utawala wake, pia mfano wa Marekani na uvamizi wa mazayuni ambavyo katika masiku haya wameonekana wakitafuta majina mazuri ili kuudimisha utawala wa Assad  na mtoto wake na kumsaidia kupitia washirika, wasaidizi na ushirika wa kificho ili kuwadhibiti watu wa syria mara nyingine baada ya kuwatesa, kuwaua na kuwaharibia na kuwahamisha makazi yao. Ili waweze kuwarejesha walinzi wa mpaka wa mayahudi kama ilivyokua katika miaka kadhaa iliyopita!!! Tunaikumbusha serikali ya Lebanon kwamba waislamu wa Lebanon, ambao ndio msaada mkubwa wa waislamu wa Syria wale waliobaki na wale na wale waliofukuzwa katika makazi yao hawatakubali makubaliano yoyote na utawala wa kihalifu wa Syria kwa ajili eti ya maslahi ya Lebanon. Maslahi ya lebanon hayatakiwi kuhusishwa na mhalifu na wasaidizi wake. Mawasiliano ya asili yanapaswa kuwa kwa watu wa Syria na wale kutoka kwa wao ambao wamepaza sauti zao kwa ajili ya kumuondoa katili, na viongozi wa Lebanon na wale wanahusishwa na kauli ya Allah (swt) isemayo:

﴾ وَإِنَّ الظَّالِمِينَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْ ض)

“Kwa hakika madhaalim wana ungana miongoni mwao”

[Al-Jathiya: 19].

Kwa kusambaa huko kwa habari, kabla ya kuthibitishwa, tunahakika watu wa Lebanon wataukataa muelekeo huu uliokatazwa na sheria na ulikataliwa na wengi katika watu wa Lebanon. Tunahakika kwamba yoyote atakayemsaidia dhaalimu basi yupo pamoja nae na nilazima ahesabiwe vyovyote itakavyokua. Tunatoa shukra za dhati kwa waislamu wa Lebanon, na waliohamishwa kutoka katika makazi yao watu wa Ash-Sham, tunahakika ma ahadi ya  Allah (swt), alietuambia batili haita dumu haijalishi itakaa kwa muda gani. Madhalimu wamelaaniwa na ni wapotevu katika hii dunia hata baada ya hapa watapata adhabu iumizayo akhera. Na bado tunaendelea kulingana na amri ya Allah katika kuukumboa ummah kutoka kwa hawa wauaji, hatutasita kusema ukweli na kusaidia hadi tutakapo ifikia ahadi ya Allah, huku tukitaraji ushindi wake na msaada wake, kama alivyosema Allah(swt):

وَاللَّهُ وَلِيُّ الْمُتَّقِينَ

 “…walakini allah ndio mlinzi alie madhubuti”

[Al-Jathiya: 19].

 Ofisi ya habari ya  Hizb ut Tahrir  Wilayah ya Lebanon

 

Maoni hayajaruhusiwa.