Madeni Ya Riba Yaiangamiza Pakistani

Inachekesha kiasi gani eti ngome ya madeni kuwa dola ya madina !!?
Muungano unaongozwa na Saudia kwa ajili ya kupambana kwa niaba ya Amerika ni muungano batili (haramu) katika uislamu sasa kwa nini unazidisha tafrani ?
Hata ubinafsishaji uzidi kiasi gani Pakistani hautaweza kukwamua nchi katika madeni
Inachekesha kiasi gani eti ngome ya madeni kuwa dola ya madina?!
Akizungumza kwa mara ya kwanza katika mkutano na vyombo vya habari baada ya uchaguzi mnamo tarehe 8 mwezi wa 8, Waziri mpya wa fedha anaependwa Asad Umar alisema kwamba kutoa msaada au ruzuku yoyote katika siku 100 za mwanzo ni kama kuwalambisha pipi. Alisema siku100 za mwanzo hazingeonyesha tu maamuzi ambayo yangebadilisha mustakbali wa nchi bali ni “mwelekeo usio na shaka wa kile tulichoahidi.” PTI wanapata tabu kuhusu chaguo la mwelekeo wao na ndio maana Asad Umar anasema, “uhalisia ulivyo hatuna namna ya kuchagua chaguo moja bali tunatakiwa kupanga machaguo yote katika mstari machaguo hayo yanajumuisha msaada wa IMF ndani ya wiki sita.” Kwa kutizama namna ya madeni mengine, kiongozi wa PTI alisema Sukuk bond na Eurobond ziliwekwa katika mjadala kwa mara nyingine, ingawa hundi hizo zilisababisha matatizo makubwa ya kifedha ikiwa ni pamoja na kudorolesha uchumi.

Kama zilivyo nchi nyingine , Pakistani imeendelea kupata tabu katika mikono ya IMF kupitia program 12 zilizopita tangu mwaka 1980. Zaidi ya hayo, madeni kutoka china yameruka mipaka hadi kutishia muanguko wa uchumi wa nchi unafikia dola 6.6 billion.
Tayari Pakistani imeshatumbukia katika mtego au dimbwi la madeni,deni lake la nje na baadhi ya mali vinafikia dola za kimarekani bilioni 92. Na bado inakopa tena kwa ajili ya kulipa madeni ya awali. Na itazidi kuwa na hali mbaya kwa sababu utawala mpya unaendeleza kufata kanuni zile zile za riba zililoshindwa. Shirika la fedha la kimataifa (Imf) ndio limekadiria madeni yote haya ya ndani ya Pakistani yatafikia dola bilioni 144 katika miaka mitano ijayo kutoka dola bilioni 93 katika mwaka wa fedha wa 2018.
Zaidi ya hayo, madeni kutoka taasisi za nje kama IMF na Benki ya dunia sio tu yanaongeza mzigo wa kila mwaka wa madeni lakini kushirikiana na taasisi za fedha za kikoloni imepelekea uchumi wa Pakistan kudorora na kuzorota na kusababisha kodi kubwa katika nishati, madini, usafirishaji, mawasiliano na viwanda vizito kupitia kasi ya ubinafsishaji na hivyo kupelekea muanguko usioepukika wa kodi, IMF inahitaji zaidi uondoshwaji wa kodi ,ambao unaathiri viwanda na kilimo na kubana matumizi.
Jee ni vipi haya yote yatapelekea Pakistani kuwa mfano wa dola ya madina ? Pia Mtume (saw) hajawahi kuchukua mkopo wa riba kutoka kwa maadui wa kikuraishi ili apate nguvu madina.

Waislamu ni lazima wajifunge katika kuhudumia uislamu kutoka viongozi waliopo kwenda utawala wa kiislamu kwa kufahamu kwamba uislamu unahitaji kutabikishwa, na hilo ndio jambo pekee litakalonusuru mabilion ya fedha.
Uislamu unahitajia urejeshwaji wa mali na utajiri kwa wale wote waliotawala Pakistan wakati uliopita. Hii ni kwa sababu katika uislamu mtawala haruhusiwi na shughuli za kibiashara na amewekewa mipaka katika mapato yake ya mwezi. Hivyo kama atakua tajiri ghafla katika wakati wake wa uongozi kile kitakachozidi katika mali zake kitarudishwa katika hazina ya dola. Dimbwi hili la utajiri lipo katika mtiririko wa mabilion ya dhulma ya dola, na nikawaida kwa Pakistan kila kiongozi aliopo madarakani kujitajirisha kwa kufanya ufisadi katika mifuko na taasisi za kifedha kwa kuchukua mikopo kwa kutumia jina la nchi. Pia dola la khilafah haiwezi kulipa kiasi chochote katika madeni kwa riba na hii yatokana na kauli ya Allah (swt) kwa kuitaja riba kuwa ni haram
وَأَحَلَّ اللهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبَا
“Wanasema riba ni katika biashara.lakini amehalalisha biashara na ameharamisha riba.”
[Surah Al-Baqarah 2:175]

Riba ndio imeifikisha hapa Pakistani, kama ilivyofanya katika nchi nyingine, imelipa madeni ya mikopo lakini imeendelea kubaki katika chaka la madeni. Na kama haitoshi bado ipo katika kulipa mabilioni ya madola ambayo yatatafuna sehemu kubwa ya bajeti yake.pia Khilafah katika njia ya Utume itakwenda haraka katika ardhi za waislamu ili kuwaunganisha waislamu chini ya dola moja na kuhakikisha kwamba nishati na madini ni mali ya ummah kama vile uislamu ulivyoagiza. Hii itamaanisha kwamba mabilioni ya pesa yanayotumiwa katika uagizaji wa nishati itakua ni jambo la kihistoria kwa sababu waislamu watakusanya rasilimali zao katika dola moja yenye nguvu,chini ya kiongozi mmoja tena chini ya hazina moja.

Muungano unaongozwa na Saudia kwa ajili ya kupambana kwa niaba ya Amerika ni muungano batili (haramu) katika uislamu sasa kwa nini unazidisha tafrani ?
Mahakama kuu iliarifu mnamo tareh 7 mwezi wa 8 2018 kwamba kiongozi wa zamani wa jeshi Gen Raheel Sharif hakupata kibali maalumu kiitwacho (NOC) kutoka baraza la shirikisho kabla ya kuondoka Saudi Arabia kwenda kukusanya majeshi ya mapigano.

Vivyo hivyo, katibu wa ulinzi alistaafu Lt Gen Zamirul Hassan aliitarifu mahakama kuwa wizara ya ulinzi ndio yenye mamlaka ya kutoa NOC kwenda kwa chief wa zamani wa jeshi baada ya makao makuu kuhakikisha kukikubali na kupokea kibali. Kwa hakika Pakistan kisha waziri wa ulinzi ,Khawaja Muhammad Asif, mnamo 6 /1 /2017 alithibitisha kwamba chief wa zamani wa jeshi, General (retd) Raheel Sharif, alifanywa kuwa ni chief wa muungano wa vikosi maalumu kwa ajili ya kupambana na “ugaidi” na baada ya hapo hatua ikawa imepigwa kwa msaada wa serikali. Baada ya kuzisikiliza pande zote, mahakimu watatu waliokaa katika sc wakiongozwa na jaji mkuu wa Pakistani (cjp) Mian Saqib Nisar waliagiza kwamba jambo hilo lipelekwe katika baraza la shirikisho . Aliongeza kwamba jambo hilo lilikua ni zito kiasili lakini bado usikilizaji uliahirishwa hadi siku ambayo haijatajwa baada ya likizo ya kiangazi.
Hivyo baada ya miezi 18 tangu uthibitisho wa wizara ya ulinzi kufanyika wa kumuidhinisha generali Raheel kama chief wa muungano wa majeshi yanaongozwa na saudia mfumo wa mahakama haueleweki. Hata ingawa jambo hili lilishawekwa mbele ya majaji, kama ingelikua ni mfumo wa kimahakama unaongozwa na uislamu basi ingelikua ni wazi dunia nzima. Majeshi ya msalaba yanalengo la kuua muamko wa ummah huu ili kuchelewesha kuanguka kwa vidola hivi na kurejea kwa khilafah kupitia njia ya Utume kwa ujumla.

Bado, Democrasia inawaruhusu viongozi waliopo katika biladi za waislamu kwenda mbio kujitolea katika majeshi kujumuika katika makundi ya kikanda na kiuimwengu kwa ajili ya kuwasaidia mabwana zao wakoloni
Democrasia imepitisha sheria kulazimisha ummah kukubali tabia zote za kinyama dhidi yake, iwe ni uchinjaji wake wa dhahiri, utekaji wake wa ardhi au iwe ni ukataji wa kutawaliwa na uislamu chini ya kivuli cha dola moja la khilafah.
Democrasia imeruhusu mawakala kwenda mbio kusaidia jeshi la msalaba la kimagharibi ambao wamefeli kuungoza ummah kwa kutumia majeshi yao yaliojawa na uoga na kwa hivyo hivi sasa wanahitajia kuwatumia majeshi ya waislamu kwa ajili ya kufanya kazi zao. Na Allah (swt) amekataza kuungana au kusaidiana katika dhambi pale aliposema:

وَتَعَاوَنُواْ عَلَى الْبرِّ وَالتَّقْوَى وَلاَ تَعَاوَنُواْ عَلَى الإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَاتَّقُواْ اللّهَ إِنَّ اللّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ
“ Na mshikamane katika mema na uchamungu, nawala msishikamane katika maasi na maovu. Na mumuogope; kwa hakika Allah ni mwenye adhabu kali.”
[Surah Al-Maaida 5:2].
Haipo wazi kwamba ushahidi wa maovu uliowazi kwa uislamu unawezekana,kwasababu hatuna dola inayotawala kwa mujibu wa Qur-an na sunna

Hata ubinafsishaji uzidi kiasi gani Pakistani hautaweza kukwamua nchi katika madeni
Asad Umar, waziri wa fedha anaekuja wa Pakistan, katika mahojiano katika gazeti la financial Times mnamo tareh 2 mwezi wa 8 2018, aliweka wazi kwamba nchi isingelijumuisha ubinafsishaji mkubwa ufanywao ili kupata nguvu za kiuchumi kwa ajili ya kujikwamua katika mgogoro wa kiuchumi. Lakini hili litasaidia kuishawishi IMF kukubali kutoa mikopo mingine kwa ajili ya nchi .
Mpango wa ubinafsishaji mkubwa ulianzishwa na serikali ya Nawaz shariff mnamo mwezi wa 9 mwaka 1990.ilitangaza ubinafsishaji kama lengo la kwanza la sera ya kiuchumi iliunda tume ya ubinafsishaji mwaka 1991, na sheria ilioeleza asilimia 90 ya ubinafsishaji unaoendelea utatumika kumaliza madeni na aslimia 10 iliyobaki itatumika kupunguza umasikini .Tangu mwaka 1991 mpaka mwezi april 2006 serikali ilikua imekamilisha miamala 160 katika jumla ya mauzo ya Rs .395.241.bilioni. Pamoja na hayo, ubinafsishaji unaoendelea haujasaidia kupunguza madeni ya Pakistani wala kupunguza umasikini. Serikali inasubiria kudai tu kwamba itaifanya Pakistani kuwa kama dola ya madina, katika uhalisia imeshaonyesha kushindwa kwa mpango wake wa kibepari. Na mpango huu wa kibepari hauna tofauti na utawala wa kifisadi uliopita na hatua zake zitazalisha matokeo yale yale, madeni mabaya zaidi na umasikini mkubwa. Iwe Threek-i-insaf ya Pakistani inafahamu au haifaham kutabikisha uchumi wa kiislamu ambao ulitabikishwa katika dola la madina.

Waislamu wa Pakistani ni lazima washikamane na harakati ya mabadiliko ya kweli ya hizb ut tahrir, kwa ajili ya kurejesha dola ya khilafah kupitia njia ya utume. Hizb ut tahrir inazalisha na kutoa vitabu vinavyofahamisha uchumi wa kiislamu, uliotabikishwa na dola la madina, ikiwa ni pamoja “Nidhamu ya uchumi ya kiislamu” ” vyanzo vya mapato katika dola la khilafah” sera za kiuchumi za kiislamu” na “migogoro ya uchumi” uhalisia wao na suluhusho lao ni kutoka katika mtazamo wa kiislam” katika utangulizi wake katika katiba. Hizb ut tahrir ina makala 46 kuhusu uchumi mbali na makala 191 zilizo na ushahidi wa kutoka katika Qur-an na sunnah. ina mashabab wengi katika dunia nzima ambao wanaufahamu wa sawa kuhusu uchumi wa kiislamu na wanauwezo wa kutoa fatawa kuhusu mibadiliko yoyote katika uchumi inayohitajika. Hivyo mabadiliko ya kweli yanaweza kufikiwa na chama ambacho watu wake wanaelewa Qu-an na sunnah, wanaweza kufanya matumizi ya sheria ya kiislamu ya kiuchumi au jambo la lolote linalohusiana na maisha yetu kutoka katika Qur-an na sunnah na wanauwezo wa kuzitabikisha.
#UislamNiHadharaMbadala

Maoni hayajaruhusiwa.